Mufindi: Afungwa Jela miaka 20 kwa kukutwa na kilo 32 za nyama ya Tandala

Kilo 32 eti thamani yake milioni 7,3..........
Yaani kila kilo sh laki mbili na zaidi.
Uongo uliokubuhu huu.
Pole yake, tulimwambia hizi nyama za porini ni kwaajili ya wazungu na waarabu yeye hakusikia.
Daah.... Ndo basi tena
 
Gharama ya hizo kilo 30 inalingana na gharama za kumtunza huyo mfungwa kwa miaka 30?
 
Kilo 32 eti thamani yake milioni 7,3..........
Yaani kila kilo sh laki mbili na zaidi.
Uongo uliokubuhu huu.
Pole yake, tulimwambia hizi nyama za porini ni kwaajili ya wazungu na waarabu yeye hakusikia.
Daah.... Ndo basi tena
Kama hamjui
Kesi hizi husimamiwa na wale jamaa wenye kinga ya kesi za mauaji.....

Najua mnanifuatilia. Siogopi kusema


Acheni kutumia risasi kuua nzi huku mafisi mkiwazawadia mabucha
 
Kwani mkikutwa na watu wa misitu au game hata na njiwa unajua ukatili ambao Huwa wanawafanyia watu?
 
Na sheria za kulinda wanyamapori ni Kali
 
Kweli wewe ni Mpemba, nyama pori tunauwa kwa risasi na haipimwi popote, usiongee kitu usichokijuwa.

Nimefanya professional hunting na kampuni na nimefanya local hunting tunajiorganise wenyewe.

Hapa naandika kitu ambacho nakijuwa fika na nimekiishi tangu nikiwa Mdogo.

Wanyama wanaopimwa ni nyama za machinjioni kwenye mifugo ya kufugwa, mambo ya wildlife tuachie wenyewe hujui lolote.
 
Tumia akili.Nyama zikiuzwa holela,na kusmbukiza maradhi binadamu,wewe na wenzako,ndio mtakuwa wa kwanza kulaumu serekali.Nyama lazima ipimwe,mnyama kafa ana maradhi ya kuambukiza,au siyo.
Nyama pori haipimwi wala wanyamapori hawapigwi sindano za chanjo, usidanganywe.
 
Mdogo wake rostam mnakumbuka ile kesi yake ya nyara za taifa mwaka 2019?
Mimi Niko hapa kunyoosha ukweli, nothing but the truth.

Rostam Ana kampuni ya uwindaji inaitwa miombo Safari ipo Masaki, kwa kampuni za uwindaji store zao huwezi kukosa nyala na bunduki nyingi tu na vyote ni halali.

Zile zilikuwa ni siasa chafu za Magufuli kupora pesa wafanyabiashara hakuna kingine.

Siwapendi kabisa hawa kina Rostam lakini ukweli halisi ndio huu lazima tuuweke wazi.
 
Kilo 32 eti thamani yake milioni 7,3..........
Yaani kila kilo sh laki mbili na zaidi.
Uongo uliokubuhu huu.
Pole yake, tulimwambia hizi nyama za porini ni kwaajili ya wazungu na waarabu yeye hakusikia.
Daah.... Ndo basi tena
- Sheria ya Trophy valuation, inasema hivi kwenye kuthaminisha thamani ya mnyama pori, tunaangalia thamani ile ya jumla ya mnyama, kwa mfano ukikutwa na nyama hata kilo1 ya nyama ya mnyamapori mwenye thamani ya shilingi Milioni 10, hatuangalii thamani ya kilo Moja ya huyo mnyamapori tunaangalia thamani ya mnyama wote.
 
Ni kosa kubwa kula nyama anayokula sultan (dubei🤣)

Ndugu yetu yamemkuta. Loh
Kina mzee mmnoja aliwahi niambia kua tz mwisho wa kula vyakuka vizur ilikua ni enzi za Nyerere, sahii vitu org vinapelekwa hukoooo
 
Kweli mkuu kama yule Mchina juzikati hapo alipigwa Fine ya Laki mbili tu. Huu ni uonevu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…