Mume amemtuma mtoto wetu wa miaka mitano dukani usiku ni sahihi?

Hili ndio jibu sahihi Zeemadeit
 
Upumbavu ni wako pamoja na ujinga, wewe ndio sababu ya mtoto kutumwa usiku huo halafu unalalamika hapa, ulikuwa wapi muda wote kuandaa mahitaji yako mapema?
Unasema saa tatu na nusu mtoto huwa kashalala wewe ndio unapika angekula saa ngapi huyo mtoto? Ulikuwa wapi hadi upike saa tatu na nusu? Unaanzisha mgogoro wa kifamilia halafu unaomba ushauri!!!
 

Huwezi kusema kwa ustaarabu unapomkosoa Mama mkwe tena ukiwa umeolewa..

Kama ni mtoto wake kweli sioni sababu ya wewe kukasirika. Lakini kama sio mtoto wake, yaani ni mtoto wako na mwanaume mwingine unahaki na hiyo ndio tafsiri ya ulichoandika
 
Wewe ndiyo mpumbavu, wakati mnabishana ungefunga domo lako ukaenda hapo dukani unaposema siyo mbali ungetatua tatizo.
Mjinga sana wewe unapata muda wa kuandika na kupost humu jf badala ya kwenda dukani.
 
Nafikiri kosa ni lako.
Kwa nini usiandae vitu vyako mapema?
Hii ndiyo shida ya house girl kukuendeshea nyumba.
Ulipaswa kunyanyuka mwenyewe kwenda dukani maana u mzembe
 
Una matatizo
 
Kwa jinsi ulivyoeleza inaonekana mazingira ya nyumbani kwako na dukani ni rafiki ndio maana mumeo akakwambia kuwa aende nae alafu mtoto arudi mwenyewe, ila binafsi mwanangu iwe usiku au mchana siwezi mwagiza dukani kulingana mazingira ninayoishi maduka yapo mbali isitoshe pikipiki ni nyingi sana so kwa kesi yako mazingira halisi mumeo alikuwa anayafahamu ndio mana alifanya ivyo kwa kujua hakuna negative impact yoyote.
 
Kaa kimya hivo hivo acha ujuaji

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hewaa maana asingekuwa mjuaji, mama mkwe ( mama yake kama anavyomkosea adabu) angeshauriana na Zeemadeit siyo kumweleza mtoto direct. Lakini kwa vile ni mbabe na mama wa watu anamuogopa, akaona atumie kitu inaitwa ‘voice of the voiceless’
 
Kingine ambacho ni tatizo kwenye familia nyingi za kiafrika ni kuishi na mama mkwe ndio imekuwa chanzo cha migogoro ya ndoa nyingi sana, kama hakuna ulazima mama mkwe akae uko uko kijijini tu kuliko kuja kuishi mjini kuanza migogoro isiyo na tija yoyote.
 
Story ndefu tulishakula na mtoto kuna muda alianza hadi kusinzia.
 
Hewaa maana asingekuwa mjuaji, mama mkwe ( mama yake kama anavyomkosea adabu) angeshauriana na Zeemadeit siyo kumweleza mtoto direct. Lakini kwa vile ni mbabe na mama wa watu anamuogopa, akaona atumie kitu inaitwa ‘voice of the voiceless’
Naishi nae vizuri changamoto hapo alikuq amerudi kutoka kwenye event flan na qlikua ameshakunywa nadhan hio pia ilichangia yeye kusuggest kitu kama hicho.
 
Ni karibu ila unavuka barabara ya mtaan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…