Uchaguzi 2020 Mufti Mkuu wa Waislamu Sheikh Zuberi leo Korogwe mbele ya Rais Magufuli

Uchaguzi 2020 Mufti Mkuu wa Waislamu Sheikh Zuberi leo Korogwe mbele ya Rais Magufuli

Nawashangaa waislam mnaomuongelea vibaya Mufti wakati mtume wa allah aliagiza muheshimu na kuwafata viongozi hata kama ni mtu mweusi mwenye kichwa kama zabibu

Allah's Messenger (ﷺ) said, "You should listen to and obey, your ruler even if he was an Ethiopian (black) slave whose head looks like a raisin."Sahih
Unfortunately he is not our ruler
Tanzanian Ruler is Magufuli
Watu wanafiki wanapenda kupitisha fatwa za kinafiki
Huyu ni kiongozi wa taasisi ya kiislamu inayoitwa BAKWATA
Sio mtawala wa nchi
Tafadhali ni haram kumzushia Mtume SAW uongo
 
Kuna watu wanajificha kwenye vivuli vya dini kwa maslahi yao binafsi ila ukiwaangalia matendo yao hawana hiyo "dini"

Mmoja wapo ni huyu Sheikh! Hatutakiwi kuhukumu ila kwa huyu Sheikh wa BAKWATA hakuna namna

Allah Anisamehe
 
Wewe ni Mufti wa Tanzania lakini pia hapo hapo Wewe ni Kiongozi Mkuu wa Kiimani nchini Tanzania bila kujali hata Sisi akina GENTAMYCINE ambaye ni Mkristo tena wa 'Dhehebu' la Katoliki kabisa. Nakuheshimu Wewe ( japo ni Muislamu ) kama vile ninavyomuamini Kadinali wangu wa Ukatoliki nchini. Na nimesikitika pia kuona Watu wako wa Karibu 'hawakukushauri' katika hili.

Kitendo chako Mufti cha kupewa nafasi ya Kuzungumza mbele ya Mkuu wa nchi huko Tanga kisha 'Ukakemea' Kauli za 'Udini' zilizoonyeshwa Juzi na Jana na Kiongozi Mmoja wa Kiislamu Sheikh Ponda kisha hapo hapo na Wewe ukaanza Kuomba Msaada wa Ujenzi wa Barabara huko Mkoani Tanga huku ukiwananga wasiompenda Mgombea Urais wa CCM na Kumsifia ni Kosa Kubwa.

GENTAMYCINE sikatai Wewe ( Nyie ) Viongozi Wakuu tena wa Kitaifa wa hizi 'Dini' Kuu mbili hapa Tanzania za Uislamu na Ukristo kuwa na 'Itikadi' zenu za 'Kisiasa' ila kuziweka hadharani sidhani kama ni Jambo jema kwani linaweza 'Kuwagawa' Watu wenu na hata kuanzisha 'Mitafaruku' mingine ya Kiimani ( Kidini ) nchini. Acheni kupenda 'Kuwalamba' Miguu 'Wanasiasa' Mungu hakuwatumeni muwe hivyo.

Nimesikitika sana kwa ulichokifanya japo Mimi ni mwana CCM na ninamkubali sana Mgombea wangu Ndugu Dkt. John Pombe Magufuli ila kuonyesha Kwako wazi wazi kuwa 'Unamkubali' hadi Kumpigia 'Chapuo' vile sikubaliani nacho na kama wana CCM Wenzangu hapa JamiiForums 'mtanichukia' GENTAMYCINE kwa hili naamini Mwenyezi Mungu juu Mbinguni atanipenda zaidi.

Kila Siku nyie Viongozi Wakuu wa Kidini nchini Tanzania huwa 'mnatukanya' Watanzania kuingiza 'Udini' katika 'Siasa' ila cha 'Kushangaza;' nyie nyie Viongozi Wakuu wa Kidini ndiyo mnakuwa wa Kwanza 'Kuvuruga' huu ( huo ) utaratibu na Kutuonyesha ( Kututhibitishia ) kuwa si tu mna 'Unafiki' uliotukuka bali pia hamlitakii 'mema' kabisa Taifa hili na Ustawi wake wa Amani yake.

Ili Mufti Mkuu wa Tanzania nikuone na nikuamini kuwa Wewe si Mufti Mkuu wa Tanzania na Chama changu Cha Mapinduzi ( CCM ) nakuomba Kesho nikuone pia katika Mkutano wa Mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu, nikuone pia katika Mikutano ya Wagombea akina Lipumba wa CUF na wa Seif Sharrif Hamad wa ACT-Wazalendo hadi na Wagombea wengineo wote.

