Mtuhumiwa wa Ubakaji amwambia Mwandishi wa Habari “Afu we Camera man nikimaliza kesi ntakutafuta”

Mtuhumiwa wa Ubakaji amwambia Mwandishi wa Habari “Afu we Camera man nikimaliza kesi ntakutafuta”

Hilo ndiyo haiba ya maafande wa jeiwii kwa 95%.
Tukiachana na uhalifu wao, hiyo ni nzuri.

Askari hatakiwi kuwa mnyonge, until the last drop of blood, he should be proud.

Nafikiri umenielewa ninachotaka kueleza hapa.

Ninaona kwamba askari wetu wa TPDF wanapata mafunzo stahiki.
 
Nimekwambia hakuna kesi hapo
Ushahidi haupo
Wa kuwatia hatiani akina nyundo
Me sio mwanasheria ila hii kesi hunifungi
Kwa nini? Aliebakwa akiwatambua kwa sura kwamba ni hawa walionibaka na kunifira, hakimu atataka ushahidi gani tena?

Hebu mtag mwanasheria unaemfahamu humu jamvini atusaidie.
 
Umeandika kitu ambacho kwa mara ya kwanza niliposikiliza hiyo clip nilikiona, MALEZI MABAYA hivi nguvu ya kujibu vile kaitoa wapi? Hao madogo wasichoelewa sasa hivi wanasiasa wanacheza na upepo wa wananchi sanaa hao WATAFUNGWA TU kwa vyovyote ili tu kuwapa watu imani na serikali hao madogo kwa malezi yao duni waliyoyapata ipo siku akili itawakaa sawa
Kweli ipo siku akili itawakaa sawa.

Ila nimeona tangu Jana nyundo amepunguza mbwembwe.
 
Nikikumbuka binamu yangu alikuwa akijiamini hivi hivi lakn mwisho wa siku akapigwa 30, Sina hamu.
Tulipokata rufaa ndio Kwanza akaongezewa shtaka lingine na miaka ikaongezwa mitano jumla 35. Ndio Kwanza amemaliza miezi 6.
Tangu hapo nikajifunza mahakamani si pakuleta mizaha.
Binamu Yako hakua na connection Sasa huyo ni askari na anajua hawezi fungwa mpaka anatamba mbele ya askari wenzie na askari tanzania hii anapigwa magoti huoni anapelekwa kama bwana harusi tanzania hii askari anaabudiwa
 
Kwa nini? Aliebakwa akiwatambua kwa sura kwamba ni hawa walionibaka na kunifira, hakimu atataka ushahidi gani tena?

Hebu mtag mwanasheria unaemfahamu humu jamvini atusaidie.
Na waliombaka wakikana, huyo shahidi atadhibitishaje
 
Watuhumiwa wanne wa kesi ya Ubakaji na ulawiti ambao ni Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) MT 140105 Clinton Damas maarufu Nyundo, Amini Lema maarufu Kindamba, Nickson Jackson maarufu Machuche na Askari wa Jeshi la Magereza C 1693 Praygod Mushi wakiondolewa mahakamani jioni hii kurudishwa mahabusu mpaka Agosti 28, 2024 ambapo kesi hiyo itaendelea tena.

Nyundo na wenzake wakati wakitoka Mahakamani mmoja wao alisikika akimwambia Cameraman kuwa akifanikiwa kumaliza kesi yao atamtafuta "Wewe cameraman nikimaliza kesi nitakutafuta" Endelea Kufuatilia kurasa Zetu kufahamu Kuhusu kilichojiri Mahakamani kuhusu Kesi hii leo Agosti 23, 2024.

🤣🤣🤣🤣👆
 
Anataka kumtafuta ili amwambie ukweli nani aliyebaka au anammaindi mpiga picha ili amfile? Nashauri huyu askari akamatwe ili aulizwe ni nini anataka kufanya kwa huyu Cameraman.
 
Back
Top Bottom