DA HUSTLA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2012
- 3,805
- 4,107
Jidanganye tuLione hili nalo bichwa kama Lisu.
Kujieleza kwa kiingereza siyo kigezo cha kuelimika .
Kiingereza ni lugha tu kama kisukuma
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jidanganye tuLione hili nalo bichwa kama Lisu.
Kujieleza kwa kiingereza siyo kigezo cha kuelimika .
Kiingereza ni lugha tu kama kisukuma
Mtoto akifeli IST ni sawa na mtu umechana mkeka,tena sio umechana bali ni Umeurarua mkeka,Unaletewa taaarifa na uongozi mwanao anatakiwa arudie mwaka mzima,mwaka ambao ADA na makorokoro yote ni 23.5M - 25M Hii kama sio kurarua mkeka ni nini?
utabeba zege mwaka mzima ila ada ya kupeleka mtoto international hutoipata,yani ubebe zege utegemee kusomesha mtoto international? labda kama karai 1 la zege watakua wanakulipa 500k per trip sio eti ulipwe 20k - 30k utegemee utasogelea hata joining instruction ya International.umeongea kweli mkuu liwe jua iwe mvua mwanangu kamwe hawezi soma hizi kayumba hata zege nitabeba.
sikatai mkuu ndio mana nimesema hapa duniani kuna vitu hatujaumbiwa binadamu kama mimi,yani kuna vitu kwenye hii dunia vipo tuvisikie na kuviangalia tu.Kaangalie tena kwenye website ya IST. Karo inazidi hiyo uliyotaja kwa mbali sana.
Ph.D kama ya Magufuli ni kielelezo kwamba Ph.D si lazima iwe usomi.Unajifariji tu. Scholarship unapata lakini haina maana kuwa ubora wako uko kama wa graduate wa IST. Walimu wanafundisha hapo chuo kikuu lakini hawawezi kujieleza kwa Kiingereza na wamepata skolaship za UK, US, Australia.. wamefanya PhD nk huko.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] multiple choice hesabu bila calculations shida serikali inaangalia idadi ya watu wengi wamaluze tu shule hata Kama hawajui kusoma. Siasa mbaya kila mtendaji serikalini hataki kutumbuliwa Bora tu hata Kama hujui kusoma ufaulishweHao wabunifu wa serikali nao wamepita mashule hayo hayo ya kukariri, watabuni nini? ndio hao hao wanaokuja na maswali ya multiplechoice hadi kwenye somo la hisabati.
Ph.D kama ya Magufuli ni kielelezo kwamba Ph.D si lazima iwe usomi.
Kwa mfano.Magufuli ana matatizo ya kujieleza, Kiingereza na Kiswahili. Maana ingekuwa Kiingereza tungesema ni lugha ya kigeni.
Na hapo unaweza kuona tatizo la elimu za kukariri mambo badala ya kuelewa.
Tofauti huwezi kuiona chuo. Utaiona mnapomaliza chuo. Ndo utajua nani wa kimataifa nani wa Mtakatifu Kayumba.Mimi sizikubali sana hizo international school kwasababu mkifika Chuo kikuu,hakuna Significance difference ya wale waliosoma St.Kayumba na waliosoma International.
Sio vizuri kwenye mada nzuri kama hii kuweka siasa ila utanisamehe.....Tundu Lissu na Cahadema ndio vinara wa ujinga huu wa kuwa wanajua kiingereza ndio wasomi sana!Unajua ni Tanzania tu pekee ndio watu wake hufikiria mtu anayejua kiingereza au lugha ngeni ndio amefanikiwa kimaisha.
Bahati nzuri nilipata exposure ya kukaa na watu wa mataifa mbalimbali ya Ulaya na Asia.
Yaani ukiwaambia unataka kwenda kusoma ili ujue lugha ya kigeni watakucheka sana hadi mbavu zao ziwaume halafu mwisho watakuona limbukeni na kuachana na wewe.
