Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Wewe Ni dhehebu gani mpaka useme Yesu sio Mungu?. Msingi wa Ukristo Ni utatu Mtakatifu. Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu. Kama huamini hilo wewe utakuwa sio mkristo Bali dini nyingine au cult.
Ni wapi Haya Mkuu umeyatoa. Kwamba Mungu ana Wingi!
 
Wewe ndio usome historia vizuri. Acha propaganda za uongo. Watu gani waliuawa, wakati wa missionary walijenga shule na mahospitali ambayo mpaka leo zinatumika. Halafu ukristo msingi wake Ni hiari sio lazima.
Soma Historia ya mapigano ya Wakristo ndugu yangu (crusade) au Alama Inayotumiaka ya P na X. Tumia akili Timamu hizo shule walisoma Watoto wa machifu kipindi cha Ukoloni wakati Babu zako ni watumwa.
images%20(1).jpg
 
Kuna Mambo Yapo Ulimwenguni ukiyatafakari kwa Kina hayaingii Akilini ndugu waafrika wenzangu

Kuna Historia katika Vitabu kwamba Mungu alimtoa Mwanae Ili aje Kuikomboa Dunia katika Dhambi (ambazo zipo mpaka Leo)

Ukiangalia kwa Undani Historia hii ya kuzaliwa kwake inatia Shaka sana kabla ya Kujua Majibu ya kuzaliwa kwake inakuja Historia kwamba hana Baba. Kabla hujapata Majibu ya Baba ni nani Inakuja Kwamba ni Uwezo wa Mungu ndio akazaliwa. Yanakuwa Maswali juu ya Maswali

Kumbuka Yusufu na Mariam si kwamba Walikuwa ni Wachumba la hasha bali walikuwa tayari wapo Ndani (wameoana) wanaishi pamoja. Hakuna wachumba Wanaoishi pamoja kwa Utaratibu wa Kuishi. Ukichumbia wewe utakaa kwako na Huyo mchumba atakaa kwao. Kama Waliishi pamoja maana Yake waliweza Kushiriki Tendo la Ndoa yao na Ukifuatilia kwa Makini Yusuf alikuwa Pamoja na Mariam kila Sehemu hakuna Sehemu inayosema Alikuja Kumuoa mariam Ikiwa na Maana Kwamba Tayari alikuwa keshaoa maana yake ule uchumba ulio andikwa Tayari ukayeyuka

Binadamu huzaliwa Kwa Mwanaume na Mwanamke hili halina ubishi. Ila Kuna Kuja Utata wa Hapa Kwamba Yesu alizaliwa bila Mfumo maalumu wa Uzazi wa Baba na Mama ila Roho Mtakatifu kama Wanavyodai (kumbuka Hata Huko india Wapo Watu wenye Hadithi hizi hizi za Kuzaliwa bila Baba)

Sasa Hapa Unajiuliza Maswali. Mungu huyo aliyeweza Kumuumba Mwanadamu wa Kwanza Bila Kutumia mifumo ya Uzazi Inakuwaje leo aje Aanze Kumuumba Binadamu mwingine anayedaiwa ni Mwanae kwa Mifumo ya Uzazi na Akaenda kwa Mariam ambaye alikuwa teyari ana Mume(kumbuka Hapa Mungu hazai na Wala Hakuzailiwa)

Sasa Anamzaa mwanae kupitia Mariam mara Yusufu atake kumkimbia Mariam maana Kuna Siri May be Yusufu aliiona akaona Hapa Nimepigwa na Baada ya Yesu kuzaliwa Yusuf Anapotea Ghafla kwenye Maandiko na Historia yake inaishia Hapo hapo

Mungu anamtoa Mwanae. Anakuja Mnamkataa, mnampiga, mnamtesa anawahubiria mnagoma Kukubali maneno yake mnamfukuza kwenye masinagogo yake, Anaenda Kusali mlimani peke yake, anakusanya wanafunzi wake. Hao wanafunzi nao mnawakataa mnawafukuza. Hivi Mungu hapo anawaogopa Nyie kisa Nini mpak Awafanyie Haya Yote Nyie Viumbe wake

Yaani Mungu mpaka Anatoa Mtoto wake Wa Pekee ili awabembeleze nyie mmrudie Yeye na Mnakataa. Sasa Hapo Mungu Anakuwa na Ule Uwezo na Kutoshindwa Kitu kweli. Kama Kawatumia Mwanae na Mmemgomea kawatumia Manabii na Mitume mmemgomea Tena na hamtaki kumrudia. Hivi Mungu anawalemba Hivyo Ili Iweje

Si kila Mtu anayezaliwa bila Baba Yake basi Baba Yake ndio Mungu. Wachawi wanazini na Binadamu kila Siku na Wachawi hao hao ndio Binadamu wenzenu. Wanawake wanabeba Mimba zingine wasizozijua zimetoka wapi

Basi Mjue Kwamba Hapo Mwenye Enzi Mungu hayupo na Mnaozeshwa Akili zenu ndugu zangu. Kaeni Chini Mtafakari kwa Akili zenu Timamu. Mungu hawezi kufanya hayo Kwa Viumbe wake. Yeye hayupo Hivyo

