PreGE2025 Muda uliobaki kabla ya uchaguzi mkuu unawatosha G55 kuanzisha chama chao kipya kushiriki uchaguzi?

PreGE2025 Muda uliobaki kabla ya uchaguzi mkuu unawatosha G55 kuanzisha chama chao kipya kushiriki uchaguzi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Sio CCM tu vyama vyote havitaki (Ukiowaondolea hilo unawapunguzia Kete yao muhimu sana) : Ya kwamba fanya hivi au tutakufukuza na tukikufukuza na Ubunge hata kama unao unaupoteza
Wapi huko ukifukuzwa uanachama unapoteza ubunge?
 
Lissu ni mpinzani wa kweli, wale njaa wote wameanza kutoa milio
 
Abduli awaanzishie chama kiitwe Nani kama Mama Party.
 
We unadhani kwanini wagombea binafsi wanapingwa na chama dola?
Kwa sababu watazigawanya na kupunguza kura za wagombea wao na kuwaongezea ugumu zaidi katika uchaguzi.

Wagombea wa chama tawala mara nyingi huwa wanateuliwa kutokea makao makuu ya chama na "wakubwa", unakuta mtu ameshinda kwa kura za wanachama au wajumbe kuwa mpeperusha bendera wa chama katika ubunge majina yakipelekwa makao makuu la kwake halirudi, wamemkata na kumteua mtu aliyekuwa nafasi ya tatu huko, sasa huyo mshindi aliyekatwa akienda kugombea kama mgombea binafsi lazima iwe shida kwa chama tawala japo kushinda ni vigumu pia.
 
Back
Top Bottom