Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Tatizo liko hv dini ndo zilizowaaminisha, watu kwa 99%, kwamba kuna mungu na yuko hv na anataka tuishi hv alafu sasa tena zilezile dini zinapingana mwenyewe kwa mwenyewe kuhusu huyu mungu, mpaka wanashikiana bunduki na kumwanga damu kumdai mungu huyu, ?
 
Unaweza kuthibitisha hili? au umeamua kuamini tu na hauwezi kuthibitisha?
Nathibitisha kwamba ulimwengu upo unaonekana hata wewe upo ndani yake.

Na kama ulimwengu upo ina maana kwamba ulikuwepo, ndio maana wewe umeweza kuwepo ndani yake.

Ulimwengu usingekuwepo, Hata wewe usingeweza kuwepo ndani yake.
 
Sawasawa..., Kwahiyo nikikuta Kikombe kwenye Kabati itakua sahihi nikisema Kikombe hicho kilikuepo kwenye kabati milele na milele, Kwakua tu nakiona kikombe hicho kwenye kabati..?

Inabidi uthibitishe hiyo kauli kwamba ulimwengu "ulikuepo tu"....

NB:- The existence of something at present does not prove its entire history.
 
Sawasawa..., Kwahiyo nikikuta Kikombe kwenye Kabati itakua sahihi nikisema Kikombe hicho kilikuepo kwenye kabati milele na milele, Kwakua tu nakiona kikombe hicho kwenye kabati..?
Uwepo wa kikombe kwenye kabati ni uthibitisho kwamba kabati lipo na lilikuwepo kabla ya uwepo wa kikombe kwenye kabati.

Vivyohivyo na binadamu, tupo na tulikuwepo ulimwenguni kwa vile ulimwengu ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo.

Kama ulimwengu usingekuwepo, Sisi binadamu tusingeweza kuwepo kwenye ulimwenguni ambao ulikuwepo na ambao mpaka sasa upo.

Ulimwengu ulikuwepo ndio maana sisi binadamu tumeweza kuwepo kwenye ulimwengu ambao tayari ulikuwepo.
Inabidi uthibitishe hiyo kauli kwamba ulimwengu "ulikuepo tu"....

NB:- The existence of something at present does not prove its entire history.
Na wewe kama unakataa ulimwengu haukuwepo, inabidi uthibitishe ni wakati gani ulimwengu haukuwepo kisha ukawepo.

Kama huwezi ni uthibitisho tosha kwamba ulimwengu ulikuwepo tu na hakuna wakati ambao ulimwengu haukuwepo.
 
Uwepo wa kikombe kwenye kabati ni uthibitisho kwamba kabati lipo na lilikuwepo kabla ya uwepo wa kikombe kwenye kabati.
Hujathibitisha kwamba kabati lilikuepo milele,...bali umethibitisha Kabati lilikuepo kabla ya uwepo wa kikombe....

Sizungumzii kipi kilikuepo kabla ya kingine bali nazungumzia uwepo wa vitu vyote kwa pamoja...
Yaani kimsingi thibitisha hoja yako kwamba, "DUNIA HAIJAWAHI KUTOKUWEPO"

Na wewe kama unakataa ulimwengu haukuwepo, inabidi uthibitishe ni wakati gani ulimwengu haukuwepo kisha ukawepo.

Kama huwezi ni uthibitisho tosha kwamba ulimwengu ulikuwepo tu na hakuna wakati ambao ulimwengu haukuwepo.

Hapana mimi sikatai,..Nataka uthibitishe tu kwamba ulimwengu haujawahi kutokuepo., ili nipate uhakika na nijifunze kutoka kwako.
 
Hujathibitisha kwamba kabati lilikuepo milele,...bali umethibitisha Kabati lilikuepo kabla ya uwepo wa kikombe....

Sizungumzii kipi kilikuepo kabla ya kingine bali nazungumzia uwepo wa vitu vyote kwa pamoja...
Yaani kimsingi thibitisha hoja yako kwamba, "DUNIA HAIJAWAHI KUTOKUWEPO"

Hapana mimi sikatai,..Nataka uthibitishe tu kwamba ulimwengu haujawahi kutokuepo., ili nipate uhakika na nijifunze kutoka kwako.
Dunia haijawahi kutokuwepo kwa sababu hakuna uthibitisho wowote ule unao onyesha kwamba Dunia haikuwepo kisha ikawepo.

Yani hakuna wakati wowote ule ambao imethibitishika kwamba Dunia haikuwepo kisha ikawepo.

Kila mtu amezaliwa ndani ya dunia na kuikuta tayari ipo.

Hakuna binadamu aliyezaliwa nje ya dunia halafu akaona dunia ikiumbwa.
 
Dunia haijawahi kutokuwepo kwa sababu hakuna uthibitisho wowote ule unao onyesha kwamba Dunia haikuwepo kisha ikawepo.
Sawasawa,...Kwahiyo unathibitisha Dunia haijawahi kutokuepo..., Kwasababu tu huwezi kuthibitisha kwamba haijawahi kuwepo kisha ikawepo?

