Mtu huyu akisimama na mgombea wa CCM mwaka 2025, ni lazima CCM tuangukie pua

Sifa hizo mimi ninazo.

Wana Jamii Forum kwa umoja wetu tuundeni chama chetu cha siasa kitachoongozwa na:
1) Mwenyekiti: Maxence Melo
2) M/mwenyekiti: Pascal Mayalla
3)Katibu mkuu: Mshana.

Kwa uongozi huu hapo juu CCM inaaga mchana kweupe
Mm nitakua mtinza hazina wenu
 
Mkuu hebu tuwe wakweli, bila muunganiko wa vyama ulioitwa UKAWA unafikiri Lowasa angepata kura nyingi kiasi kile? Kumbuka Lowasa aliungwa mkono na vyama vyote vikubwa vya upinzani Tanzania kama vile CUF ya Maalim iliyokuwa na mamilioni ya wapiga kura kule Zanzibar lakini pia ilikuwa na mtaji wa wapiga kura kadhaa huku bara.

CDM na NCCR MAGEUZI nao kwa umoja wao walikuwa na mamilioni ya wapiga kura bara, lkn pia walikuwa na mtaji wa wapiga kura kadhaa Zanzibar.
kwahiyo ni lazima angepata kura zile alizopata. Hata ingekuwa wewe ndio unagombea afu vyama hivyo nilivyotaja hapo juu vinakuunga mkono, amini ungepata kura nyingi ambazo wewe mwenyew hukutarajia.

Ndomaana baada ya uchaguzi ule kuisha na UKAWA kusambaratika kilichofuatia ilikuwa ni aibu.
Wapinzani walianza kuangukia pua hata katika chaguzi ndogo tu za kawaida hapo Kinondoni na kupelekea wapinzani kujifanya kuitisha maandamano na hatimae maandamano yale yakaondoka na roho ya Akwilini.

Kuhusu wapinzani kunywea hii haisababishwi na utawala wa Magufuli, bali watanzania wenyewe wamechoshwa na siasa uchwara za hawa wapinzani butu. Kina Mwangosi wameteswa na kuuwawa wakati wa utawala wa nani? Vipi vifo vya kule Zanzibar? vipi yale mabomu yaliouwa watu kule Soweto Arusha? Vipi kina Lipumba kujaribu kuandamana na kuambulia kipigo kilichosababisha avunjwe mkono wakati wa utawala wa Kikwete? I mean tawala zote wapinzani walichezea kichapo na wapo waliouwawa pia, ila kwa vile wanachama walikuwa na imani na upinzani basi walikuwa tayari kufa kuliko kuendelea kutawaliwa na CCM. Ila baada ya kile kilichofanyika 2015, wote waliokuwa tayar kuweka maisha yao hatarini waliamua kuanza kufikiria mara mbili mbili kuhusu upinzani waliokuwa wanaupigania na hapo wengi wakaamua kuachana na mambo ya kisiasa kwani waliona siasa za Tanzania ni za kinafiki tu.
 
Haya magaidi hayawezi ingia ikulu pale. Ikulu ni mahala patakatifu alisikika akisema mzee mmoja.
 
Kabisa, CCM watu hawaipendi, ila ukikaa vizuri ukifikiria kwa kina unaona bora niwape kura CCM au nisipigie kura chama chochote.
Upinzani upo katika hali mbaya sana, pamoja na kujaza chawa mitandaoni lkn bado haisaidii chama kusonga mbele.
 
Mleta mada angekuwa ni mtu makini angekusoma kwa uangalifu zaidi ya kukupa 'like' kama alivyofanya hapa.

Kama kuna mtu aliyejitoa kikwelikweli (hata kama hilo halikuwa lengo na tegemeo mwanzoni mwa harakati zake), mtu huyu anayesemwa hapa kajitoa hasa. Lakini pamoja na kujitoa huko, watu aliotegemea wataelewa maana ya kujitoa kwake ikawa kama hawana habari naye. Hili linakatisha tamaa mtu yeyote yule, hata kwenye siasa.

Kuna kitu/jambo ambalo CHADEMA hawajalitambua vizuri kuhusu waTanzania, na kwa nini CCM inaonekana kuendelea kuwashikilia kama wapo jela.
CHADEMA inawapasa kudadisi na kuelewa ni jambo gani hilo.
Pamoja na ubovu wooote ilioufikia CCM, lakini waTanzania ni kama wameshikwa na sumaku wasiweze kujinasua. Jibu la CHADEMA na vyama vingine vya upinzani lipo hapo.
Wajiulize wenyewe, na wakilijua, CCM inakwisha.

Ukweli ni kwamba CCM imebaki kama mzoga tu, unaosubiri kufukiwa.
 
Ni hayo tu ninayoyaona mimi, katika kuijenga Tanzania bora zaidi ya kesho.
Upungufu wa mada yako ni kama ifuatavyo.

1. Kichwa cha mada hakiendani na yaliyomo ndani ya mada yenyewe. Kichwa kinasema "mtu" maelezo yanazungumzia chama.

2. Mada inajikita kushambulia chama kimoja cha upinzani, na kusahau kwamba kuna vyama vingi vya upinzani.
Kuelekeza nguvu zako zote kwenye hicho chama kimoja maana yake ni kwamba hicho ndiyo chama kinachokutia hofu zaidi ya kukiondoa chama unachokipigania wewe.

3. Kuondolewa kwa CCM sasa hivi hakuhitaji hayo yote uliyoyazungumzia ndani ya mada. Kule tu kukiondoa CCM kwa njia yoyote ile ni lengo linalojitosheleza kabisa kutokana na jinsi chama hicho kilivyogeuka kuwa adui wa waTanzania.

Haihitajiki hata kidogo chama kiwe na sera na mengi mengine unayolemba hapa.
 
Uzi tayari kazi kweli kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…