Mtu kukopa pesa mtandaoni na kukuweka kama mdhamini bila ridhaa yako ni sawa?

Mtu kukopa pesa mtandaoni na kukuweka kama mdhamini bila ridhaa yako ni sawa?

Wakati anakuweka mdhamini, wao walidhibitisha vipi kama umekubiana nae kukopa hiyo pesa, maana matokeo yake watu namba zao zinaandikwa tu kiholela bila mawasiliano wa makubaliano yoyote yale
Yaani haya makampuni uchwara sijui hawana wasomi wa kuwashauri,mm kuna siku walinipigia wakaniuliza unamjua fulani nikawajibu ndio ni wife wangu,wakasema amekopa hela kwetu na ameweka no yangu kama mdhamini,wakimpigia sim hapokei kwahiyo wamenipigia sim mm ili niwajibe kumkumbusha alipe deni nilichowajibu wao ndio wanajua [emoji2][emoji23]
 
Hao jamaa hata kama hujawekwa kama mdhamini wanakupigia ilimradi namba yako ipo kwa phonebook ya huyo aliye kopa. Ni wasumbufu.
Kakopa mwingine wanasumbua watu wote walio kwenye phonebook ya aliyekopa

Nimeshapigiwa simu kama mara 4 hivi, na wanatumia namba tofauti, na ni wakali hasa! Kwa kweli wananifanyia harassment mimi wakijua kwamba siwezi kuzima simu yangu, maana yule aliyekopa kawazimia simu, ni kweli namfahamu, lakini mimi sikushirikishwa lolote wakati anakopa.

Inabidi nianze mkakati wa kuwashtaki washenzy hawa, eti wananitishia kuepeleka taarifa zangu TCRA na kuanza kunikata moja kwa moja kwenye akaunti yangu ya pesa hadi deni liishe. Nasubiri watie mkono wachukue hata mia waone moto wake.

TCRA
 
 
Back
Top Bottom