Kwamba Ukikuta Nyumba imejengwa sehemu fulani,..kisha ukasikia habari kwamba hiyo Nyumba kuna kipindi haikuepo,. then Wewe na hao wanaokuambia habari hiyo wakashindwa kuthibitisha kwamba kuna kipindi hiyo Nyumba haikuepo,....Wewe utaamua kuhitimisha kwa kujithibitishia mwenyewe kwamba hiyo Nyumba haikuwahi kutokuwepo, yaani ilikuepo hapo milele, kwa kuwa tu huwezi kuthibitisha kwamba kuna kipindi Nyumba hiyo haikuepo??
 
Kila binadamu amezaliwa ndani ya ulimwengu. Kwa maana hiyo kila binadamu amekuta ulimwengu upo.

Hakuna anayejua kwamba ulimwengu uliumbwa ilihali kila mtu kazaliwa kwenye ulimwengu huohuo ambao kaukuta upo.

Hivyo ulimwengu ulikuwepo.
 
Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini
Kabla ya zama za leo watu wapikuwa wanaishi kwenye mapango je mfano wa kwanza wa nyumba waliupata wapi??!

Ndio maana ya kufikiri na kuamua kitu vile unavyotaka kiwe, na hii na hata kwako ukitaka kitu unaweza kubuni bila kupata mwongozo wowote ule ukaamua kuja na ubunifu wako

Ndio maana Mungu aliumba vitu kwa hatua alianza kwa kutenganisha maji na nchi kavu, kisha na vitu vyote vya asili uvionavyo ndani ya siku sita kisha baadae ndio akamuumba binadamu

Ni uamuzi tu
 
Hakuna anayejua kwamba ulimwengu uliumbwa ilihali kila mtu kazaliwa kwenye ulimwengu huohuo ambao kaukuta upo.

Hivyo ulimwengu ulikuwepo.
Kwahiyo Binadamu kuukuta ulimwengu ndiyo uthibitisho kwamba Dunia ilikuepo milele?

Yaani ukizaliwa na kumkukuta Babu yako,. Inatosha kuthibitisha kwamba Babu yako alikuepo milele,kwa kuwa tu umemkuta?

Yaani kwamba kutokujua (ujinga) historia ya kitu ndiyo watu wote tuchukulie kama uthibitisho?
 
Ni uthibitisho ndio unless otherwise uje na uthibitisho wako unao onyesha kwamba ulimwengu uliumbwa.
 
Ni uthibitisho ndio unless otherwise uje na uthibitisho wako unao onyesha kwamba ulimwengu uliumbwa.
Ni uthibitisho wa nini?........Mimi sijasema kama Dunia iliumbwa nataka uthibitisho tu toka kwako kwamba Dunia ilikuepo milele kama ulivyodai.

Kama haiwezekani kuleta uthibitisho,... utuambie ni assumptions tu umefanya huna uhakika wala uthibitisho wowote.
 
Unaposema MUNGU aliona wapi mfano wa dunia ndipo akaumba, hivi unamfananisha BWANA MUNGU na Mwanadamu?

Umekosa akili, umekosa adabu kwa MUUMBA wako kiasi unaona hawezi kufanya chochote mpaka kwanza awe ameona?

Na kama mpaka aone kwanza, unataka kusema yupo mwingine aliye mkuu kumzidi YEYE?

Kijana kuwa na adabu kwa MUUMBA wako. Usifikie hatua ya kumdharau MUNGU kuwa hawezi kutenda, hawezi kuumba mpaka awe ameona kwanza.
Turudi katika perspective ya religion scriptures.

"Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na ardhi."

At the same time, vitabu vinadai Mungu ni wa milele yani yupo siku zote hata kabla ya huo uumbaji.

Lakini Vitabu havijaeleza Mungu alikuwa eneo lipi wakati akifanya huo uumbaji.

Na hilo eneo liliumbwa na nani?

Na kama hilo eneo liliumbwa, je ni sahihi kusema mbingu na ardhi ndio uumbaji wa mwanzo?

Unaweza kutusaidia majibu ya hayo maswali?
 
Sasa kama mwanadamu anaweza akajenga nyumba kwa kubuni na kuchora ramani vipi kuhusu Mungu?
Kila kitu alikibuni na kukifanya!
 
Ndiyo maana anaitwa MUNGU ni cheo Cha ngazi ya juu kuliko vyote kwenye muundo wa maisha na uhai kabla na baada ya maisha haya.

Uwezo wa fikra zetu na utambuzi haviwezi kueleza bayana kuhusu sifa, uwezo na hali ya MUNGU.

Kumjua MUNGU linabaki fumbo asilia linalohitaji mlango wa Imani pekee Ili uwezakano huo uwepo.

Yeyote anayetumia ishara bayana kutaka kumjua MUNGU hataweza kwa maana MUNGU hayupo katika ulimwengu wa macho haya bali kiroho.

