Mume amemtuma mtoto wetu wa miaka mitano dukani usiku ni sahihi?

Mume amemtuma mtoto wetu wa miaka mitano dukani usiku ni sahihi?

Huwezi kusema kwa ustaarabu unapomkosoa Mama mkwe tena ukiwa umeolewa..

Kama ni mtoto wake kweli sioni sababu ya wewe kukasirika. Lakini kama sio mtoto wake, yaani ni mtoto wako na mwanaume mwingine unahaki na hiyo ndio tafsiri ya ulicho

Kama ni mtoto wake kinachokuuma ni nini kama sio tabia mbaya
Jaman tabia mbaya tena..Kinachoniuma ni mtoto kua exposed kwenye mazingira ya usiku akiwa peke yake...usiku u a mambo mengu na mimi ni yule mama ambae anapenda kuhakikisha mwanae yupo salama kila anapoweza
 
Naishi nae vizuri...hio point ya kusema amenipa kama adhabu na mimi nahisi hivyo...naona kama amejaribu kunionesha nmemkosoa mama mkwe na ma mkwe yupo sahihi
Mimi sidhan kama kuangalia zaidi usalama wa mtoto ni kumkosea heshima na nilisema kwa ustaarab
Kwahiyo wewe unaufahamu Usalama wa mtoto zaidi ya mama mkwe wako?
 
Hajawahi kufanya hivyo ni mara ya kwanza. Ilikua hivi mama yake ambae kwa sasa tupo nae aligundua kuna kitu kimepelea jikoni akamwambia mtoto wetu wa kike (ambae mara nyingi muda huo wa saa tatu na nusu usiku anakua ameshalala kasoro hii leo ) waongozane yeye kuna sehem anaenda mara moja wapitie dukan wanunue hicho kiungo ampe arudi mwenyewe .

Mimi kusikia hivyo nikamwambia sasa hiv usiku na kuna giza huko nje japo duka halipo mbali. Dada wa kazi akimaliza anachofanya au mimi nitaenda kuchukua . Mama mkwe akajibu sawa akaondoka, baada ya kama dakk 5 mume wangu akasema kwann mtoto asiende dukan yeye anamtuma. Nikamwambia sio sawa ni usiku sana mimi nitaenda akalazimisha .

Mtoto akatoka nje alivyofika mbal na eneo la nyumbani akarudi kumuomba baba ake akae nje awe anamuangalia kwa kua anaogopa. Mimi sijapenda hichi kitendo kwa kua hakukua na ulazima wq mtoto kwenda. Je ni sahihi na mimi nina overreact? Ushauri tafadhali ili nijue namna nzuri ya kuhandle hii situation ikitokea tena.
Swali ni kwamba mtoto arirudi ama arikataria ukouko?
 
Kwahiyo wewe unaufahamu Usalama wa mtoto zaidi ya mama mkwe wako?
Ndio nina ufahamu usalama wa mwanangu bila kulinganishwa na mtu yeyote. Na hatulingani katika malezi kuna mwingine yeye kumuacha mtoto kwa jiran siku nzima ni sawa kwake na kuna mimi hapa siwez na wote kuna siku tutakua mama wakwe.
 
Watu tumekujaji kulingana na jinsi ulivyomuita mama mkwe wako. Umeonesha kutomheshimu; hili limetuoatia picha ya namna ulivyomjibu.

Kabla sijaendelea hilo duka liko umbali gani kutoka kwenu?
 
Jaman tabia mbaya tena..Kinachoniuma ni mtoto kua exposed kwenye mazingira ya usiku akiwa peke yake...usiku u a mambo mengu na mimi ni yule mama ambae anapenda kuhakikisha mwanae yupo salama kila anapoweza

Jitahidini muwe kitu kimoja.
Mmoja asimjali mtoto kuliko mwenzake. Mtaivunja hiyo nyumba.

Hapo ungetumia akili tuu kuwa uende naye dukani kwa maana hata wewe kuna kitu unaenda kuchukua.
 
Ume side na huyo popoma wa kike kuonesha dharau kwa huyo mama. Read btwn lines utagundua huyo mwanamke ni tatizo hapo nyumbani
Mmh hakuna issue yeyote kabla ya hapo ingekuwepo ningeizungumzia . Au kisa imeinvolve mama
Jitahidini muwe kitu kimoja.
Mmoja asimjali mtoto kuliko mwenzake. Mtaivunja hiyo nyumba.

