Mume amfikisha mahakamani mkewe kwa kupeleka mshahara wake kanisani


Wewe utakuwa ni single mama bila shaka!! Naona machozi ya uchungu wa kuzalishwa na kutupwa hapo nyumbani kwenu,unakutesa sana,nikukumbushe majukumu ya kutunza familia ni ya wazazi wote,sio ya mwanaume au mwanamke tu,mnapoingia kwenye jukumu la kuanzisha familia,mjue mmeanzisha kampuni,mkifanikiwa sifa ni za kwenu wote,mkifeli lawama ni za kwenu wote,binafsi yangu siwezi kuishi na mwanamke ambae sijui kipato chake kinatumika vipi,hata kama sina mpango na pesa yake. Lakini ni vizuri nijue kwa faida ya wetu,kama mke anapeleka pesa zote kwa wahuni wa makanisani,siku nikiwa sipo duniani si atauuza rasilimali zote za watoto apeleke uko kwa wahuni wenzake na watoto wageuke panya road!! Ukichunguza panya road wengi wanalelewa na mzazi mmoja wa kike. Kama wanawake wanataka usawa na wanaume wa hamsini kwa hamsini basi waelewe hata majukumu watayabeba.
 
Yaani logic ya jamaa ni hii. MWANAMKE HATAKI KUSAIDIA MAJUKUMU YA NYUMBANI AMBAPO KUNA MUME WAKE NA WATOTO WAKE WA KUZAA MWENYEWE LAKINI ANAAMUA NA KUONA BORA KWENDA KUPELEKA MSHAHARA WOTE KANISANI KWA MCHUNGAJI.


Huu ni ujinga uliopitiliza. Huyo mwanamke na wanawake wengine pamoja na wanaume wengine mnaomuona jamaa ni mjinga nyie ndyo wajinga grade one! Yaani wewe mwanamke unaona haifai kumsaidia mume wako majukumu ambayo ni pamoja na kuwahudumia watoto wako lakini unapeleka pesa hiyo hiyo kwa mwanaume mwingine aliyejivisha vazi la uchungaji! STUPIDITY!!!!


Pia hilo suala la kusema mwanaume ameng'ang'ania kadi ya mwanamke ni uongo! Wanawake ni wajanja sana, wanajua kucheza na huruma ya jamii. Mwanamke anaweza kufanya tukio hadi shetani mwenyewe akakaa chini kujifunza.

Kwa upumbavu wa huyo mwanamke, vunja ndoa brother ili yeye akaolewe na MCHUNGAJI huyo ambae hana busara za kujenga ndoa za kondoo zake bali anaziharibu. Au aende akaolewe na mwanaume ambae ataruhusu mwanamke wake afanye kazi mwezi mzima halafu mshahara ukitoka anapeleka wote kanisani kwa mwanaume mwingine. Stupid!!!!
 
Bora waachane harafu mwanamke aendelee kupeleka mshahara wake kanisani...
Nakuhakikishia wakishaachana huyo mwanamke hatopeleka tena mshahara wake wote KANISANI kwasababu atakuwa na majukumu ya kuhakikisha anakula, analipa kodi ya nyumba, anavaa, anasafiri na matumizi mengine. Kwasasa anajifanya kichaa wa kupeleka mshahara wote kanisani kwasababu kuna mtu anamlisha, anamvalisha, analala bure na kila kitu anakikuta kipo nyumbani.
 
Yes ,ajue nini maana ya matumizi bora ya pesa...
 
word!
 
Nakazia hapa brother asante umemaliza hakuna la nyongeza hapa atakae elewa na aelewe!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo kubwa si kuhama tu dhehebu bali namna mwanamke anavyotoa hela yote kwa mchungaji badala ya kufanya angalau matumizi ya kifamilia
Kutoa sadaka ni kumpa mchungaji?

Sadaka hutolewa kanisani kwenye vyombo vya sadaka umkabidhi mchungaji mkononi. Na Ukiweka kwenye chombo huwa hazina majina ya aliyeweka

Kanisa ndio hupokea sadaka

Huyo mwanaume akiulizwa ushahidi kuwa adhibitishe kuwa hizo pesa huwa huyo.mwanamke anampa mchungaji hatakuwa nao
 
Kanisa linazipeleka wapi hizo sadaka?
 
Zamani nilikuwa napenda sana kuangalia movies za Kinaigeria.
Mara nyigi zilikuwa zinaonyesha mambo ya kilokole na miujiza-miujiza!
Zilikuwa zinaonyesha kwamba mabingwa wote wa miujiza walikuwa wanapata ujuzi huo kwa waganga maarufu wa ndumba!!
Inaelekea kuna ukweli ndani yake!!
 
Yaani wanawake wanaohama madhehebu yao kwenda kwenye ulokole, wanakuwaga kama wamepagawa hivi, hawasikii la mume, ndugu, wala wazazi, sijui wanalishwaga nini!!?
 
Yaani wanawake wanaohama madhehebu yao kwenda kwenye ulokole, wanakuwaga kama wamepagawa hivi, hawasikii la mume, ndugu, wala wazazi, sijui wanalishwaga nini!!?
Sababu matatizo yao wanakuwa wameongea na mume na ndugu na wazazi hakuna anayesikia

Sasa inakuwa zamu yao kutosikilizwa.Inaitwa usimuamshe aliyelala akiamka utalala wewe
 
Ok, mke anapokea mshahara na wote haujukikani unaenda wapi. Unaweza kusaidia hapo?
 
Ni aibu dume Zima kung'ang'ania fedha za mkeo. Sio kazi yake kuhudumia familia. Kidume ng'ang'ana !!! Akikunyima chini ya kitovu hapo nenda mahakamani... Lakini sio kadi yake ya benki.!!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Huu ni ujinga wa feminists. Lengo la ajenda ya mume kumuhudumia mke kwa kila kitu, lilikuwa zuri. Ila utekelezaji wake sasa. Haiwezekani mume umuhudumie mke kwa kila kitu wakati wote mnaondoka asubuhi na kurudi usiku. Hapo bado mshahara wa dada wa kazi utoe wewe (mume). Pesa yake ina kazi gani iwapo hata kumuhudumia yeye mwenyewe haiwezi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…