Wao wanachokifanya wakienda ugenini nchi yoyote ile iwe ya kifaransa ama kiarabu au hata ya kiswahili wakifika watajifunza muda huo huo kwa kujichanganya na raia wa nchi hiyo.
Na mimi baada ya kuligundua hilo niliachana na ule ulimbukeni wa kysujudu lugha au kumuona mtu ni kichwa kwa sababu anajua lugha fulani,kwa hiyo ninachokifanya na mimi nikienda ugenini najifunza lugha yao muda huo huo.
Nadhani hujamuelewa mtoa mada amesema int schools zinafundisha analytical skills, creativity, reasoning , logic nkHahaa...mtoto akiwa bright huhitaji kumpeleka mashule yenye majina makubwa sijui ada mil. 10. Mwache hapo hapo ila habari yake wataipata tu kwenye matokeo ya kitaifa. Mimi ilinigharimu niliposoma O-level private ambapo kila kipindi mwalimu anaingia, shida ikaja A-level mwalimu humwoni na material unajitafutia. Kwenye mazingira kama hayo ndo utamwona mwanafunzi ambaye ni kichwa.....
Wewe unaonaje?Sijui unakubaliana nami ama unanipinga?
Hayo matokeo ya kitaifa ndio hayo tunayoyakataaHahaa...mtoto akiwa bright huhitaji kumpeleka mashule yenye majina makubwa sijui ada mil. 10. Mwache hapo hapo ila habari yake wataipata tu kwenye matokeo ya kitaifa. Mimi ilinigharimu niliposoma O-level private ambapo kila kipindi mwalimu anaingia, shida ikaja A-level mwalimu humwoni na material unajitafutia. Kwenye mazingira kama hayo ndo utamwona mwanafunzi ambaye ni kichwa.....
Lazima kuwa makini na mitazamo ambayo wanaweza kumjengea kijana, hususan maswala ya ushoga na upotofu mwingine wa kimaadili ya kitanzania na kibinadamu kiujumla.Nadhani hujamuelewa mtoa mada amesema int schools zinafundisha analytical skills, creativity, reasoning , logic nk
Amesema tuachane na exam based schools
Kupata A haimaanishi ndio unaakili Sana .
Tunatakiwa tuachane na Mambo ya kuangalia mtoto kwenye mtihani kapata A na kutunga mitihani ambayo haimsaidii mtoto ku reason Wala kuwa mbunifu na kujua jinsi ya kutatua matatizo yake (problkem solving)
Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Hivi maadili ya kitanzania ni yapi hasa, ambayo hao wazungu hawana?Lazima kuwa makini na mitazamo ambayo wanaweza kumjengea kijana, hususan maswala ya ushoga na upotofu mwingine wa kimaadili ya kitanzania na kibinadamu kiujumla.
Tofauti huwa ni kubwa sana kati ya mwanafunzi mwenye uelewa wa kawaida na yule mwenye uelewa wa juu. Yeye atatumia nusu saa kuelewa material ambayo wewe itakubidi kukesha ili uambulie chochote..Kichwa kwenye kumeza au? Kichwa gani kwa maana huyo kichwa atatoka na one kali halafu atakutana chuo kimoja na yule aliyepata division three na wote watapata mkopo na wote watasoma chuo kwenye carriers zao na wote watamaliza na kupata cheti.
Sasa hapa najiuliza faida ya kuwa kichwa ni nini hasa na je? Kuna faida ganinya kuwa na special schools?
Huwezi kufaulu katika viwango vya juu kama huna hizo analytical skills, hakuna mitihani inayotungwa kwa ajili ya wanafunzi wanaokariri labda ujitungie mwenyewe.Hapa nimehakikisha kabisa wewe ni wale waliosoma shule za kukariri. Focus yako iko kwenye kupass mitihani wakati mwenzako anaongelea kitu kingine kabisa. Shule nyingi za Bongo zimejikita kwenye kukaririsha wanafunzi ili wa pass mtihani kwa gharama yoyote lakini unakuta hawana upeo wa kuchambua mambo.... kama wewe!