Mufti sheikh Zuberi aitisha maombi ya siku tatu kwa Waislamu wote kuombea mvua

Mufti sheikh Zuberi aitisha maombi ya siku tatu kwa Waislamu wote kuombea mvua

Ingekuwa dua inafanya kazi hivyo, mbona uarabuni kusingekuwa na jangwa

Tumechoka na vimbwanga saizi tunataka wakiomba hiyo dua watutajie na tarehe na mwezi kabisa ambao Mungu wao kawaahidi mvua ataishusha ili ikitokea haijanyesha tujue ni uwongo

Hizi habari za kusema tunafanya dua mvua inyeshe na unaelewa kabisa kua tuko ukingoni mwa kiangazi tumekikaribia kifuku na ni wazi kabisa kua kifuku ni season ya mvua, kutuambia mvua imenyesha kwasababu ya dua yako huko ni kututapeli kizungu
Walikua wapi kuomba kipindi cha mwezi wa8 leo tarehe za vuli zimefika ndio wanajifanya kuomba dua ya mvua..waende jangwani saudia waombe mvua kama wana Mungu kweli.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mvua kunyesha ni muujiza, hao wenye muujiza ili tuone muujiza waiombe nchi, barabara zote ambazo hazina lami tumka tukute zina lami bila ushiriki wa mtu kujenga.

Ila kuomba kitu ambacho kinatokea kikitokea ni kawaida tu.
Yaani kuna binadamu, uwezo wao kufikiria ndipo ulipoishia... yaani wanafikiri kila kitakachotokea siku za mbeleni kuna uwezekano wa kubadilishwa kwa maombi... Ndio maana kuna mtaalam mmoja aliwahi kusema, kama kutakuwa kuna jiwe kubwa linakuja kuangukia kwenye uso wa dunia basi hawa wenzetu watakachofikiria ni kuomba usiku na mchana ili libadilishwe uelekeo... lakini those who think otherwise watakuwa wanatafakari watume chombo kikabadili uelekeo wa jiwe hilo kitu.
 
Hivi mvua kunyesha ni muujiza, hao wenye muujiza ili tuone muujiza waiombe nchi, barabara zote ambazo hazina lami tumka tukute zina lami bila ushiriki wa mtu kujenga.

Ila kuomba kitu ambacho kinatokea kikitokea ni kawaida tu.
Kama mvua ingekuwa inanyesha kwa kufuata hii filosofi basi tusingekuwa na majangwa... kwamba Congo kuwa nq mvua nyingi ni kwasababu wanaomba sana dua.... nonsense
 
Kiongozi mkuu wa waislamu Mufti Sheikh Zuberi aitisha maombi ya siku tatu kwa waislamu wote kuombea mvua yenye heri kuanzia kesho Alhamisi

Maaskofu wakristo naona wanashindana tu kuvaa barakoa hawaitishi maombi kulikoni?

Haki huinua taifa. Haki huleta baraka katika nchi. Haki hukufanya usilipwe baya kwa baya. Haki ni msingi wa kutendewa yaliyo mema. Tuombe/tutendeane haki kabla ya kuomba hivyo vidogo
 
Unadhani baba yako na mama yako na walipofanya mapenzi ndo wewe ukatoka kimiujiza?
Kama kulikuwa na mbegu za kiume milioni 150 alafu moja tu ndio ikatunga mimba hauoni kama hiyo ilikuwa ni kamari?... that is probability, kuna mbegu kibao potential zilichelewa... haina tofauti na bahati nasibu.
 
Mungu huangalia kiongozi kwanza, ndio maana ktk biblical kiongozi alipokuwa akikosea Taifa zima linaadhibiwa
Duh na hapo ndio alipokuwa anafeli... sitegemei kabisa kwa uwezo mkubwa anaotukuzwa nao alafu aka-behave kitoto hivi...
 
Kama kulikuwa na mbegu za kiume milioni 150 alafu moja tu ndio ikatunga mimba hauoni kama hiyo ilikuwa ni kamari?... that is probability, kuna mbegu kibao potential zilichelewa... haina tofauti na bahati nasibu.
Kwa hyo mbegu za mwanaume na yai la mwanamke vikikutana Basi mtoto anatokea tu?.
ingekuwa rahisi hivyo hata mawe na miti vingepata mimba vikimwagiwa mbegu
 
Hivi waisilamu wanaweza kuomba hadi muujiza ukatokea?

mtume wao aliwahi kufanya muujiza gani?
Majini million 1 yakitumwa kuleta Mvua ujue ni mafuriko.... So Majini 1,000 yanatosha kuleta Mvua ya kupunguza joto mjini.
 
Kwa hyo mbegu za mwanaume na yai la mwanamke vikikutana Basi mtoto anatokea tu?.
ingekuwa rahisi hivyo hata mawe na miti vingepata mimba vikimwagiwa mbegu
Hapana, bali huwa tunaomba dua alafu ndio inatokea, bila dua haiwezekani.
 
UAE wanatumia maji ya bahari ,sisi tuna sources za maji na umeme za kufa mtu lakini kuna mgao wa umeme na maji.
 
Hili Jambo ni La Kheri, Waislamu Wameliona kupitia Mufti ipo haja Ya Kumuomba Mungu Mwenyezi atunusuru....! Wala Mama hatukulaumu kwa Ukosefu huu Wa Mvua.

Hoja hapa ni moja tu kuwa WaTz tupo mchanganyiko, Kuna Waislamu,Budha,Hindu, Wakristo Wa Madhehebu mbalimbali na Wapagani pia Wapo...! Sasa Mpendwa Rais Samia Suluhu Hassan tunaomba Uwakumbushe WaTz Wote dini Zote tuingie Kwenye Maombi...! Maombi ya Kuliombea Taifa na Baa la Ukosefu Wa Mvua..!

Chonde tushikamane kwa pamoja dhidi Ya hili linaloathiri Taifa Zima..!
 
Hayo maombi yangeelekezwa kwenye Corona ingekuwa kheri badala yake wanaamini Sayansi.
Kwenye Mvua wanasema Twende kwa Mungu

Hawa hawa waliochoma chanjo ya Corona kuogopa kifo wanataka kuongoza maombi ya Mvua
Kama Chanjo mpango wa shetan haya maombi yatajibiwa yanayoongozwa na wachoma chanjo.

Raisi yeye anaamini Sayansi
 
Kwani miti shamba yake iliyomuokoa naliliu kule Lindi haiwezi kuleta mvua ?
 
Back
Top Bottom