Mtu kukopa pesa mtandaoni na kukuweka kama mdhamini bila ridhaa yako ni sawa?

Mtu kukopa pesa mtandaoni na kukuweka kama mdhamini bila ridhaa yako ni sawa?

Nimeshapigiwa simu kama mara 4 hivi, na wanatumia namba tofauti, na ni wakali hasa! Kwa kweli wananifanyia harassment mimi wakijua kwamba siwezi kuzima simu yangu, maana yule aliyekopa kawazimia simu, ni kweli namfahamu, lakini mimi sikushirikishwa lolote wakati anakopa.

Inabidi nianze mkakati wa kuwashtaki washenzy hawa, eti wananitishia kuepeleka taarifa zangu TCRA na kuanza kunikata moja kwa moja kwenye akaunti yangu ya pesa hadi deni liishe. Nasubiri watie mkono wachukue hata mia waone moto wake.

TCRA
hahah ni mikwara mbuzi tu hawana shida. wapotezee hawana cha kukufanya
 
Kuna mmoja alitoa taarifa kuwa hao jamaa wanalazimisha app yao uipe permission ya contacts/phone book. Inasemekana wakati mwingine wanadukua namba huko.
Muulize kistaarabu mdau mkopaji kama kweli alikuandika wewe.
 
1) Mtu anakopa pesa mtandano kisha anaandika namba yako kama mtu wake wa karibu bila ridhaa yako

2) Anaposhindwa kulipa, wale waliomkopesha wanaanza kukupigia simu eti uwasaidie kumfikishia taarifa kwamba alipe deni

3) Baada ya hapo anaposhindwa kulipa deni, eti wanatishia kukuchukulia hatua z akisheria wewe kama mdhamini.

Sasa najiuliza, hawa watu wamechanganyikiwa? Wakati anakopa sikushirikishwa wala kuambiwa lolote, ila ghafla bin vuu unaitwa mdhamini, hivi kuwa na ukaribu na mtu inamaanisha automatically weww ni mdhamini, hii imekaaje kaaje? 😂😂🤣🤣🤣

===========================
View attachment 2902362
Hapo kwenye brown wanakiri kabisa kwamba wanakupa usumbufu kwa makusudi kabisa kwa jambo hambalo hukushirikishwa, hii itakuwa ni point nzuri sana kwenye judicial proceedings.

Sasa mimi nataka nikope elfu 10 halafu niweke namba ya Nape Nnauye kama mdhamini, maana ninayo, halafu silipi, na yeye aanze kufaidi matunda ya sheria zake...
Siyo Sawa... Utabebeshwa zigo la lawama hapo na madeni juu, ikiwemo kulazwa selo.
 
Hawa jamaa sio kwamba kakuweka kama mdhamn wanakua na acces ya kuptia contact zote kwenye simu wanaangalia mawasiliano yenu kama mnawasiliana mara kwa mara ndio wanakutumia msg ni wasumbufu to the extent kauli mbovu yan hizo kampun hazifai kabisa na riba ni 95%
 
Nimeshapigiwa simu kama mara 4 hivi, na wanatumia namba tofauti, na ni wakali hasa! Kwa kweli wananifanyia harassment mimi wakijua kwamba siwezi kuzima simu yangu, maana yule aliyekopa kawazimia simu, ni kweli namfahamu, lakini mimi sikushirikishwa lolote wakati anakopa.

Inabidi nianze mkakati wa kuwashtaki washenzy hawa, eti wananitishia kuepeleka taarifa zangu TCRA na kuanza kunikata moja kwa moja kwenye akaunti yangu ya pesa hadi deni liishe. Nasubiri watie mkono wachukue hata mia waone moto wake.

TCRA
No! ..bila hata kukata sh. mia yako, pia unaweza kuwafungulia MASHTAKA mahakamani...

Yani natamani waje wajichanganye waingie anga zangu...
 
