Mtu ukiwa na pesa, somesha mwanao international schools, achana na hizi exam based schools or education

Mtu ukiwa na pesa, somesha mwanao international schools, achana na hizi exam based schools or education

Mtoto akifeli IST ni sawa na mtu umechana mkeka,tena sio umechana bali ni Umeurarua mkeka,Unaletewa taaarifa na uongozi mwanao anatakiwa arudie mwaka mzima,mwaka ambao ADA na makorokoro yote ni 23.5M - 25M Hii kama sio kurarua mkeka ni nini?

Mtu anaeweza somesha mtoto International ni yule mwenye income ya not less of 20M per month,yani kama kwa mwezi huna income hiyo internatinal isikilize tu humu JF tuki iongelea na kuipgia story.

Hamna ubishi kwamba huko ndipo penye ELIMU huko kote wala sibishi na sidhani kama kuna mende yeyote humu ataeweza kubisha,swala lililopo mezani ni Dooooo hapa tunaongelea Doooo wajua nini maana ya Dooo wewe,sio dooor ya mlango naongelea Doooo....hehehehe

Nitavimba sana town,ntakua na kiburi sana ila kiburi cha kusomesha international sijafikia na nadhani hata muda huo ukifika wanangu nao watakua washamaliza kusoma,hebu msinipe stress zingine mimi Pale maromboso nafasi zipo pananitosha vizuri tu,st patrick ipo panantosha vizuri tu acha akadanganywe huko huko na walimu sina namna.

ila international wajuba ni story zingine ishu sio kumiliki Mercedes-Benz Maybach Exelero ishu ni kuihudumia hii ndinga,ishu sio ADA ishu ni zile vi cost vya hapa na pale,kubabeki unaweza jikuta unaimba Mwambie Farao nimeokoka kwenye kundi la alshabaab wewe mwenyewe yani.
 
Kaangalie tena kwenye website ya IST. Karo inazidi hiyo uliyotaja kwa mbali sana.
Mtoto akifeli IST ni sawa na mtu umechana mkeka,tena sio umechana bali ni Umeurarua mkeka,Unaletewa taaarifa na uongozi mwanao anatakiwa arudie mwaka mzima,mwaka ambao ADA na makorokoro yote ni 23.5M - 25M Hii kama sio kurarua mkeka ni nini?
 
umeongea kweli mkuu liwe jua iwe mvua mwanangu kamwe hawezi soma hizi kayumba hata zege nitabeba.
utabeba zege mwaka mzima ila ada ya kupeleka mtoto international hutoipata,yani ubebe zege utegemee kusomesha mtoto international? labda kama karai 1 la zege watakua wanakulipa 500k per trip sio eti ulipwe 20k - 30k utegemee utasogelea hata joining instruction ya International.

Mkuu kuna mambo chini ya JUA ifike mahali tukubali kuwa hii dunia si kila kitu kilichopo ni lazima tukitumie au tukipate,kuna vitu vimewekwa duniani tuvitumie lakini hatujalengwa sisi aseee,kalengwa Billgert Na kina Jeff sio sisi.

Mungu hashindwi jambo kama aliweza wavusha wana wa israel kwenye ule mto,anaweza pia kukupa ADA ya kupeleka mtoto international,kwake yeye tu ndio tegemeo letu ila kibinadamu Kutoboa kwenye hiyo ada ya international ngumu ariffff..
 
Kaangalie tena kwenye website ya IST. Karo inazidi hiyo uliyotaja kwa mbali sana.
sikatai mkuu ndio mana nimesema hapa duniani kuna vitu hatujaumbiwa binadamu kama mimi,yani kuna vitu kwenye hii dunia vipo tuvisikie na kuviangalia tu.

sasa ada nilipe million 70 halafu toto niambiwe anatakiwa arudie mwaka mzima kama sio kutaftiana presha nini? kuna vitu MUNGU kaviruhusu viwepo duniani ila ajue kuna kina sisi ni kama tunaringishiwa tu.
 
