Katika muunganiko wowote hasa NDOA, jambo la kwanza la kuangalia ni upendo, upendo ukizidi yote mambo mengine ni rahisi ku deal nayo. Binafsi mke wangu ni mtumishi, ila kati ya vitu ambavyo hatuna tatizo kabisa ni suala la pesa, tunafanya kwa kushirikiana sana na ikitokea atoe fedha zake basi ananipa mimi ndio nampa. Hakuna mtu kati yetu mwenye uroho wa kutumia pesa zetu. Atm card zetu za mishahara zipo hapo tu na password wote tunazijua( ingawa nina account zingine za DEV). Hivyo, kama mwanamme, pamoja na kumzidi mshahara lazima nifanye kazi ya ziada kupata pesa nyingi zaidi na hii inasaidia sana, maana ni mara chache kutumia fedha zake ingawa tupo huru sana. Shemeji yenu anampenda Mwamposa sana ila nilimpiga beat, amebaki kumtazama kwenye tv tu, nilimwondoa kabisa na wachungaji wa kilokole maana walianza mazoea sana mpk magroup ya whatsap. Kama wanaume tunapaswa kutumza ndoa zetu, wanawake huwa wanakosa imani hasa akigundua fedha mnazotunza ndizo unahonga michepuko, au kugawa hovyo hovyo, tujitahidi kuwa vyanzo vya ziada vya mapato ili kuwa na backups ambazo mwanamke hajui, mwisho kuishi na mtoto wa mtu ni MTEGO.