Mtu kukopa pesa mtandaoni na kukuweka kama mdhamini bila ridhaa yako ni sawa?

hahah ni mikwara mbuzi tu hawana shida. wapotezee hawana cha kukufanya
 
Kuna mmoja alitoa taarifa kuwa hao jamaa wanalazimisha app yao uipe permission ya contacts/phone book. Inasemekana wakati mwingine wanadukua namba huko.
Muulize kistaarabu mdau mkopaji kama kweli alikuandika wewe.
 
Siyo Sawa... Utabebeshwa zigo la lawama hapo na madeni juu, ikiwemo kulazwa selo.
 
Hawa jamaa sio kwamba kakuweka kama mdhamn wanakua na acces ya kuptia contact zote kwenye simu wanaangalia mawasiliano yenu kama mnawasiliana mara kwa mara ndio wanakutumia msg ni wasumbufu to the extent kauli mbovu yan hizo kampun hazifai kabisa na riba ni 95%
 
No! ..bila hata kukata sh. mia yako, pia unaweza kuwafungulia MASHTAKA mahakamani...

Yani natamani waje wajichanganye waingie anga zangu...
 
Dah mwamba ulidhalilishwa sana

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Kuna mmoja alitoa taarifa kuwa hao jamaa wanalazimisha app yao uipe permission ya contacts/phone book. Inasemekana wakati mwingine wanadukua namba huko.
Muulize kistaarabu mdau mkopaji kama kweli alikuandika wewe.
Awe aliandika au hakuandika, so as long as sikushirikishwa, siwajibiki kwa lolote, ila wao watalipia hii harassment mahakamani.
 
Mwenye namba ya mwenezi naoomba nimuweke mdhamini wangu mkopo pesa x. πŸ˜‚
 
Kopa afu usisahau kutuletea mrejesho.
 
Hao jamaa TCRA na mitandao ya sm tanzania washawaweka mfukoni kwa sababu mmiliki wa mtandao wa sm huwezi kuruhu mteja wako akaingiliwa mawasiliano yake usalama wa nchi upo wapi ikiwa kampuni furani ipo nchini inaweza duka mawasiliano ya wateja wako kwa sababu sheria ya faragha hairuhusu mtu ku access mawasiliano yako mpaka kibali maalumu sasa hao jamaa wanatoa wapi kibari cha wao kuwa na ruhusa ya kuweza kuaccess mawasiliano yako ikiwa sheria ya nchi hairusu wao nani kawaruhusu watumie kipengele hicho

Kiufupi hizo kampuni zinashirikiana na watu serikalini kuendesha uhuni wao hapa nchini kwakua ni shamba la bibi TRCA ndio hawasikii kabisa wala kuelewa tuma email piga sm wameziba masikio mitandao ya sm nayo ipo kimya sijui nani yupo nyuma wa hizi biashara
 
Wanachofanya ni kuingia kwenye contacts list ya aliyekopa na kutuma sms kwa kila mtu aliyekuwa kwenye hiyo list na sio kwamba huyo mtu amekuweka kama mdhamini.

Kuwa makini usije ukagombana na rafiki, ndugu au jirani yako kwa kufikiri alikuweka wewe kama mdhamini

Ni wasumbufu sn lkn pia na matapeli pia wamo humo pengine muhusika wala hakukopa kwao wanafanya hivyo ili ujichanganye ulipe then inakula kwako.
 
Jana nimepigiwa simu mara 80, sms mara 200, whatsapp mara 50. Na sijahusika wakati wanakopeshana hata chembe. Je, hii ni haki?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…