Mume amfikisha mahakamani mkewe kwa kupeleka mshahara wake kanisani

Naona wengi hamuelewi hizi concepts, Mwanamke hapaswi kuchangia pato ndani ya nyumba kama ni mama wa nyumbani kwa kuwa nguvu zake, muda na maarifa yake anayatumia kutunza familia au mume kama hawana mtoto. Ila akishaenda kazini ina maana ule muda wake ambao angefanya kazi za nyumbani anautumia kazini na hivyo pengine mnalazimika kumlipa mtumishi wa ndani then huyu mama apate mapato kwa kumwacha akafanye kazi na asiwe na muda wa kuiangalia familia then mseme mshahara wake usitumike nyumbani!!? Hell No. Huo utakuwa ni wizi. Kwamba achangie kiasi gani hapo ndipo kunaweza kuwa na mjadala...Hata akichangia 20% au 10% sawa ila kama anafanya kazi lazima achangie. Kwasababu mume umempa muda wa kwenda kushinda kazini badala ya kushinda nyumbani kuiangalia familia.
 
Sasa hapo haki sawa ipo wapi, kwenye kupata maslahi kama kazi na ajira mnataka haki sawa lakini linapokuja kwenye majukumu hamtaki kuchangia sasa hizo kazi mnataka za nini?
Na ndio nimemchana huyo jamaa kuwa ni mzigo hata kwenye eneo lake la kazi. Hana faida. Chunga mno unachoongea, na angejua angekaa kimya afiche uzwazwa wake.
 
Unageuka CIA wapelelezi kila kona kama humuamini mke

Kama humuamini ulimuoa wa nini

Hadi umuwekee wapelelezi kila kona akikuwekea wewe utanusurika?
Mke asiyefuata maelekezo ya Mumewe huyo ni Mwanamke Changu tu,Kama kampenda sana Mchungaji wake si akaishi nae tu!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Uko sahihi kabisa
 
yani inakuaje askari magereza na mwalimu wote mkawa vichaa huyu anapeleka pesa zote kanisani mwingine anataka kusaize ATM card ya mwenzake
 
Kila mtu anachagua kilicho bora kwake 😀😀😀
Wacha litemwe sasa iki likaolewe na huyo mchungaji! Walokole wanakuwa brain washed sana na hawa mitume na manabii! Hawajielewi tu!
 
Wacha litemwe sasa iki likaolewe na huyo mchungaji! Walokole wanakuwa brain washed sana na hawa mitume na manabii! Hawajielewi tu!
Ukiwakuta wanaotoka kwa kuhani musa saa saba usiku hadi huruma
 
Kuna mdogo wa rafiki yangu, yeye alikua askari polisi, kitengo cha usalama barabarani, Rwangwa mkoani Lindi.

Huyu mwamba alimsomesha chuo cha ualimu mkewe. Baada ya kuajiriwa, jamaa akataka kumpima mkewe, kama atakua na mabadiko baada ya kuwa na ajira yake.
Alichofanya mshahara wa kwanza, akamwambia nipe pesa zote, akaenda kuzipiga pombe. mshara wa pili na watatu, ila mke hakua na neno.

Baada pale jamaa akamwachia pesa zake apange matumizi yake, Mwenyewe.
 
Jamani msicheke na wanawake ndoa nyingi zimevunjika kwa wanaume kutowafuatilia wanawake,mimi mke wangu anafanya kazi kila mwezi nahitaji (Lazima)anipe orodha ya matumizi ya mshahara wake kuna wakati ananunua viatu pear 3 kwa wakati mmoja ndani kuna pear zaid ya 40 ujinga huu siuruhusu hapo ni ban ya kununua viatu miezi 3,kuna wakati kwa makusudi akiniambia sukari imekwisha namwambia kanunue na pesa yako na nikute mfuko upo ndani ni amri sio ombi.mshahara wa house girl ni jukumu lake na ninachotaka kujua kalipwa ni lazima sio ombi ,na nimemwambia kama hataki nifuatilie matumizi ya mshahara wake akae nyumbani hakuna tatizo .
 
Mwanamke akishajiunga na makanisa ya kilokole anakua gaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…