Unaeleza dhana usiyoijua.
Maskini ndio anaweza kuishi bila tajiri ila kamwe tajiri hawezi kuishi Bila Maskini.
Tajiri anaweza kuishi bila maskini.
Kama maskini anaweza kuishi bila tajiri hata tajiri anaweza kuishi bila maskini.
Kuwa tajiri hakuzuii mtu kufanya kazi fulani.
Binadamu wote tungekuwa matajiri, bado kuna kazi tungehitaji kuzifanya bila kujali utajiri wetu.
Mazingira huchafuka, lazima tunge lazimika kuyafanyia usafi hata kama binadamu wote ni matajiri.
Tunahitaji barabara, kama binadamu wote tungekuwa matajiri, bado tunge lazimika tu, kujenga hizo barabara bila kujali utajiri wetu.
Binadamu wote kuwa matajiri sio kigezo cha kuacha kufanya kazi.
Lazima ujue umaskini ni Older than utajiri. Lazima ujue utajiri unazaliwa na umaskini. Yaani utajiri umenyonya ziwa la Umaskini. Ndio maana ili uwe tajiri itakupasa ufanye jitihada. Lakini sio kwa umaskini.
Hata kuwa maskini kuna vitu lazima uvifanye ndio uwe maskini. Umaskini hauji hivihivi tu.
Ili uwe maskini lazima uwe na mipango mibovu, uvivu, ujinga na maamuzi mabovu, mazingira duni.
Utajiri
hauzaliwi na umaskini.
Utajiri unazaliwa na mipango thabiti, maarifa chanya, fikra bunifu, maamuzi sahihi na mazingira wezeshi.
Are you there?
Maskini hana anachopoteza asipomtegemea Tajiri. Ataishi maisha ya kimaskini kama wanyama. Lakini tajiri hawezi kuishi bila maskini, kwani anahitaji cheap labour wakumzalishia, wakununua bidhaa zake, kumtumikia, n.k.
Nafikiri hujui msingi wa utajiri ni nini. Na hiyo inaweza kuonyesha bado hata wewe kwa tajiri itakusumbua.
Utajiri unahitaji rasilimali watu, kutumia muda wa watu wengine, na ujuzi wao kukuzalishia n.k.
Hata umaskini unahitaji rasilimali watu. Ndio maana hakuna wanyama maskini.
Umaskini ni wa binadamu na utajiri ni wa binadamu huyohuyo.
Alafu unasema watu waache ubinafsi, 😂😂 sasa eleza mtu anakuaje tajiri bila ubinafsi na kunyonya wengine? Utajiri ni tafsiri ya ubinafsi na kunyonya wengine.
Kwa nini wewe ukubali kunyonywa na wengine?
Hivi kama kila binadamu angekataa na kupinga kunyonywa, ina maana kusingekuwa na matajiri?
Kwa sababu hakuna ubinafsi na unyonyaji?
Aliyekwambia utajiri ni ubinafsi na unyonyaji ni nani?
Unajua kanuni za matajiri?
Maskini anavyotumia internet, nguo, vyakula au bidhaa vingine hatumii kanuni za matajiri. Ndio maana maskini wanamatumizi makubwa kuliko Matajiri lakini najua huwezi elewa.
Wanavitumia na kuvihitaji kwa kanuni na matumizi yapi?
Wangekuwa hawawezi kuhudumia watoto watoto wangekufa.
Kuzaa na kukuza watoto hakuna uhusiano na utajiri au umaskini.
Kuzaa na kukuza mtoto ni nature inahitaji hivyo. Na nature inatoa rasilimali zote kwa viumbe wake kuzaliana.
Wewe sema kuzaa ni nature, Halafu uzae mtoto tuone kama hiyo
nature italipa bills.
Nature haijui wewe ni maskini au tajiri. Mtoto akishazaliwa pesa inahitajika. Lazima uwe na pesa za kumhudumia huyo mtoto.
Alafu kingine utajiri na umaskini kwa sehemu kubwa ni suala la mindset. Sijui kama unaelewa hilo.
Au shule imeshaku-program?
Nakwambia hivi dunia inaweza kuendelea bila kuwapo maskini.