Mtu kukopa pesa mtandaoni na kukuweka kama mdhamini bila ridhaa yako ni sawa?

Wakati anakuweka mdhamini, wao walidhibitisha vipi kama umekubiana nae kukopa hiyo pesa, maana matokeo yake watu namba zao zinaandikwa tu kiholela bila mawasiliano wa makubaliano yoyote yale
Yaani haya makampuni uchwara sijui hawana wasomi wa kuwashauri,mm kuna siku walinipigia wakaniuliza unamjua fulani nikawajibu ndio ni wife wangu,wakasema amekopa hela kwetu na ameweka no yangu kama mdhamini,wakimpigia sim hapokei kwahiyo wamenipigia sim mm ili niwajibe kumkumbusha alipe deni nilichowajibu wao ndio wanajua [emoji2][emoji23]
 
Hao jamaa hata kama hujawekwa kama mdhamini wanakupigia ilimradi namba yako ipo kwa phonebook ya huyo aliye kopa. Ni wasumbufu.
Kakopa mwingine wanasumbua watu wote walio kwenye phonebook ya aliyekopa

 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…