Muhimu: Kanisa Katoliki lirudishe zawadi ya Hela Mil 20 lilizopewa na Serikali ili kujali Maumivu ya Dkt Kitima

Muhimu: Kanisa Katoliki lirudishe zawadi ya Hela Mil 20 lilizopewa na Serikali ili kujali Maumivu ya Dkt Kitima

Vinginevyo hawateleweka. Inavyoonekana hii vita ya haki inapiganwana maaskofu wachache sana wa katoliki, walio wengi ni walamba asali.

Bado nakumbuka jinsi askofu Kilaine alivyoyafaidi mabilioni ya mfanyabiashara Rugemalira enzi za Kikwete.

Wakatoliki tuungane kuupinga usaliii huu dhidi ya uhai wa Dr. Kitima. Yaani drm Kitima anaumiza na ccm , halafu mwingine apokea hongo hadharani toka kwa watesi wa Dr. Kitima

20M IRUDISHWE.
na kama hiyo hela inahitajika basi niko tayari kuichanga mimi binafsi, maana ninayo
 
Hapo kila anaye fungua mdomo lengo lake ni tumbo lishibe haijarishi ni ndani ya Imani ya dini au mdomo wa muumini! Katoliki ni taasisi inaendeshwa kwa taratibu na misingi inayozingatia haki za waumini wake, lkn je ni wote wanaishi na imani hizo? Sina ushahidi kuhusu 20M kama ni kwaajili ya aliye jehuriwa inamaana inawezekana imetolewa kama sadaka! Ni kweli tunahasira na mihemko lakini tupunguze kugombanisha serikali na viongozi wa kidini.
 
Hivi wanavyosema siasa isiwe makanisqni ,hivi mchimbi kaenda kufanya nini .Angetakiwa aingie asali aondoke na atoe mchango kama muumini mwingine aondoke .Kuutubia kwenye madhabahu sijaelewa
Yule father muchunguzi alisema, wanaingia makanisani wanaongea alafu habari inarushwa yao badala habari ya neno la Mungu iliyotolewa na mtumishi
 
Katibu wa TEC Father Kitima ameshambuliwa na Dunia nzima inafahamu nani ni mtuhumiwa (kasoro Polisi wa Tanzania), Sasa ni vema Kanisa likajitenga na wanaotuhumiwa, hakuna sababu yoyote ya kupokea hela za Watuhumiwa ili kupoza mambo, Uhai wa Kitima hauna thamani ya hela ndogo sana kama hiyo mil 20, hii ni kashfa kwa Kanisa.

Hatuna haja ya kusema Mengi kila kitu kinafahamika, na kwa vile serikali haina dini basi kukataa hela hiyo iliyojaa damu ya Kitima haiwezi kuwa Udini.

Ni Matarajio yangu kwamba Dr Mpango atarejeshewa hela yake ifikapo kesho asubuhi, Na wala hili halitakuwa la kwanza , Aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Kilaini alimrejeshea hela yake Rugemalila kwenye kashfa ya ESCROW.
Watu waovu hupenda sana kumkejeli Mungu wakidhani ataulinda UOVU wao...

Tukio la Rais Samia na pesa zake hizo (Milioni 20 akiziita za mafuta ya gari la Askofu) kumpa mtumishi wa Mungu ktk namna ya kutangaza hadharani, watu wasiojua na wenye tamaa ya kijipatia pesa bure waweza kudhani "Rais katoa sadaka..."

Ukweli ni kuwa siyo. Hiyo ni chambo ya mauti ya kiroho kwa Askofu huyo na Kanisa Katoliki Hiyo...

Kilicho nyuma ya pesa hiyo ni hatari. Kama hawajui au wamesahau, wamuulize Askofu wa KKKT Dr Shoo na ile 150,000,000 aliyoitoa huyu mama kwa mkono wa Freeman Mbowe inavyomtesa kiroho mpaka leo...

Pesa za huyu mama ni hatari. Zina sura zote za hongo na rushwa ya "fungeni midomo" ili kanisa lisione UOVU wowote ndani ya Rais huyu na serikali yake unaondelea sasa..

Biblia Neno la Mungu halijaacha kuyasema mambo haya...

Kwamba, hili tukio linafanana na lile lililorekodiwa ktk Biblia - kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya 8 kuwahusu Mtume Petro na Yohana na mchawi mmoja aitwaye Simioni aliyetaka kuwahonga Mitume hawa pesa kuficha UOVU wake...

Bahati njema Petro na Yohana walikuwa na Roho Mtakatifu ndani wa kuwawezesha kutambua hila na mikakati ya roho ya shetani kuharibu kazi ya Mungu...