Kukipenda mno Chama changu cha CCM na Mgombea wake Urais JPM haimaanishi nikiona Jambo la 'Kipumbavu' basi nilinyamazie tu. Nimekereka!
Unastahili kuigwa na WaTz wenye uelewa . Na hasa Ile team kusifu na kuabudu
 
Labda wewe ulikua husikii kwa sababu unasubiri TBC ikuonyeshe
Ukweli ni kwamba
Kila siku ya ijumaa misikiti yote tunachanga hela kwa ajili ya wao na Familia zao isipokua misikiti ya BAKWATA
Kila ijumaa tunapata marejesho ya mateso makali wanayopewa jela
Kila ijumaa tunapata marejesho kuhusu barua tulizowaandikia viongozi wa serikali
Wewe huna Habari labda wewe ni muuminiin wa BAKWATA na Muft
Nani kakwambia wanashikiliwa kwa sababu za kiusalama?
Watu wa nazungumza Sana wakati wa kampeni kwa sababu kuna mgombea ameonyesha uadilifu anasikutishwa na dhulma hizo
Na kuna wengine hawasemi kitu wapo kimya kama vile hakuna kitu
Afadhali wangekiri au kukanusha
Sisi waislamu wa haki kura zetu kwa Lissu
Waislamu wanafiki kura kwa katili
Wewe ushafuatilia mijadala ya humu kuhusu hao masheikh wa Bakwata kabla ya kipindi hiki cha kampeni? Kuna watu tena wapinzani kabisa ila walikuwa wakipongeza serikali kwa kuwashikilia hao masheikh wa uamsho kwa madai walikuwa wakileta machafuko huko Zanzibar halafu et kipindi hiki cha kampeni ndio wanajifanya nao kuwazungumzia masheikh kuwa hawajatendewa haki kisa Lissu anataka kura za waislamu kazungumzia suala la masheikh wa uamsho.

Waislamu wana matatizo wana matatizo lukuki ila leo mnataka tukampigie kura Lissu kisa tu masheikh wa uamsho,hivi hamuoni kweli kama mnatumika? miaka yote hawa watu mbona hawakuwa wakipiga kelele kero zetu waislamu hadi wasubiri wakati wa uchaguzi?
 
Huwa wanasema muislam ndugu yake muislam, kwa hilo tu bado alikuwa na dhamana ya kuwasemea si tu waislam bali wale ni Masheikh wenzie.
Sasa mbona Sheikh Ponda anataka waislamu tumpigie kura Lissu wakati anajua kabisa Lissu ni kafiri hivyo hatuna udugu nae?

Kwanini asituambie tumpigie Hashimu Rungwe muislamu mwenzetu?
 
Sasa mbona Sheikh Ponda anataka waislamu tumpigie kura Lissu wakati anajua kabisa Lissu ni kafiri hivyo hatuna udugu nae?

Kwanini asituambie tumpigie Hashimu Rungwe muislamu mwenzetu?
Kwa hiyo huyo mufti anapowataka mumpigie Meko huyo mna udugu naye kwa mantiki yako ya ukafiri?

Halafu soma niliyemquote wala sikuzungumzia suala la kumpigia nani kura, niliyemjibu aliuliza uhalali wa mufti kuwasemea masheikh wa uamsho wakati hawapo chini ya BAKWATA ndipo nikamjibu bado angeweza kuwasemea kama waislam/masheikh wenzie.
 
Hawezi kutetea wachochezi wanataka kutuletea fujo za Somalia huku

Usihukumu Mkuu usije uka hukumiwa na wewe ,bila ya kujali umetenda Kosa au haukulitenda.Nenda taratibu na chunga sana Ndimi yako.
 
Huyu si muft wetu huyu ni muft wa BAKWATA tu wewe endelea na ibada zako wanafiki wasikuyumbishe
Kura za waislamu wa haki kwa lissu
Wanafiki kwa katili
Mm mapema tu kwa Lissu mm mpk Leo hii kiongozi wa wa dini ninaemuanini ni Ponda tu tokea zamani hawa wengine yaan wakisema jambo lolote sipotezi muda wangu kuwasikiliza wauni tu
 
Mufti ana familia yake, ana maisha yake. Ulitegemea aongee nini mbele ya mimbari ya dikteta?
 
Huyu ndio kiongozi mkuu wa Waislamu, huu ni msiba mzito.[/QUOTE]Bado watu japo wanajiita wasomi ipo sehemu ina shida barabara nzuri, Maji, Huduma za Afya Bora, Umeme, Maji, Elimu bora hivi vitu vipo kisheria na ni haki ya mwananchi haitakiwi kuombwa sijui shida ni elimu ya uraia au tumelogwa!?
 
Mufti ubwabwa tu masheikh wa kiislamu walioko gereza kwa mujibu wa Lissu ni karibu 200 na zaidi kwanini yeye yupo kimya? kama anashindwa kumkabili rais kwanini asijiuzulu?
 
Back
Top Bottom