Mtu binafsi anaweza kumiliki soko?

Mtu binafsi anaweza kumiliki soko?

Badala ya soko jenga Tower au Mall itayotoa huduma ya maduka na services zingine huko ndani weka eneo la Supermarket za kisasa zenyewe zinabeba kila kitu mpaka hizo mboga na vyakula vya asili.
 
Kwanza ungejiuliza tafsiri ya soko ni nini,.Je wale wanaojenga majengo makubwa ya biashara na kuwapangishia watu maeneo ya kuuzia bidhaa(Mall)
Jibu rahisi ni kwamba inawezekana.
 
Kwanza ungejiuliza tafsiri ya soko ni nini,.Je wale wanaojenga majengo makubwa ya biashara na kuwapangishia watu maeneo ya kuuzia bidhaa(Mall)
Jibu rahisi ni kwamba inawezekana.
Ni kweli, malls na masoko yetu havina tofauiti kiutendaji, vimetofautiana hadhi tu. Kama mtu binafsi anaweza kujenga mall basi hata soko inawezekana.
 
Inatakiwa iwe hivyo, sababu haina tofauti na umiliki wa majengo ya biashara kama malls. Shida inakuja pale ambapo serikali inanyang'anyana biashara na watu binafsi sababu serikali eg. Manispaa, mamlaka na kampuni za Umma havina vyanzo vya mapato ndio maana zinajiingiza katika kufanya biashara. Cases hizi hazina tofauti na Kazi za watu binafsi kupewa SumaJKT etc.
 
Kwa jina la jamhuri,

Wakuu hivi kama nina kiwanja naona kimekaa sehemu nzuri naweza kukifanya kiwe soko? Yaani hapo kati nijenge au niwape watu wajenge meza za kuweka mambo ya mbogamboga, nafaka na vyakula vingine halafu pembeni nijenge furemu kuzunguka. Kama tu yalivyo masoko mengi.

Hapo nakuwa nachukua miatatu miatatu za wenye vibanda, miambilimiambili za chooni na kodi za maduka kwenye frem zinazozunguka.

Inawwzekana hii kitu, ishu za mipango miji zikoje?
Unaweza kufanya hivo ila tatizo pakinoga serikali inaweza amua kupachukua kabisa.
 
Inawezekana Ila fanya kama vile fremu
Pasiwe open kabisa
Weka zege chini
Na Kodi Kwa halmashauri ulipe
Kwanini asijenge hizo frames na mabanda akodishe kwa mwezi halafu halmashauri wakusanye ushuru wao kama kawaida ?
 
Mkuu mbona CCM huwa inamiliki open space kisha inawakodishia watu wanaoweka vibanda na kuwa soko, hujawahi ona hilo?
Usijilinganishe na ccm mkuu, ccm wanamiliki nchi pamoja na raia wake waliomo ndani ya nchi.

Waliweza kujimilikisha viwanja vya mpira na majengo yote ya umma.

Awamu iliyopita walimiliki kundi la watanzania wanaitwa wanyonge ikawa Mali yao halali.

Walijitwalia hadi uwezo wa kuondoa uhai wa yoyote asiyekubali kuwa mnyonge.

Usijilinganishe na ccm.
 
Soko ni chanzo muhimu cha mapato ya halmashauri na tushajijengea imani kuwa masoko ni ya halmashauri maana ndio wamiliki wa ardhi.. hivyo kuna hatari ya kujuta kwa kuwa mshindani wa halmashauri.. siku utaamka utakuta SI MMILIKI TENA
Mkuu Red Giant kuna eneo moja nimeona hapa Dar ni soko bubu yaani linamilikiwa na mtu binafsi. Hapo unapata kuanzia mitumba mpaka nyanya mpka electronics yaani pako busy kma upo tandika vile.

The thing is pengine alifanya lobbying ama ni mtu mzito serikalini/mzee wa zamani. Otherwise usiliite soko per se ila eneo ambalo unakutanisha biashara zote. Wewe uchukue gharama ya pango tu tozo zingine waachie halmashauri ili kuepusha mgogoro.

Hilo eneo naloongelea serikali ilijenga soko kwa mabilion na stendi hapo hapo (Era ya jiwe) ila pamedoda kabisa daladala zinasimama karibu na hilo soko na wauzaji/wanunuzi wote wanaishia hapo. Na hakuna kitu serikali imefanya mpka navyoongea hapa.
 
Inawezekana ila ramani ya mji inasemaje?
Halmashauri haitakubali ila akaanzishe Genge hapo hakuna atakayemfuata na atatoza vimeza vyake viwili hadi kumi
Soko ni lazima liwe na Choo, Jalala /dampo, barabara ya kuingizia mizigo na ya kutolea uchafu
sasa shangaa wenye magenge hata usafi wa kumwaga mabaki hawana iwe mkokoteni au kwama, choo hakuna wala usimamizi wa afya punde kipindupindu
 
Back
Top Bottom