Haya ndiyo majibu ya Mtume Petro kwa mchawi yule:


Matendo Ya Mitume 8:20-23 SUV

".....Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako. Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu...
."
​
Kanisa Katoliki na Askofu uliyelengwa na zawadi hiyo, kama nyie ni watumishi wa Mungu wa kweli, basi, epukeni mtego huo. Rudisheni pesa hiyo. Mtumikieni Mungu wenu kwa haki. Kemeeni na onyeni juu ya UOVU kwa kila mtu. Pesa hiyo ni kifungo kwenu. Fanyeni kama walivyofanya Mtume Petro na Yohana kwa mchawi Simioni...

Rais Samia Suluhu Hassan yupo kwenye "kifungo cha UOVU". Huyu mama anahitaji msaada wa kiroho. Hiyo pesa ni mkakati wa shetani kuwafanya mpotezee, msigundue hila za shetani juu ya mama huyu na hivyo msipate nafasi kuomba kwa ajili yake maana atatumia kigezo cha pesa hizo kupeleka mashitaka kwa Mungu Ili yeye shetani aendelee kuwa na uhalali wa kuendelea kumshikilia huyu mama ktk UOVU wake...

Na kiti cha u - Rais wa nchi kikikaliwa na shetani mwenyewe, maamuzi yote kutoka kwenye kiti hicho yanakuwa ni yale yenye athari hasi pekee kwa nchi na wananchi. Ndiyo haya tunayoyaona sasa....

Petro na Yohana Kwa kusimama katika ukweli wa Neno la Mungu na haki yake, walimuokoa yule mchawi na hukumu Kali ya Mungu. Askofu uliyepewa pesa hizo, fanya likupasalo kufanya sasa...

Suppose kama wangeichukua ile pesa yake, kungetokea nini...?
 
Watu waovu hupenda sana kumkejeli Mungu wakidhani ataulinda UOVU wao...

Tukio la Rais Samia na pesa zake hizo (Milioni 20 akiziita za mafuta ya gari la Askofu) kumpa mtumishi wa Mungu ktk namna ya kutangaza hadharani, watu wasiojua na wenye tamaa ya kijipatia pesa bure waweza kudhani "Rais katoa sadaka..."

Ukweli ni kuwa siyo. Hiyo ni chambo ya mauti ya kiroho kwa Askofu huyo na Kanisa Katoliki Hiyo...

Kilicho nyuma ya pesa hiyo ni hatari. Kama hawajui au wamesahau, wamuulize Askofu wa KKKT Dr Shoo na ile 150,000,000 aliyoitoa huyu mama kwa mkono wa Freeman Mbowe ilivyomtesa kiroho mpaka leo...

Pesa za huyu mama ni hatari. Zina sura zote za hongo na rushwa ya "fungeni midomo" ili kanisa lisionye juu ya UOVU wa huyu Rais na serikali yake unaondelea sasa..

Biblia Neno la Mungu halijaacha kuyasema mambo haya...

Kwamba, hili tukio linafanana na tukio lililorekodiwa ktk Biblia ktk kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya 8 kuwahusu Mtume Petro na Yohana na mchawi mmoja aitwaye Petro aliyetaka kuwahonga Mitume hawa pesa wasigundue UOVU wake...

Bahati njema Petro na Yohana walikuwa na Roho Mtakatifu ndani wa kuwawezesha kutambua hila na mikakati ya roho ya shetani kuharibu kazi ya Mungu...

Haya ndiyo majibu ya Mtume Petro kwa mchawi yule:


Matendo Ya Mitume 8:20-23 SUV

".....Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako. Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu...
."
​
Kanisa Katoliki na Askofu uliyelengwa na zawadi hiyo, kama nyie ni watumishi wa Mungu wa kweli, basi, epukeni mtego huo. Rudisheni pesa hiyo. Mtumikieni Mungu wenu kwa haki. Kemeeni na onyeni juu ya UOVU kwa kila mtu. Pesa hiyo ni kifungo kwenu. Fanyeni kama walivyofanya Mtume Petro na Yohana kwa mchawi Simioni...

Rais Samia Suluhu Hassan yupo kwenye "kifungo cha UOVU". Huyu mama anahitaji msaada wa kiroho. Hiyo pesa ni mkakati wa shetani kuwafanya mpotezee, msigundue hila za shetani juu ya mama huyu na hivyo msipate nafasi kuomba kwa ajili yake maana atatumia kigezo cha pesa hizo kupeleka mashitaka kwa Mungu Ili yeye shetani aendelee kuwa na uhalali wa kuendelea kumshikilia huyu mama ktk UOVU wake...

Petro na Yohana Kwa kusimama katika ukweli wa Neno la Mungu na haki yake, walimuokoa yule mchawi na hukumu Kali ya Mungu. Askofu uliyepewa pesa hizo, fanya likupasalo kufanya sasa...

Suppose kama wangeichukua ile pesa yake, kungetokea nini...?
Amen
 
Back
Top Bottom