Daah, huyu Mwamba atusamehe wale tuliompinga kwa nguvu zote.
Ni kweli kabisa wasomi ni tatizo kubwa sana linapokuja suala la uzalendo.
Ndio maana hata majeshi ya kule Nigeria yalishindwa kudhibiti Boko haramu kutokana na kuwa na wasomi wengi wabinafsi na waoga waliokua wanaogopa kukatwa shingo na Magaidi wa boko Haram ,mpaka Walipoanza kuajiri vijana wenye Elimu ya Kawaida ndipo walipoanza kuwadhibiti Boko Haram.
Wasomi wakiwa na Kiongozi Imra na anayeweza kuwafilisi na kuwafunga gerezani au hata kuwaua ndipo wanapofanya kazi kwa uadilifu mkubwa mana ni waoga na wanaopenda nafsi zao.
Awamu hii imerudi nyuma zaidi ya ile ya JK . Imekwenda mrama zaidi .
Pesa zinakusanywa nyingi kila mahali na ardhi inaizwa kila mahali lakini pesa za mauzo zinaishia kwenye familia za watawala na mabosi wasomi wanaomuongoza kiongozi asiyekua na maono na kuijua misingi ya Uchumi unaotokana na Rasilimali za asili . Matokeo yake anagawa rasilimali za kutumika karne nzima kwa bajeti ya mwaka mmoja.
2025 Tanganyika ichukue maamuzi Magumu mana bila hivyo hii nchi itageuka kuwa Kongo .
Nimejua maana ya Royol tours haikua utalii bali kutangazia wezi utajiri wa nchi ili waje wainunue. Ndio maana hatuoni ongezeko la watalii Tanganyika zaidi ya wanunua ardhi na kujenga mahoteli huku wakiwafukuza wazawa kama Kongo wanavyowafukuza na kuwaua Banyalenge na kuwaacha wawekezaji wakichota madini.
Kitakachofuata ni Waarabu kujitangazia himaya yao Kaskazini na majeshi ya nchi kushindwa kuwadhibiti mana wapo eneo lisilo na wenyeji ambao ndio walinzi wa kwanza wa rasilimali za nchi.
Tundu Lisu anastahili kuwa Rais wa Tanganyika kwa faida ya Wote kwa sababu hii mikataba mingi imefanywa kimaslahi badala ya sheria.
Yule alitepo kwa sasa uwezo wake wa kisheria ,kiuchumi na kimaono mdogo sana . Anaongozwa na hisia za kifamilia na makuzi yake tu . Ndio maana anapoona mwarabu basi anaamini ni mtu mwema na mchamungu bila kujua kuwa dunia nzima wafanyabiashara hawana ubinadamu linapokuja suala la pesa.
Tupate Rais mwenye maono na kujua sheria na historia sahihi ya ulimwengu. Mwenye uwezo wa kujenga hoja za kisheria duniani sio vijembe na sijui Rais wa kwanza sijui mvulana au kijana au mwanamke. Ni upuuzi usiotusaidia chochote kwenye vita ya kiuchumi na mikataba ya kinyonyaji na Kimangungo.
Wakuu wa vyombo vya usalama waache Watanzania wachague Rais na wabunge wenye maono mapana itawasaidia wao pia .Yanayoendelea chini ya CCM ya awamu hii ni hatari sana kwa usalama wa nchi baadae na watakaoumia ni watoto wa maskini waliopo chini kwenye majeshi yetu ambao hawana mwanya wa kuchota mapesa na kujenga majumba Dubai na mahoteli ya kitalii kwenye hifadhi. Watasumbuliwa na ugaidi na ujambazi na vurugu nyingi toka kwa wananchi walionyanganywa ardhi zao na kubaki maskini.