Mume amfikisha mahakamani mkewe kwa kupeleka mshahara wake kanisani

Mume amfikisha mahakamani mkewe kwa kupeleka mshahara wake kanisani

Naona wengi hamuelewi hizi concepts, Mwanamke hapaswi kuchangia pato ndani ya nyumba kama ni mama wa nyumbani kwa kuwa nguvu zake, muda na maarifa yake anayatumia kutunza familia au mume kama hawana mtoto. Ila akishaenda kazini ina maana ule muda wake ambao angefanya kazi za nyumbani anautumia kazini na hivyo pengine mnalazimika kumlipa mtumishi wa ndani then huyu mama apate mapato kwa kumwacha akafanye kazi na asiwe na muda wa kuiangalia familia then mseme mshahara wake usitumike nyumbani!!? Hell No. Huo utakuwa ni wizi. Kwamba achangie kiasi gani hapo ndipo kunaweza kuwa na mjadala...Hata akichangia 20% au 10% sawa ila kama anafanya kazi lazima achangie. Kwasababu mume umempa muda wa kwenda kushinda kazini badala ya kushinda nyumbani kuiangalia familia.
 
Sasa hapo haki sawa ipo wapi, kwenye kupata maslahi kama kazi na ajira mnataka haki sawa lakini linapokuja kwenye majukumu hamtaki kuchangia sasa hizo kazi mnataka za nini?
Na ndio nimemchana huyo jamaa kuwa ni mzigo hata kwenye eneo lake la kazi. Hana faida. Chunga mno unachoongea, na angejua angekaa kimya afiche uzwazwa wake.
 
Unageuka CIA wapelelezi kila kona kama humuamini mke

Kama humuamini ulimuoa wa nini

Hadi umuwekee wapelelezi kila kona akikuwekea wewe utanusurika?
Mke asiyefuata maelekezo ya Mumewe huyo ni Mwanamke Changu tu,Kama kampenda sana Mchungaji wake si akaishi nae tu!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza ni kujidhalilisha kwendà mahakamani kisa umenyimwa K unachotakiwa kufanya ukinyimwa tafuta sababu kwanini unyimwe na wakati kuna kipindi alikuwa anaichukua mwenyewe na kuielekeza kunako tena kwa mashamsham?
Mbona Kuna wakati alikuwa akikumis hadi anakupigia simu kwamba uwahi kurudi ukampe muhogo wake wa jang'ombe?

Mwanamke akinkunyima kuna mahala hapaja kaa sawa na hapo jambo hilo humalizwa kwa mazungumzo siyo kwenda mahakamani kwani hakimu hata polisi hawana ubavu wa kumlazimisha mwanamke akupe tamu yake kwani masuala ya faragha ni hiari ya mtu vinginevyo utakuwa ubakaji ulawiti etc.
Uko sahihi kabisa
 
yani inakuaje askari magereza na mwalimu wote mkawa vichaa huyu anapeleka pesa zote kanisani mwingine anataka kusaize ATM card ya mwenzake
 
Wacha litemwe sasa iki likaolewe na huyo mchungaji! Walokole wanakuwa brain washed sana na hawa mitume na manabii! Hawajielewi tu!
Ukiwakuta wanaotoka kwa kuhani musa saa saba usiku hadi huruma
 
Mama abakie hapo hapo.
Anaitaka ATM aisee

Mwanamke kweli umkabidhi mume ATM? That is too much

Wanawake vizuri kuomba Mungu kutopata kidume kilofa kama hicho hopeless kabisa kiofisa magereza

Kinadhalilisha jeshi la magereza wanawake wenye kazi zao watakatakaa kuolewa na Askari magereza kuwa watawapokonya ATM
Kuna mdogo wa rafiki yangu, yeye alikua askari polisi, kitengo cha usalama barabarani, Rwangwa mkoani Lindi.

Huyu mwamba alimsomesha chuo cha ualimu mkewe. Baada ya kuajiriwa, jamaa akataka kumpima mkewe, kama atakua na mabadiko baada ya kuwa na ajira yake.
Alichofanya mshahara wa kwanza, akamwambia nipe pesa zote, akaenda kuzipiga pombe. mshara wa pili na watatu, ila mke hakua na neno.

Baada pale jamaa akamwachia pesa zake apange matumizi yake, Mwenyewe.
 
Jamani msicheke na wanawake ndoa nyingi zimevunjika kwa wanaume kutowafuatilia wanawake,mimi mke wangu anafanya kazi kila mwezi nahitaji (Lazima)anipe orodha ya matumizi ya mshahara wake kuna wakati ananunua viatu pear 3 kwa wakati mmoja ndani kuna pear zaid ya 40 ujinga huu siuruhusu hapo ni ban ya kununua viatu miezi 3,kuna wakati kwa makusudi akiniambia sukari imekwisha namwambia kanunue na pesa yako na nikute mfuko upo ndani ni amri sio ombi.mshahara wa house girl ni jukumu lake na ninachotaka kujua kalipwa ni lazima sio ombi ,na nimemwambia kama hataki nifuatilie matumizi ya mshahara wake akae nyumbani hakuna tatizo .
 
Mwalimu wa shule ya Sekondari Jijini Mbeya, Julieth Kabuja (32) ameieleza Mahakama ya mwanzo Mkoani hapo kuwa ni bora ndoa yake ivunjike kuliko kumkabidhi mumewe kadi yake ya benki.

Ameyazungumza hayo mbele ya Mahakama ya mwanzo jijini hapo baada ya mumewe Charles Meshack (31) kufungua shauri la madai ya talaka akitaka kuachana na mkewe kwa kuhama dhehebu la katoliki na kuhamia la kilokole.

Aidha Meshack ambaye ni Askari Magereza amedai mkewe baada ya kuhamia katika ulokole fedha zake amekuwa akizipeleka kanisani kitendo kinachosababisha yeye kuzidiwa na majukumu ya familia.

“Naumia sana na majukumu, kodi ya nyumba nilipe mimi, ada za Watoto na chakula vyote mimi, halafu yeye mshahara wake apeleke kanisani, bora tuachane” alisema Meshack.
Hata hivyo Julieth aliiambia Mahakama kuwa yeye na mume wake wote ni wafanyakazi, lakini anashangaa anataka kumiliki kadi zote.

“Siku moja aliniamsha usiku na kuniambia nisipokubali kumkabidhi kadi yangu ya benki bora tuachane kwa kisingizio yeye alinilipia mahari hivyo mimi na kila kitu changu kipo chini yake, yaani kazi nifanye mimi halafu mshahara nimuachie huyu bwana, nipo tayari kuachika lakini siyo kuacha kadi yangu” alidai Julieth

Baada ya Hakimu Hafsa Shelimo kusikiliza pande zote mbili, aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 12, mwaka huu kwaajili ya hukumu.

Chanzo: Swahili Times
Mwanamke akishajiunga na makanisa ya kilokole anakua gaidi.
 
Back
Top Bottom