Tunapaswa kujali matokeo Bora ya MUNGU wetu katika maisha yetu kuliko kumpima uwezo wake ambao kamwe hauwezi kubainika kwa akili zetu finyu
🙏🙏🙏🙏🙏
Mi sikuzote nilidhani watu wanaanza kuamini kitu baada ya kukielewa.

Sasa kama fikra zetu na utambuzi haviwezi kumuelewa Mungu, ni ipi sababu ya sisi kumuamini?

Vipi akija mtu wa dini tofauti na yako unaweza kushawishika na aina hii ya utetezi kuonesha Mungu wake ni wa kweli kuliko wako?

Au tuseme.

Linapokuja swala la uongo ambao umepakwa rangi uonekane ni ukweli katika namna ya kukuficha ili urubunike ushindwe kuelewa uongo wake.

Na wakati huo zile njia kuu kama logical reasoning, za kutambua ukweli zimekuwa sealed

Utatumia procedure gani ili usimame katika mstari sahihi?
 
Ni uthibitisho wa nini?........Mimi sijasema kama Dunia iliumbwa nataka uthibitisho tu toka kwako kwamba Dunia ilikuepo milele kama ulivyodai.

Kama haiwezekani kuleta uthibitisho,... utuambie ni assumptions tu umefanya huna uhakika wala uthibitisho wowote.
Nilishakwambia hakuna binadamu yeyote yule anayejua ulimwengu ulianzaje.

Dunia ipo milele kwa sababu hakuna wakati wowote ule ambapo dunia haikuwepo.

Dunia ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo.
 
HIvi unajua maana ya swali kuwa specific ?

Kumbe nikupe mfano wa pili : Tanzania ni nchi ya ulimwengu wa tatu, nataka kujua kwanini tanzani ni masikini.

Wewe unakuja kwanza kukanusha kuwa tanzania siyo nchi ya ulimwengu wa tatu, hapa swali lazima kwanza lijibiwe na watu walio na mtazamo kuwa tanzania ni nchi ya ulimwengu wa tatu ndiyo watatoa sababu za kwanini ni maskini.

Ila wewe ambae hujakubali kuwa tanzani iko kundi la nchi za ulimwengu wa tatu huwezi kujibu swali hili maana utakosa sifa za kujibu.
Hata wewe mwenyewe haupo specific.

Unapotaja neno Mungu ni neno ambalo lina maana nyingi zenye kutofautiana.

Katika historia za dini kuna Miungu wengi wanaohusishwa na uumbaji wa mbingu na ardhi, ulitakiwa uwe specific unakusudia Mungu gani.

Lakini pia kuhusu aina ya jibu ulilopewa naona ni sahihi.

Unayeuliza swali kwa muktadha wa hadithi na yule pia anayetoa maoni yake kwa muktadha wa uhalisia wote mpo sahihi.

Japo wewe focus yako inelenga kupewa majibu kwa mujibu wa simulizi za hiyo hadithi.

Kwasababu gani nasema mdau yupo sahihi?

Ni kwasababu licha ya kwamba swali lililoulizwa limetokana kwenye hadithi za kufikirika lakini bado lipo kundi la watu linaloitazama hiyo hadithi kama ni habari za kweli zenye uhalisia.

Mfano unaweza ukauliza swali kuhusu kujua ni panya wa jamii gani aliye host kikao chini ya mti kujadili namna ya kumvisha paka kengele.

Watu wakajitokeza kusema panya mabaka wengine panya majivu, lakini kumbe kati ya hao watu waliotoa hayo majibu wana amini hizo stori kuwa ni za kweli.

Sasa kwakua hii ni platform huru ambayo pia inatoa elimu ni busara kwa hilo kundi la watu nao waweze kuufahamu ukweli.
 
Nilishakwambia hakuna binadamu yeyote yule anayejua ulimwengu ulianzaje.

Dunia ipo milele kwa sababu hakuna wakati wowote ule ambapo dunia haikuwepo.

Dunia ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo.
Nilishakuambia hayo ni maneno tu na si uthibitisho.

Ukipata uthibitisho lete.
 
Kwani mtu wa kwanza kabisa kujenga Nyumba,alitoa wapi ramani au mfano wa Nyumba? Aliyetengeneza Gari,Meli,Ndege,Simu,Viatu,Saa,Tv....nae alitoa wapi ramani au mfano wa hivyo vitu?

Ukipata majibu ya hayo maswali yangu utakua umepata jibu la swali lako.
Two different scenarios

Mfumo wa maisha ya mtu upo katika vipindi vya evolution.

Nyumba ni sehemu ya utunzi wa mtu alioweza kuupata kupitia nature.

Mapango na misitu minene ambayo ilikuwa sehemu salama kwa watu wa kale kuweza kujilinda na wanyama wakali.

Karne za baadaye kusogea ikaja kubadilika kuwa makazi sio tu sehemu ya kujificha dhidi ya wanyama bali ni sehemu ambayo unaweza ku settle familia yako.

Sasa mfano huu hauwezi ku apply kwa Mungu ambaye kwa mujibu wa vitabu yeye ndio kaumba nature.

Sasa swali hilo linabaki kwake ilikuwaje?
 
Back
Top Bottom