Hawa jamaa hata mtu asipo kuweka mdhamini, unapodownload app yao kuna kipengele cha kuwapa access ya contacts na SMS, kwahiyo wanauwezo wa kuangalia majina na namba unazo wasiliananazo mara kwa mara, binafsi niliwahi kopa 30k siku moja kabla ya muda wa marejesho nikiwa nimeenda shambani maeneo flani network chenga nikawa sipatikani kurudi jioni nakuta wamempigia wife, mother na bro hao wote sikuwaweka kama wadhamini Wangu, walivyokuja kunipigia mimi nikawaambia kwa jinsi mlivyonichoresha siwalipi hiyo hela huu mwezi wa 6 sasa, inshort nikwamba jamaa wanatumia vibaya taarifa za wateja/wakopaji kinyume na sheria. n.b wengi wanaokopa huwa wanaweka namba na majina ya wadhamini ya kubumba.
Dah mwamba ulidhalilishwa sana

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
15B722B5-D274-45C8-B5DD-5ABA3AD10A84.jpeg

😂😂😂😂
 
Kuna mmoja alitoa taarifa kuwa hao jamaa wanalazimisha app yao uipe permission ya contacts/phone book. Inasemekana wakati mwingine wanadukua namba huko.
Muulize kistaarabu mdau mkopaji kama kweli alikuandika wewe.
Awe aliandika au hakuandika, so as long as sikushirikishwa, siwajibiki kwa lolote, ila wao watalipia hii harassment mahakamani.
 
1) Mtu anakopa pesa mtandano kisha anaandika namba yako kama mtu wake wa karibu bila ridhaa yako

2) Anaposhindwa kulipa, wale waliomkopesha wanaanza kukupigia simu eti uwasaidie kumfikishia taarifa kwamba alipe deni

3) Baada ya hapo anaposhindwa kulipa deni, eti wanatishia kukuchukulia hatua z akisheria wewe kama mdhamini.

Sasa najiuliza, hawa watu wamechanganyikiwa? Wakati anakopa sikushirikishwa wala kuambiwa lolote, ila ghafla bin vuu unaitwa mdhamini, hivi kuwa na ukaribu na mtu inamaanisha automatically weww ni mdhamini, hii imekaaje kaaje? 😂😂🤣🤣🤣

===========================
View attachment 2902362
Hapo kwenye brown wanakiri kabisa kwamba wanakupa usumbufu kwa makusudi kabisa kwa jambo hambalo hukushirikishwa, hii itakuwa ni point nzuri sana kwenye judicial proceedings.

Sasa mimi nataka nikope elfu 10 halafu niweke namba ya Nape Nnauye kama mdhamini, maana ninayo, halafu silipi, na yeye aanze kufaidi matunda ya sheria zake...
Kopa afu usisahau kutuletea mrejesho.
 
Hao jamaa TCRA na mitandao ya sm tanzania washawaweka mfukoni kwa sababu mmiliki wa mtandao wa sm huwezi kuruhu mteja wako akaingiliwa mawasiliano yake usalama wa nchi upo wapi ikiwa kampuni furani ipo nchini inaweza duka mawasiliano ya wateja wako kwa sababu sheria ya faragha hairuhusu mtu ku access mawasiliano yako mpaka kibali maalumu sasa hao jamaa wanatoa wapi kibari cha wao kuwa na ruhusa ya kuweza kuaccess mawasiliano yako ikiwa sheria ya nchi hairusu wao nani kawaruhusu watumie kipengele hicho

Kiufupi hizo kampuni zinashirikiana na watu serikalini kuendesha uhuni wao hapa nchini kwakua ni shamba la bibi TRCA ndio hawasikii kabisa wala kuelewa tuma email piga sm wameziba masikio mitandao ya sm nayo ipo kimya sijui nani yupo nyuma wa hizi biashara
 
Wanachofanya ni kuingia kwenye contacts list ya aliyekopa na kutuma sms kwa kila mtu aliyekuwa kwenye hiyo list na sio kwamba huyo mtu amekuweka kama mdhamini.

Kuwa makini usije ukagombana na rafiki, ndugu au jirani yako kwa kufikiri alikuweka wewe kama mdhamini

Ni wasumbufu sn lkn pia na matapeli pia wamo humo pengine muhusika wala hakukopa kwao wanafanya hivyo ili ujichanganye ulipe then inakula kwako.
 
Jana nimepigiwa simu mara 80, sms mara 200, whatsapp mara 50. Na sijahusika wakati wanakopeshana hata chembe. Je, hii ni haki?
 
Back
Top Bottom