Mume amemtuma mtoto wetu wa miaka mitano dukani usiku ni sahihi?

Jaman tabia mbaya tena..Kinachoniuma ni mtoto kua exposed kwenye mazingira ya usiku akiwa peke yake...usiku u a mambo mengu na mimi ni yule mama ambae anapenda kuhakikisha mwanae yupo salama kila anapoweza
 
Kwahiyo wewe unaufahamu Usalama wa mtoto zaidi ya mama mkwe wako?
 
Swali ni kwamba mtoto arirudi ama arikataria ukouko?
 
Kwahiyo wewe unaufahamu Usalama wa mtoto zaidi ya mama mkwe wako?
Ndio nina ufahamu usalama wa mwanangu bila kulinganishwa na mtu yeyote. Na hatulingani katika malezi kuna mwingine yeye kumuacha mtoto kwa jiran siku nzima ni sawa kwake na kuna mimi hapa siwez na wote kuna siku tutakua mama wakwe.
 
Watu tumekujaji kulingana na jinsi ulivyomuita mama mkwe wako. Umeonesha kutomheshimu; hili limetuoatia picha ya namna ulivyomjibu.

Kabla sijaendelea hilo duka liko umbali gani kutoka kwenu?
 
Jaman tabia mbaya tena..Kinachoniuma ni mtoto kua exposed kwenye mazingira ya usiku akiwa peke yake...usiku u a mambo mengu na mimi ni yule mama ambae anapenda kuhakikisha mwanae yupo salama kila anapoweza

Jitahidini muwe kitu kimoja.
Mmoja asimjali mtoto kuliko mwenzake. Mtaivunja hiyo nyumba.

Hapo ungetumia akili tuu kuwa uende naye dukani kwa maana hata wewe kuna kitu unaenda kuchukua.
 
Ume side na huyo popoma wa kike kuonesha dharau kwa huyo mama. Read btwn lines utagundua huyo mwanamke ni tatizo hapo nyumbani
Mmh hakuna issue yeyote kabla ya hapo ingekuwepo ningeizungumzia . Au kisa imeinvolve mama
Jitahidini muwe kitu kimoja.
Mmoja asimjali mtoto kuliko mwenzake. Mtaivunja hiyo nyumba.

Hapo ungetumia akili tuu kuwa uende naye dukani kwa maana hata wewe kuna kitu unaenda kuchukua.
Sawa next time nitaongeza busara kwenye kuhandle haya mambo
 
Watu tumekujaji kulingana na jinsi ulivyomuita mama mkwe wako. Umeonesha kutomheshimu; hili limetuoatia picha ya namna ulivyomjibu.

Kabla sijaendelea hilo duka liko umbali gani kutoka kwenu?
Kusema mama yake mume wangu ni katika kumtambulisha tu ni mama mkwe wangu na namuita MAMA siku zote. Na kuna kipindi nilishaish nae karibu mwaka mzima bila tabu yeyote. Kiufup sina tatizo na mama mkwe wangu ni hii situation tu iliyotokea.

Duka halipo mbal ila unavuka barabara ya mtaan na huku kimara hakuko smooth vilima vilima sana
 
Mambo mengine utadhani ni ''mahoka''. Wewe ni mtu mzima tena mwanamke uliye kwenye ndoa na unashindwa namna ya ku-handle tatizo dogo namna hii?
 
Ni kweli mimi siwezi kua zaidi ya mama yake...wakat nasema nitaenda mimi haikua katika mabishano tulielewana tu kawaida.
Ungeenda mda huo huo...

Japo unajitetea ila unaonekana hauna maelewano na mkwe wako na unamchekea kinafiki tu ila deep down unatamani aondoke kwenu...

Halafu una ule mtazamo wa kumwona mtoto kama wa kwako na sio wa kwenu...

Believe me ukiendelea hivi ndoa yenu itakufa, badilika...

Mama mkwe wako muone kama mama yako...

Mtoto si wako ni wenu.
 
Uko sahihi kabisa. Eti nyumba ina li-baba, li-mama na msichana wa kazi halafu wanatuma mtoto wa miaka 5 usiku dukani kwa sababu ni karibu. Sasa kama ni karibu si ndiyo ingekuwa kichochezi cha hilo-li-baba kwenda? Mbona mimi ni mwanamme na kuna siku nakwenda kununua hata chumvi kwenye mazingira kama haya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…