Hapo ungetumia akili tuu kuwa uende naye dukani kwa maana hata wewe kuna kitu unaenda kuchukua.
Sawa next time nitaongeza busara kwenye kuhandle haya mambo
 
Watu tumekujaji kulingana na jinsi ulivyomuita mama mkwe wako. Umeonesha kutomheshimu; hili limetuoatia picha ya namna ulivyomjibu.

Kabla sijaendelea hilo duka liko umbali gani kutoka kwenu?
Kusema mama yake mume wangu ni katika kumtambulisha tu ni mama mkwe wangu na namuita MAMA siku zote. Na kuna kipindi nilishaish nae karibu mwaka mzima bila tabu yeyote. Kiufup sina tatizo na mama mkwe wangu ni hii situation tu iliyotokea.

Duka halipo mbal ila unavuka barabara ya mtaan na huku kimara hakuko smooth vilima vilima sana
 
Hajawahi kufanya hivyo ni mara ya kwanza. Ilikua hivi mama yake ambae kwa sasa tupo nae aligundua kuna kitu kimepelea jikoni akamwambia mtoto wetu wa kike (ambae mara nyingi muda huo wa saa tatu na nusu usiku anakua ameshalala kasoro hii leo ) waongozane yeye kuna sehem anaenda mara moja wapitie dukan wanunue hicho kiungo ampe arudi mwenyewe .

Mimi kusikia hivyo nikamwambia sasa hiv usiku na kuna giza huko nje japo duka halipo mbali. Dada wa kazi akimaliza anachofanya au mimi nitaenda kuchukua . Mama mkwe akajibu sawa akaondoka, baada ya kama dakk 5 mume wangu akasema kwann mtoto asiende dukan yeye anamtuma. Nikamwambia sio sawa ni usiku sana mimi nitaenda akalazimisha .

Mtoto akatoka nje alivyofika mbal na eneo la nyumbani akarudi kumuomba baba ake akae nje awe anamuangalia kwa kua anaogopa. Mimi sijapenda hichi kitendo kwa kua hakukua na ulazima wq mtoto kwenda. Je ni sahihi na mimi nina overreact? Ushauri tafadhali ili nijue namna nzuri ya kuhandle hii situation ikitokea tena.
Mambo mengine utadhani ni ''mahoka''. Wewe ni mtu mzima tena mwanamke uliye kwenye ndoa na unashindwa namna ya ku-handle tatizo dogo namna hii?
 
Ni kweli mimi siwezi kua zaidi ya mama yake...wakat nasema nitaenda mimi haikua katika mabishano tulielewana tu kawaida.
Ungeenda mda huo huo...

Japo unajitetea ila unaonekana hauna maelewano na mkwe wako na unamchekea kinafiki tu ila deep down unatamani aondoke kwenu...

Halafu una ule mtazamo wa kumwona mtoto kama wa kwako na sio wa kwenu...

Believe me ukiendelea hivi ndoa yenu itakufa, badilika...

Mama mkwe wako muone kama mama yako...

Mtoto si wako ni wenu.
 
Kwanini yeye hakwenda kununua mpaka amtume mtoto mdogo hivyo tena mtoto mpaka anamwambia baba yake kuwa anaogopa daa inasikitisha sana
Huu ndio ukatili kwa watoto

Nikisema sisi kwa dini na maadili tunakatazwa kabisa kumtoa mtoto nje pindi jua likizama na wote wanakuwa wamerudi ndani
Ila kila mmoja na Imani yake na hapa kuna watakaobeza na kusema mbona kawaida ila akipatwa kitu chochote atalaumiwa mzazi au wazazi kwa kumtoa nje usiku

Utakuta baba alikuwa kwenye simu maana ndio wengi wamerogewa siku hizi
Kweli maisha yamekuwa tofauti sana nowadays
Uko sahihi kabisa. Eti nyumba ina li-baba, li-mama na msichana wa kazi halafu wanatuma mtoto wa miaka 5 usiku dukani kwa sababu ni karibu. Sasa kama ni karibu si ndiyo ingekuwa kichochezi cha hilo-li-baba kwenda? Mbona mimi ni mwanamme na kuna siku nakwenda kununua hata chumvi kwenye mazingira kama haya?
 
Back
Top Bottom