Unajifariji tu. Scholarship unapata lakini haina maana kuwa ubora wako uko kama wa graduate wa IST. Walimu wanafundisha hapo chuo kikuu lakini hawawezi kujieleza kwa Kiingereza na wamepata skolaship za UK, US, Australia.. wamefanya PhD nk huko.
Ph.D kama ya Magufuli ni kielelezo kwamba Ph.D si lazima iwe usomi.

Kwa mfano.Magufuli ana matatizo ya kujieleza, Kiingereza na Kiswahili. Maana ingekuwa Kiingereza tungesema ni lugha ya kigeni.

Na hapo unaweza kuona tatizo la elimu za kukariri mambo badala ya kuelewa.
 
Hao wabunifu wa serikali nao wamepita mashule hayo hayo ya kukariri, watabuni nini? ndio hao hao wanaokuja na maswali ya multiplechoice hadi kwenye somo la hisabati.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] multiple choice hesabu bila calculations shida serikali inaangalia idadi ya watu wengi wamaluze tu shule hata Kama hawajui kusoma. Siasa mbaya kila mtendaji serikalini hataki kutumbuliwa Bora tu hata Kama hujui kusoma ufaulishwe
 
Uko sawa kabisa ndio maana hata wanasiasa wanasomesha watoto wao huko ! Halafu kwa hawa wanaowaita wanyonge wanaambiwa elimu bure! Sasa kitu cha bure tangu lini kikawa kizuri maana akiamka kesho anaweza kubadili maamuzi na hawana cha kuhoji!
 
Sijui unakubaliana nami ama unanipinga?
Ph.D kama ya Magufuli ni kielelezo kwamba Ph.D si lazima iwe usomi.

Kwa mfano.Magufuli ana matatizo ya kujieleza, Kiingereza na Kiswahili. Maana ingekuwa Kiingereza tungesema ni lugha ya kigeni.

Na hapo unaweza kuona tatizo la elimu za kukariri mambo badala ya kuelewa.
 
Mimi sizikubali sana hizo international school kwasababu mkifika Chuo kikuu,hakuna Significance difference ya wale waliosoma St.Kayumba na waliosoma International.
Tofauti huwezi kuiona chuo. Utaiona mnapomaliza chuo. Ndo utajua nani wa kimataifa nani wa Mtakatifu Kayumba.
 
Unajua ni Tanzania tu pekee ndio watu wake hufikiria mtu anayejua kiingereza au lugha ngeni ndio amefanikiwa kimaisha.
Bahati nzuri nilipata exposure ya kukaa na watu wa mataifa mbalimbali ya Ulaya na Asia.
Yaani ukiwaambia unataka kwenda kusoma ili ujue lugha ya kigeni watakucheka sana hadi mbavu zao ziwaume halafu mwisho watakuona limbukeni na kuachana na wewe.
Wao wanachokifanya wakienda ugenini nchi yoyote ile iwe ya kifaransa ama kiarabu au hata ya kiswahili wakifika watajifunza muda huo huo kwa kujichanganya na raia wa nchi hiyo.
Na mimi baada ya kuligundua hilo niliachana na ule ulimbukeni wa kysujudu lugha au kumuona mtu ni kichwa kwa sababu anajua lugha fulani,kwa hiyo ninachokifanya na mimi nikienda ugenini najifunza lugha yao muda huo huo.
Sio vizuri kwenye mada nzuri kama hii kuweka siasa ila utanisamehe.....Tundu Lissu na Cahadema ndio vinara wa ujinga huu wa kuwa wanajua kiingereza ndio wasomi sana!
 
Hahaa...mtoto akiwa bright huhitaji kumpeleka mashule yenye majina makubwa sijui ada mil. 10. Mwache hapo hapo ila habari yake wataipata tu kwenye matokeo ya kitaifa. Mimi ilinigharimu niliposoma O-level private ambapo kila kipindi mwalimu anaingia, shida ikaja A-level mwalimu humwoni na material unajitafutia. Kwenye mazingira kama hayo ndo utamwona mwanafunzi ambaye ni kichwa.....
Nadhani hujamuelewa mtoa mada amesema int schools zinafundisha analytical skills, creativity, reasoning , logic nk
Amesema tuachane na exam based schools
Kupata A haimaanishi ndio unaakili Sana .
Tunatakiwa tuachane na Mambo ya kuangalia mtoto kwenye mtihani kapata A na kutunga mitihani ambayo haimsaidii mtoto ku reason Wala kuwa mbunifu na kujua jinsi ya kutatua matatizo yake (problkem solving)

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Sijui unakubaliana nami ama unanipinga?
Wewe unaonaje?

