Mtu anapoomba maji baada ya ajali na ukampatia, ni nini kitamtokea?

Mkuu kwani mtu akitoka kufanya mazoezi mbona anakunywa maji ?
anakunywa lakini anashauriwa yasiwe ya baridi sana na ikiwezekana achukue muda kidogo
lakini pia inawezekana yasilete shida kwa kuwa yeye hufanya mazoezi kama tendo la hiyari na mwili wake umezoea hivyo sasa huyu ghafla lazima inaweza sumbua.
 
Ni Imani tu hakuna chochote. Imetokea mara nyingi Mtu akikaribia kukata roho huwa anapatwa na kiu na kuhitaji maji, sasa naona watu wameconnect dots

Ila sioni kama kuna uhusiano wowote kisayansi wala kiimani.
 
Kama tunataka kuelewa hivi, halafu havileweki. ebu iweke kwa kiswahili itapendeza zaidi.
 
Wiki tatu nyuma mgonjwa wangu wa ajali alifariki baada ya kupewa maji maana alikuwa akilalama sana kuhusu kiu
Nazani ni Imani tu na hii kisayansi ni kwamba mtu wa ajari anaweza fikia kwenye oparation moja kwa moja ndo maana hairuhusiwi si tu maji hata Chakula hakiruhusiwa
 
Kuna kitu kinaitwa NPO yaani Nill per Oral, hii ni kwamba kwenye Kufanya Oparation mgonjwa anatakiwa asiwe amekula kitu chochote kile kwa masaa kadhaa sasa kwa mtu wa ajari huwa kuna uwezekano wa wa majeruhi jufikia chumba cha upasuaji moja kwa moja so kitendo cha kumpatia maji kitachelewesha upasuaji wake. Hii ndo sababu kuu, na sio Maji pekee hata chakula asipewe
 
Ni Imani tu hakuna chochote. Imetokea mara nyingi Mtu akikaribia kukata roho huwa anapatwa na kiu na kuhitaji maji, sasa naona watu wameconnect dots

Ila sioni kama kuna uhusiano wowote kisayansi wala kiimani.
Hapana mkuu sababu kuu ni kwamba mtu wa ajari huenda akafikia Chumba cha upasuaji moja kwa moja na kuna kitu kinaitwa Nill Per Oral(NPO) sasa endapo atakuwa kapewa maji maana yake upasuaji utacheleweshwa na hapo anaweza pata matatizo zaidi.na sio maji tu hata Chakula asipewe
 
Kwanini maji au chakula kitachelewesha upasuaji wake?
 
Unaweza kumpa maji ila yawe ya moto kiasi

katika hali hii mhusika huwa katika hali ya taharuki jambo linalofanya damu yake kuwa na joto kubwa sambamba na mgandamizo mdogo wa mwili hivyo ukiweka maji ya baridi tumboni kiasi cha joto la damu hupanda zaidi kuliko kwaida na hata kupelekea kifo

chukulia mfano wa mafuta yanayotokota kwenye kaangio halafu uweke maji bila kitu kingine chochote je nini kinatokea moto huripuka

nb;yale maji ya dripu hospitalini huwa na viungo maalumu ambavyo huongezwa humo ili kufanya mchangamano wa maji hayo na damu kushabihiana

.
 
Thanks
 
Lakini kumbuka maji anayokunywa hayaingii kwenye mishipa ya damu directly ni mpaka yafanyiwe absorption.
 
Unashauriwa usimpe maji ili ku avoid Aspiration. Maan asilimia kubwa ya watu wanaopat ajali huwa hawako conscious na syestem mbalimbali za mwili zko disturbed. Kwahy ukimpa maji kuna uwezekano mkubwa maji kupita katika njia ya hewa
 
Kuna sababu kadhaa ni kwa nini huwa haishauriwi kuwapatia maji wagonjwa walopata ajali, na kwa nini hii hali..
Kawaida Mwili unapokua kwenye Shock, mzunguko wa damu hupungua katika mfumo wa chakula hivyo kufanya mfumo wa chakula kutofanya kazi ya ipaswavyo na kupelekea maji na chakula kutofyonzwa ipaswavyo na Kusababisha Kiu.

Sababu ni kwa nn tusimpatie mtu huyu chakula au maji
1.Yawezekena mtu huyo akawa ameumia Vibaya sana mno hivyo atuhitaji Upasuaji mkubwa wa Haraka, hivyo ukiwa umempatia Maji ama chakula itasababisha Complications wakati wakupatiwa dawa za Usingizi(anaesthesia).

2. Mtu akiwa kaumia vibaya na kupoteza fahamu hupaswi kumpatia maji sababu anaweza tapika na matapishi yale kuingia katika koo la hewa na kusababisha kifo chake.

3. Yawezekana mtu huyu akawa pia ana ongezeko la msukumo wa damu( High blood Pressure) hivyo hapaswi kuongezewa maji maana Pressure itazid kuwa juu na kumsababishia Madhara katika ubongo wake( Haemoregic shock).

Nadhan Nimejibu.
Mawere Francis
EMD Dept..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…