Mtu huyu akisimama na mgombea wa CCM mwaka 2025, ni lazima CCM tuangukie pua

Ila Halima Mdee alistahili kuwa hata M/kiti wa CDM kuliko huyu aliyepo sasa! Yule dada anajua, anajiamini na ni mchapakazi. Hayumbishwi na walioshikilia rungu iwe ndani ya chama au nje ya chama. Yuko imara kusimama na kile kilicho sahihi, siyo huyu wa mbingu na Ardhi. 😂😂 ukisema mbingu na ardhi tafsiri yake ni kuwa umeridhika na utendaji kazi wa mtu huyo 100% hivyo hauna haja ya kuweka upinzani ni halali yake aendelee bila hata kupingwa. (Mbingu na Ardhi = pepo na jehanamu) sa uko peponi sa hv nini unahitaji tena?
 
Kiukweli, hiyo point ya kwanza Chadema inaikidhi. Chadema ina sura ya Kitaifa.... Ni propaganda za CCM tu ndiyo zinazotaka tuone vingine kwa kuwa Wachaga na watu wa Kaskazini walikiunga mkono mapema.
 

Kwani huwa mnashinda?
 
Ukweli mchungu,

Kukosa itikadi na misimamo kunaidhohofisha CHADEMA pakubwa.
Ya ni kweli mkuu, wengi hili la kukosa msimamo wanajifanya hawalioni. Na matokeo yake na hivi kila unapofika uchaguzi wanaangukia pua na kuisingizia tume ya uchaguzi.
 
Mbowe enzi za JPM sio Mbowe (mlamba asali) wa SSH.
Hahaha. Mbowe, Zito, Lisu, Mbatia, Lipumba na wengine wa aina hiyo washampata mtu wa kuwapa mzinga wa nyuki ili wajichotee asali watakavyo huku wanachama wao wakiishia kupiga kelele mitandaoni.
 
Tukuchague wewe mkuu. Ni vyema ukajitokeza kugombea naamini sifa ulizotaja unazo
Hahaha.. kuna mdau katika post namb #23 amejitokeza tumchague katika uchaguzi mkuu wa 2025, anadai vigezo hivi anavyo 😂😂🤣
 
Ili kuelewa chochote, ni lazima kwanza kichwani akili iwemo maana ndiyo inayokupa uwezo wa kuelewa jambo.
Kweli mkuu, hapa umemjibu vyema kabisa 🙏.
 
Hahaha.. Sidhani kama chawa wa mwenye chama watakuelewa.
 
Kiukweli, hiyo point ya kwanza Chadema inaikidhi. Chadema ina sura ya Kitaifa.... Ni propaganda za CCM tu ndiyo zinazotaka tuone vingine kwa kuwa Wachaga na watu wa Kaskazini walikiunga mkono mapema.
Ya ni kweli kwenye utaifa CDM wamejitahidi ndo maana wana wanachama mikoa yote ya Tanzania including Zanzibar. Ila kwa haya mengine kama hawakujisahihisha kumpata mtu sahihi, basi kila siku watakuwa wanamtafuta mchawi na wakati mchawi mwenyew wanae ndani.
 
Acha uongo, hakuna uchaguzi ulivokua na wapiga kura wengi kama 2015 sasa wakina nani walikata tamaa kisa Lowassa?? Sema walikata tamaa ya kushinda milele maana chance ya 2015 ilikua realistic zaidi so walivunjika moyo kura zilipoibiwa.

2. Kuhusu nguvu ya umma iliwezekana sababu serikali haikuwa violent kama ya JPM. Enzi za Kikwete kina Mnyika na Dr Slaa walikua moto sana ila sikuwahi ona Slaa akimiminiwa SMG au Mnyika kutekwa!! Hivi unadhani baada ya tukio la Lissu na SaaNane kuna mwenye ujasiri aingie barabarani?

3. Hiyo CUF unayosifia hapa nayo ilipoa baada ya machafuko ya zenji walipomwagiwa risasi kama mvua. Ukiwa violent unadhani raia wasio penda vurugu watalipiza?? Unless kama unataka tuanzishe armed wings kama vyama vya huko uarabuni.

All in all vyama vilipoa sababu ya violent crackdown ya serikali huku napoishi kuna mdhamini wa kisiri wa CHADEMA ni tajiri wa hardware ila alisakwa mpaka akapotea mpaka Leo Hana hamu ya kusikia siasa. Sasa huyo utasema ni sababu ya Lowassa?
 
Ni Mbulumakenge tu anaweza kuandika ulichoandika.!!

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…