Naeleza matatizo ya elimu za kukariri mambo na kudesa bila critical thinking.

Elimu inatoa mtu ana Ph.D lakini huwezi kujua hilo kwa kumsikiliza au kuangalia kazi yake.

Mpaka uambiwe huyu ana Ph.D, unauliza huyu naye ana Ph.D? Hapo hapo unaishusha thamani Ph.D ya Tanzania.
 
Hahaa...mtoto akiwa bright huhitaji kumpeleka mashule yenye majina makubwa sijui ada mil. 10. Mwache hapo hapo ila habari yake wataipata tu kwenye matokeo ya kitaifa. Mimi ilinigharimu niliposoma O-level private ambapo kila kipindi mwalimu anaingia, shida ikaja A-level mwalimu humwoni na material unajitafutia. Kwenye mazingira kama hayo ndo utamwona mwanafunzi ambaye ni kichwa.....
Hayo matokeo ya kitaifa ndio hayo tunayoyakataa
NI exam based
Angalia ma graduate wanapikea wako mtaani na GPA nzuri kabisaa kisa walisema wafaulu mtihani was taifa hawana skills za ku analyse Mambo
Hawako creative
Hawawezi kutatua matatizo yanayowazunguka
Wanaweza kuaniriwa ofisini tu kisa wamefaulu mtihani was taifa
Tunatakiwa kubadilika

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Nadhani hujamuelewa mtoa mada amesema int schools zinafundisha analytical skills, creativity, reasoning , logic nk
Amesema tuachane na exam based schools
Kupata A haimaanishi ndio unaakili Sana .
Tunatakiwa tuachane na Mambo ya kuangalia mtoto kwenye mtihani kapata A na kutunga mitihani ambayo haimsaidii mtoto ku reason Wala kuwa mbunifu na kujua jinsi ya kutatua matatizo yake (problkem solving)

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Lazima kuwa makini na mitazamo ambayo wanaweza kumjengea kijana, hususan maswala ya ushoga na upotofu mwingine wa kimaadili ya kitanzania na kibinadamu kiujumla.
 
Lazima kuwa makini na mitazamo ambayo wanaweza kumjengea kijana, hususan maswala ya ushoga na upotofu mwingine wa kimaadili ya kitanzania na kibinadamu kiujumla.
Hivi maadili ya kitanzania ni yapi hasa, ambayo hao wazungu hawana?

Manake naona wenzetu wana maadili kuliko sisi, Sisi tuna uvivu mwingi, hatujali muda, wizi wizi tukipewa nafasi n.k

Labda maadili ya kimaskini ndio tunayo.
 
Kichwa kwenye kumeza au? Kichwa gani kwa maana huyo kichwa atatoka na one kali halafu atakutana chuo kimoja na yule aliyepata division three na wote watapata mkopo na wote watasoma chuo kwenye carriers zao na wote watamaliza na kupata cheti.
Sasa hapa najiuliza faida ya kuwa kichwa ni nini hasa na je? Kuna faida ganinya kuwa na special schools?
Tofauti huwa ni kubwa sana kati ya mwanafunzi mwenye uelewa wa kawaida na yule mwenye uelewa wa juu. Yeye atatumia nusu saa kuelewa material ambayo wewe itakubidi kukesha ili uambulie chochote..
 
Hapa nimehakikisha kabisa wewe ni wale waliosoma shule za kukariri. Focus yako iko kwenye kupass mitihani wakati mwenzako anaongelea kitu kingine kabisa. Shule nyingi za Bongo zimejikita kwenye kukaririsha wanafunzi ili wa pass mtihani kwa gharama yoyote lakini unakuta hawana upeo wa kuchambua mambo.... kama wewe!
Huwezi kufaulu katika viwango vya juu kama huna hizo analytical skills, hakuna mitihani inayotungwa kwa ajili ya wanafunzi wanaokariri labda ujitungie mwenyewe.
 
Back
Top Bottom