Mtu anapoomba maji baada ya ajali na ukampatia, ni nini kitamtokea?

Please summarize hata sentensi Tano, umeelewaje baada ya kugoogle?
afu kwa lugha ya taifa basii
 
Ndugu, hujajibu swali.
Achana na mambo ya predestination.
Mfano: Binti mmoja jirani yangu alifanya abortion na mauti yakamkuta lakini cha ajabu pale msibani nilisikia wazee wakitoa pole kuwa hiyo ni kazi ya Muumba, kwamba wakati ulikuwa umetimia!
Ni kweli kuwa wakati ulikuwa umetimia?
Mtu anayeomba maji baada ya kupata ajali yawezekana asipewe maji na akapona.
Ninaamini wajuvi wa mambo watatoa jibu ni kwanini.
 
Kwa sababu umepunguza maji mwilini kwa kutoka jasho. Haishauriwi unywe maji au kuoga mara unapo maliza mazoezi, bali upumzike mwili upoe kwanza.
Nafanya mazoezi ya GYM na Proffesional unashauriwa upige mazoezi na maji pembeni.
 
Labda maji yanaweza kusababisha cardiac overload 😂😂
 
Tafsiri:
1 mtu aliyepata ajali, anakuwa hana ufahamu mzuri, licha ya kuhisi kiu, anaweza asiweze kunywa maji vizuri, ikapelekea kupaliwa na hatimae kifo.

2 baada ya ajali, mtu anaweza kuhitaji upasuaji mkubwa wa dharura. Upasuaji hufanyika mtu anapokuwa hajakula au kunywa chochote. Hivyo ni vizuri kutompa aliyepata ajali maji au chakula ili aweze kusaidiwa kwa haraka hospitalini.

3 mtu anapoumia kichwani, kuna uwezekano wa kuwa na uvimbe ndani ya ubongo hasa asipotoka damu (nyingi au hakuna damu kabisa). Akipewa maji, kuna uwezekano wa kuongeza kasi ya kuvimba ubongo na kusababisha ubongo kuharibika na mtu asipone tena.(koma, kupoteza fahamu kwa muda mrefu hadi kifo).

Pia baada ya ajali, mtu anakuwa katika mshituko. Katika hali hii, damu inakimbizwa zaidi katika viungo muhimu, kama moyo, na mapafu.
Mfumo wa chakula unakuwa haupati mzunguko wa kutosha wa damu, hivyo ukimpatia maji, kuna uwezekano mkubwa akaanza kutapika, na hii itapelekea azidi kupoteza maji mwilini, kupoteza fahamu hasa anapopaliwa na maji yaliyoingia katika mfumo wa hewa na pengine kupelekea kuzimia hata kifo.
 
swali limeulizwa kiswahili unajibu kiingereeza,,,
 
Well
 

Ni nani aliyekufa ktk familia yako au rafiki zako kisha baada ya kuwa ameshakufa akakueleza kwamba kile kiu alichosikia hadi akakuomba maji ya kunywa kilitokana na ujio wa kifo chake?

Ajabu sana hii,unatoa conclusions kwa kitu ambacho hata hujawahi kuhisi kinafananaje/kinakuwaje!
 
Mhasiriwa anaishi kwa damu iliyo mwilini. Kwa hivyo kutoa maji husababisha upunguzaji wa damu na mwathiriwa huanguka hadi kufa kabla ya kupata msaada wa matibabu.

Ikiwa jeraha ni dogo sana kama vile mikwaruzo ya kina, kuvunjika kwa mkono au miguu mtu anaweza kuchukua maji lakini hata hivyo inashauriwa kuzuia mpaka msaada wa matibabu.

Usije kuwapa maji wahasiriwa kama vile waliondondoka kutoka umbali mrefu, aliepata majeraha maeneo ya tumbo au sehemu yoyote ya mwili. Pia usimsonge mwathirika. Watu wengi wanauawa wahasiriwa pale wanapo jaribu kusaidia kabla ya misaada ya kwanza kufika.

Mhasiriwa hakika anahisi kiu, kwa hivyo ili kuipunguza mtu anaweza kulowesha ulimi na karatasi ya kitambaa, leso nk.
 

Hapa ndipo msingi wa tofauti baina ya sayansi na nyungu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kutoa maji kunasababishaje upunguzaji wa damu mwilini?
 
Kuna mshikaji alikuwa amelewa chakari mchana wa jua Kali akaanguka kutembea hawezi ila alikuwa amekaa tu na anaonekana hana nguvu,akawa anaomba sana maji kwa wapita njia

Kuna jamaa alikuwa karibu akafuata maji alipokaribia Kuna mama mmoja akasema usimpe maji atakufa,kama una chumvi mpake kwenye nyayo pombe itakata

Je aliyelewa sana nae ukimpa maji atakufa?
 
Hatutaki kiislam tunataka kibailojia
 
Umetaka kupinga na bado hujaweka unachokielewa..
Naona hujaelewa nimejibu hivi kupona ama kutokupona inategemea na wakat wake anaweza akaomba maji asipewe na asife, nadhani ukilegeza kichwa utaelewa nilichomaanisha chief.


Ni hivi kila mtu na wakati wake, atakufaje inategemea, na hiki ndio utahukumiwa nacho, ahada ni ww kufa tarehe 30/12/1995, saa 1330, ukifika muda huo utakifa tu, iwe ulikiwa guest, uwe kanisani, uwe umelala kwako, uwe umelazwa hospitali, uwe unatoa misaada kwa yatima, uwe unaendesha ndege utakifa tu.
jiulize wangapi wanafanya abortion na hawafi, ni sahihi kazi ya Mungu(lazima sote tufe) ila namna gani kafa ni juu yake.

Mtu anaugua kansa vipimo vinaonesha baada ya mwezi ni kushney lakini anakuja kuishi miezi kadha wa kadha mpaka madaktar wanashangaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…