Muda sahihi wa kuiweka Dar es Salaam kwenye “lockdown” ni sasa

Muda sahihi wa kuiweka Dar es Salaam kwenye “lockdown” ni sasa

mike2k,
Hapana rais amesema tuchape kazi lockdown kwa Dar kuna vitongoji 8 vinatutegemea haukusikia?🎤🎤🎤🎤
 
Mkuu kwa wale watu wa Dar watanielewa kwamba kupeana nauli na kununuliana chakula ni kitu cha kawaida sana na kimesha zoeleka
Hivi katika umri wako wote ushawahi kuona hata mara moja abiria mmoja kutoa hela kwenye daladala na kulipia watu nauli kwa kujitolea tu?
 
Wazungu wanakufa pamoja na lockdown zao!

Wewe mswahili usiyejua Kesho utakula nini unajifanya unataka lockdown!

Kwanza vijumba tu vilivyopangana huko, huwezi kujua kama watu wako lockdown au wako pagarani! Vijumba kama slums!

Ukitoka mlango huu ukiingia mlango mwingine umeshafika chumbani kwa jirani! Ukikatiza dirisha la pili sentimeta tano umeshafika dukani kwa mangi!

Hiyo lockdown itakuwa kituko!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu weng ambao wanatka lock down ni watu ambao kidg kiuchumi wako vizuri au wanategemea mishaara .sasa mtu kama mimi ambaye nategemea nikatafte labda 5000 uko mjin nije nile ukinifungia ndani utaniua tu na ndo maisha ya watanzania yalio wengi na umeona kenya wanavoipinga io lock down haswa walala hoi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga hoja mkono
Siungi mkono hoja! Hali na mazingira yetu hayaruhusu hatua hiyo ya kuliweka jiji katika karantini. Madhara ya kufanya hivyo ni mabaya zaidi kuliko corona yenyewe! Tusichukue hatua kwa kuiga wengine.

Kama kila mmoja atazingatia maelekezzo ya serikali ya kujikinga na kuwakinga wengine, tutaishinda corona!

Watu wasijifanye kuwa ndo wanaijali sana kuliko Rais wetu au kuliko wataalamu wa wizara ya afya!! Wengi humu hawajui hata madhara mapana ya total lockdown.

Nchi zilizoendelea asiye na kazi anapewa posho. Sisi sehemu kubwa ya watu wasipofanya kazi kwa siku tatu tu wanakosa hata buku ya kununulia nusu kilo ya sembe, halafu uwafungie kwa zaidi ya miezi mieili kama huko Wuhan China, si utszika kwa malaki wala si kwa mamia kwa siku!!

Halafu uchumi ukifa kwa kutofanya kazi unahitaji kuuinua kwa nchi kuingiza pesa kwenye taasisi na makampuni yaliyokufa ili kuyafufua! Halafu siyo pesa ndogo. USA wameidhinisha dola trilioni 5, Japan trilioni 1, Uingereza pua takriban dola trilioni 1. Sasa bongo tukiwaiga hao tutauinuaje uchumi wetu utakaoathirika? Mungu wetu atatusaidia!!

Kama kuna wakati Rais Magufuli amekuwa wa msaada sana kwa nchi yetu ni katika kipindi hiki!! Yawezekana kabisa Mungu alimwandaa ili aliongoze na kulivusha Taifa letu kwenye kipindi kigumu kama hiki. Ninamwombea afya njema na maisha marefu.
 
PNC, Anashindwa vipi ye na family yake kujifungia ndani?

Senti bai yuzingi tecno T301
 
Kama mnataka lock down, fanyeni iwe binafsi. Yaani kaeni nyie na familia zenu ndani.

Waacheni watanzania waendelee na shughuri zao za kila siku ila kwa kuchukua tahadhari.

Wa kukaa ndani, akae asikatazwe

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana!! Huzuiwi MTU ns familia yako kujiwekea lock down/ kujifungia!! Mtoa uzi anza wewe na familis yako kujifungia kwa uaminifu kwa wiki 4 halafu njoo hapa utupe mrejesho!!
 
mbingunikwetu,
Inaonekana upo kwa ajili ya kusifu

Nani kakwambia anayependekeza lockdown anataka majanga zaidi? Hata mm sikubali total lockdown unayowaza wewe ya kila kitu kisimame.

Namaanisha dar iwekwe kwenye lockdown na miji mingine pia. Magari ya mizigo yafanye kazi, biashara ndani ya dar na miji mingine iendelee ila watu wasisafiri kabisa kuingia na kutoka kwa kutumia mabasi, ndege au meli, wakae ndani ya miji yao.
Raisi ameliona hili na ameshazuia usafiri wa anga.
 
Kwako Mkuu wa mkoa wa Dar au mamlaka ya juu (rais)

Kwa kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 na takwimu zinazotolewa kila siku na Mheshimiwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, ni dhahiri kuwa jiji la Dar limekuwa kitovu cha ugonjwa huu hapa nchini. Kila siku idadi ya wagonjwa inapanda kwa kazi sana.

Nashauri mamlaka husika mfuate ushauri wangu ili kupunguza kazi ya maambukizi nchi nzima.

Ikiwapendeza au ikiwezekana ushauri huu ufanyiwe kazi mapema iwezekanavyo kwa kuwa kila siku mabasi na vyombo vya abiria vinaingiza na kutoa watu kwenye hilo jiji.

Naomba kuungwa mkono.

Nawasilisha.
 
Kwako Mkuu wa mkoa wa Dar au mamlaka ya juu (rais)

Kwa kazi ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 na takwimu zinazotolewa kila siku na mheshimiwa waziri wa afya Ummy Mwalimu, ni dhahiri kuwa jiji la Dar limekuwa kitovu cha ugonjwa huu hapa nchini.

Nashauri mamlaka husika mfuate ushauri wangu ili kupunguza kazi ya maambukizi nchi nzima.

Ikiwapendeza au ikiwezekana ushauri huu ufanyiwe kazi mapema iwezekanavyo kwa kuwa kila siku mabasi na vyombo vya abiria vinaingiza na kutoa watu kwenye hilo jiji.

Naomba kuungwa mkono.

Nawasilisha.
Ukipuuza ushauri wa kitaalamu au usubiri hadi Serikali itakapoweka karantini, kama unavyoshauri, utaambukizwa na kupoteza maisha.

Ni wajibu na jukumu la kila mwananchi kulinda afya yake.
 
Back
Top Bottom