Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Ndiyo mwanzo wa watoto kuanza kutangatanga katika malezi, leo anakuwa kwa bibi, kesho kwa uncle, wiki ijayo kwa Mama mdogo

Na hata kama wazazi waliacha Mali, na watoto kusoma English medium school, watarudishwa shule za kayumba
Ndomana unaambiwa siku zote unapopata changamoto za kindoa nk
Tafuta watu sahihi wa kuzungumza nao,wakupe ushauri
Hilo ni kwa pande zote

Ova
 
Kweli kabisa mana kama hapo wameshawapa ugumu watoto kwani mama kafa baba anaenda jela.

Sesten Zakazaka hii ni hatari.
Na sio mama kufa tu!!! Issue ni kuwa amekufaje!!?
Yaani kabisa wamejua baba kamuua mama 😭😭😭😭😭
Trauma ya maisha, na kuja kumsamehe huyo baba sio rahisi hata km aliishi nao kwa mapenzi ya namna gani. Inaumiza mnoooo, it's not easy kwa hao wtt
 
 

Attachments

  • 6411686-f8395ae6769aaed011115d8d0214cf51.mp4
    18.5 MB
Huwa ninatamani sana ninapoona nyumba nzuri ina fence. Kumbe haya ndiyo yanayoendelea huko ndani? Basi acheni tu wazi si bora muwe kama huku kwetu uswahilini kwenye matukio kama haya utasaidiwa na polisi jamii, wanasheria na waandishi wa habari wa mtaa, Nina uhakika hamuwezi fikia kuuwana kabla hujasikia sauti za majirani, "wewe baba naniiii muache utamuua mwenzako kesi hiyo utakuja kwenda jela bure.......! kama vipi mpe talaka yake tu.

Au ukiwa na aibu kama mimi ugomvi ukianza inabidi uwashe bufa ufungulie hadi mwisho na yakikushinda unasepa uaenda zako kijiweni unarudi saa 8 usiku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…