Mtoto wako amewahi kukuaibisha mbele za watu?

Hii ni chai. Mtoto wa miaka miwili, mwenye wazazi wasiokunywa bia/pombe mbele yake. Aone bia na alilie eti anataka pombe?
 
Hii ni chai. Mtoto wa miaka miwili, mwenye wazazi wasiokunywa bia/pombe mbele yake. Aone bia na alilie eti anataka pombe?
Mbona kuna mtoto wa jamaa yangu tuliemda naye benki akiwa na Baba yake. Alipowaona askari wana bunduki akaamza kulikia bunduki pale CRDB Mpanda. Kwani mzazi wake alikuwa na bunduki hadi dogo aliloe bunduki?
 
daah watoto wakweli sanaaa
 
Mwenyewe mkuu sipendi mtu abakize chakula na kitupwe, unasema mapema kama ni kingi.......
Sitaki uharibifu watu wanalala njaa ujue. Una binti smart Kwa kweli
 
Niliwahi kukaribishwa chakula kwenye familia fulani ya kishua nikapikiwa ugali na nyama ya mchuzi. Nikaona ili nifaidi vizuri lile chuzi nikawa kila nikimega tonge natumia dole gumba langu kupiga lile shimo katikati ya donge la ugali ili kuchota ule mchuzi. Kumbe kuna dogo wao wa miaka mitatu hajawahi kuona kile kitu. Basi aliponiona kakimbia kwenda jikoni akiita mama mamaa njoo uone mama yake kaja dining anamuulizia nione nini. Dogo karopoka mgeni anatengeneza kwa kutumia ugali kichoteo cha mchuzi. Niliona aibu acha tu.
 
Hahahaha...mgeni
 
Mwenyewe mkuu sipendi mtu abakize chakula na kitupwe, unasema mapema kama ni kingi.......
Sitaki uharibifu watu wanalala njaa ujue. Una binti smart Kwa kweli
😄
 
Huyu mtoto ana akili sana
 
Kuna katoto changu kana miaka miwili kanapenda pombe balaa.kakiipatia kanaigonga kinoma hata kisungura.Sasa hivi huwa nakaficha kasiione.
 
Nilijisikia vibaya pale mwanangu aliposema baba hapa tunakula mpaka tunashiba, hivi naweza kubaki hapa mpaka shule ifunguliwe mwakani? Alikuwa anayasema haya kwa jirani yetu tulipokwenda kutoa pole ya msiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…