Mtoto wako amewahi kukuaibisha mbele za watu?

Ila hii tabia ya mtu anajipakulia chakula mwenyewe halafu eti anakula nusu au robo anaacha huwa ni tabia mbaya sana.
 
Una malezi ya hovyo.... Halafu kwa nini nguo za wenzio unaita manguo?? Wewe na mwanao wote sawa tuu..
 
Tuliwahi kumtembelea jirani, tukaletewa soda hatujakaa sawa mtoto wake akaja na likikombe likubwa anaomba soda, ukimuwekea anaipiga tarumbeta anaomba tena, sio mtoto wangu ila nilihisi aibu.
Ulitakiwa umiminie nusu huyo mtoto, na akimaliza muongezee tena iishe yote ili kupeleka ujumbe kwa mwenyeji wako kuhusu malezi...
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nilijisikia vibaya pale mwanangu aliposema baba hapa tunakula mpaka tunashiba, hivi naweza kubaki hapa mpaka shule ifunguliwe mwakani? Alikuwa anayasema haya kwa jirani yetu tulipokwenda kutoa pole ya msiba.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] aibu hii
 
[QUOTE="

Na hiyo tabia ya kuropokaropoka watoto wwnu wanaiga kwenu wazazi na walezi,wafundisheni watoto kuwa na khaba si kila wanachokiona/kusikia ni lazima waongee,

i,[/QUOTE]

Ni kweli.Mimi nakumbuka siku moja nilienda na mtoto wangu kumsalimia rafiki yangu.Tulipofika tulikaa muda mrefu bila kukaribishwa kitu chochote kama wageni.
Mimi mtoto wangu alishazoea nyumbani wakija wageni lazima tuwanunulie soda.Sasa yeye alivyokaa muda mrefu bila kuletewa soda,alinyanyuka alipokuwa amekaa (maana alikaa mbali na mimi) akanifuata akaniuliza,mbona hatupewi soda? Nilicheka sana.Ninachotaka kusema hapa hakuropoka na tabia hiyo amekua nayo maana sasa ni mtu mzima 22 years lakini kama kuna mgeni akitaka kukwambia kitu lazima akusogelee aongee kwa sauti ndogo.
 
Watoto ni wazuri sana .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Sure..

Comedy zao burudani sana.

Kuna mwamba wangu mmoja yeye anakimbiza vifaranga anavinyonga, yaani kuku akitotoa pale home inabidi wawekwe mbali nae.

Kosa umfunge kuku kamba asweze kukimbia utamkuta yeye anamchezea chezea shingo, nataka nije kumfundisha kuchinja kuku sabab naona ndo anapoelekea
 
Miaka kama mitatu hv imepita kabinti kangu kalikua ndo kana miaka mi5 na wa kiume ana miaka 2

Sasa nipo sebulen nmekaa wao wanaangalia tamthilia fln hv na mm nazuga tu naangalia wala akili haipo kwenye TV, ikafika scene waigizaji wanataka kukiss kale ka kike kakamkimbilia mwenzake mdg wa kiume kakamziba macho kwa kiganja. Nilicheka sana hio siku
 
Kuna katoto changu kana miaka miwili kanapenda pombe balaa.kakiipatia kanaigonga kinoma hata kisungura.Sasa hivi huwa nakaficha kasiione.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Duh we jamaa wewe, so na wewe unagonga kisungura
 
Kuna katoto changu kana miaka miwili kanapenda pombe balaa.kakiipatia kanaigonga kinoma hata kisungura.Sasa hivi huwa nakaficha kasiione.
Mimi wa kwangu alikuwa na miaka kama minne, so nilikuwa nikienda washroom anaipiga pombe yote kwenye grasi then anarudishia so mimi nikirudi sijui kama kaipiga ya kwenye grasi. Hawa watoto hawa
 
Mimi wa kwangu alikuwa na miaka kama minne, so nilikuwa nikienda washroom anaipiga pombe yote kwenye grasi then anarudishia so mimi nikirudi sijui kama kaipiga ya kwenye grasi. Hawa watoto hawa
Mwanao alikua na haki zote kuipiga pombe Yako sababu pombe haikai kwenye grasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…