Mtu kukopa pesa mtandaoni na kukuweka kama mdhamini bila ridhaa yako ni sawa?

Huko PesaX ukitaka kukopa unajaza form.

Miongoni mwa vipengele ni kile kinachohitaji taarifa za mtu wako wa karibu, ikiwemo namba ya simu.

Sas pindi ukishindwa kulipa, mtu yule wa karibu anabadilishwa cheo na kuwa mdhamini.

Hapo ndipo timbwiri linaanzia sasa mdhamini kuanza kupigiwa simu na kutishiwa kuletewa polisi.

Pengine iwapo mwanzo kabisa wangedai kuwa wanamuhitaji mdhamini mtu angeweza kujipanga; shida ni kwamba wanakuambia wanamuhitaji mtu wa karibu.
 

Yes Sir, kuwa na ukaribu na mtu inamaanisha by default wewe nu mdhamini[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

[emoji23][emoji23]
 
Mdhamini hawi mdhamini bila kuridhia, haijalishi wanampa jina gani, so as long as hawakumshirikisha wakati wa kukopa, hawajibiki kwao kwa lolote, dawa ni kuwashtaki kwa ‘Harrasment’
 
Sasa mie kuna mtu alinipigia ananiambia nimwambie bwana Omari alipe deni sababu mie ni mdhamini wake. Kiukweli sijui mtu anayeitwa Omari na sijawwhi kumdhamini mtu akope pesa popote pale.

Nilipomuelezea yule mwanamke aliyepiga simu akaanza kuwa mkali kwangi,kwakweli matusi yaliyonitoka alikata simu yeye mwenyewe. Shenzi kabisa.
 
Safi sana, hata kama ungekuwa unamjua huyo Bwana Omary, So as long as hawakukushirikisha wakati anakopa, huwajibiki kwao kwnalolote lile!
 
Hawa wapuuzi tu,Wapuuze!, Sasa wakati jamaa anawapa no.yako Kwanini wasikupigie hapo hapo wakuulize kama unakubali au Vipi? Jamaa aliposhindwa kulipa ndio wanaanza kukusunbua
 


Hapo kwenye brown wanakiri kabisa kwamba wanakupa usumbufu kwa makusudi kabisa kwa jambo ambalo hukushirikishwa, hii itakuwa ni point nzuri sana kwenye judicial proceedings.
 
Uzuri hufungwi
Ubaya ni kufanyiana harassment na kupeana msongo wa mawazo. Hii ni criminal na watawajibika nalo kisheria, tatizo ni ushahidi, inabidi uwe na ushahidi hasa wa kitabibu na kidijitali kuprove kweli unastahili kulipwa fidia kwa damage za kisaikolojia walizokusababishia kwa makusudi..
 
Sio sawa, washitaki wao na aliekuweka kuwa mdhamini bila kushauriana na wewe kwanza.

Inatakiwa hao wakupigie wewe kuhakikisha kabla hawajampa mkopo.

Ukishindwa kuwashitaki ina maana unaelewa unachokifanya na unatuzuga tu JF.
 
Walikuja moto, wakarudi baridi!
 
Hawa jamaa hata mtu asipo kuweka mdhamini, unapodownload app yao kuna kipengele cha kuwapa access ya contacts na SMS, kwahiyo wanauwezo wa kuangalia majina na namba unazo wasiliananazo mara kwa mara, binafsi niliwahi kopa 30k siku moja kabla ya muda wa marejesho nikiwa nimeenda shambani maeneo flani network chenga nikawa sipatikani kurudi jioni nakuta wamempigia wife, mother na bro hao wote sikuwaweka kama wadhamini Wangu, walivyokuja kunipigia mimi nikawaambia kwa jinsi mlivyonichoresha siwalipi hiyo hela huu mwezi wa 6 sasa, inshort nikwamba jamaa wanatumia vibaya taarifa za wateja/wakopaji kinyume na sheria. n.b wengi wanaokopa huwa wanaweka namba na majina ya wadhamini ya kubumba.
 
Kumbe ndio uhuni wanaofanya huo?! Kisha wanaharass watu ambao hata hawakuhusika wakati wa kukopa, watapata kesi moja tamu sana, ngoja waendelee kuleta uwendawazimu wao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…