[emoji3507]Mungu si Mmoja
[emoji3507]Mungu si Wengi
[emoji3507]Mungu si Baba
[emoji3507]Mungu si Mama
[emoji3507]Mungu si Kiumbe
[emoji3507]Mungu hachukii Viumbe
[emoji3507]Mungu hapendi Viumbe wake ila Ana Enzi na Viumbe wake (usijione wewe Kiumbe Mtu unapendwa na Mungu Kuliko Viumbe wake wengine aliowaumba)
[emoji3507]Mungu hakuzaa wala Kuzaliwa

Yachunguzeni maandiko Yenu mtajua kwamba si Maandiko ya kiucha Mungu ila Maandiko ya Viumbe wenye Tamaa

ASANTENI
Mwaana Mariamu alikuwa Demu tu , ambaye alikuwa amemtolea mahari, hakuwa mkewe bado wala hawakuwa wanaishi nyumba 1
Screenshot_20220303-102510.jpg
 
Soma Historia ya mapigano ya Wakristo ndugu yangu (crusade) au Alama Inayotumiaka ya P na X. Tumia akili Timamu hizo shule walisoma Watoto wa machifu kipindi cha Ukoloni wakati Babu zako ni watumwa. View attachment 2137107

Unaniletea picha ndio nifanyeje?. Unaleta Vita vya zamani uingereza na ottoman unadai ukristo unaenezwa kwa Vita. Wewe ndio ukasome Ni jinsi gani uislamu uliingia misri na majirani zake wakati ilikuwa nchi ya kikristo.

Halafu Acha uongo shule nyingi za dini mpaka leo zipo nyingi, mf mazengo ya zamani, Musoma Tech, Ngaza girls, Nsumba Tabora TTC.
 
Sasa Mbona Kwenye Mahubiri mnawambiwa watu watachomwa Moto kama Hawatamwamini Mwana wa Mungu na Yeye tu ndio Njia ya ukweli

Ndugu kila mmoja ana hiari ya kutangaza Imani yake ilimradi asivunje sheria. Sisi tunatangaza Imani yetu, Ni hiari yako kuiponda au kuikubali. Ila jehanamu ipo na wengi wataenda huko Kama hawakumpokea Yesu Kristo na kuishi Maisha matakatifu hapa duniani.
 
Naamin haujalazimishwa uamin, ukienda china utakuta watu wengi tu hawana dini na wanaishi vizuri hata wewe unaweza fuata mkondo huo, kila binadamu ana uhuru wa kuishi atakavyo ili mradi asivunje sheria na asiwe kero kwa mwenzake

Aidha umekosea kuni-quote, ama hujaelewa nilichoandika.
 
Sasa Mbona Kwenye Mahubiri mnawambiwa watu watachomwa Moto kama Hawatamwamini Mwana wa Mungu na Yeye tu ndio Njia ya ukweli
Kwanini wewe unaenda kusikiliza uongo Halafu unakuja kubisha humu jf? Kwanini usibishane na huyo anayekwambia utachomwa Moto?
Nenda kasikilize siasa ndo za ukweli achana na Mungu ambaye humwamini halafu unamfuatilia.
 
Shida ya mtoa mada ni kuwa umeziamini sana Akili zako na kuona ww unauwezo mkubwa wa kuchanganua mambo na kuyaelewa..
labda tu nikwambie kitu ambacho kitafanya ujue kuwa akili uliyonayo ni ndogo sana kwa ufahamu wa mambo ya Mungu(Yesu).
.
hapa duniani sio watu wote wamezaliwa na baba na mama, kuna watu wengi sana wanatembea wakionekana ni watu lakin sio watu, wengine majini, wengine walozi waliovaa miili ya watu, wengne misyuka lkn wanaonekana katika hali ya mwili kabsa. so usiishi kwa kukariri...
.
ushauri wangu kwako:- mambo ya Mungu(Yesu) ni mambo ya kiroho kwaiyo ukitaka kuyaelewa vzr nenda kiroho zaid lakini ukienda kimwili kwa akili hizo unazozitegemea hakuna kitu utaelewa
 
Aliyezaliwa sio Yesu ila ni Kristo

Mama D hivi unaona jinsi Gani akili zetu zimevurugika. Kwahiyo Yesu na Kristo ni Watu wawili tofauti tena. Hapa unakana Kabisa kwamba Yesu hakuzaliwa ila Alizaliwa Kristo ambaye Hata Hatujui ametajwa wapi.

Jina la Yesu lilishushwa toka kwa Mungu na malaika
Nabii anaye takwa kama Isaya Alitabiri Kuwa Ataitwa Emanueli Ila Malaika akaja akasema ataitwa Yesu wewe umemnasibu hapo ataitwa Kristo. Sasa Libebwe lipi liachwe lipi ndugu yangu

Mungu anafanya kazi ndani yetu kupitia roho, Mungu alikaa ndani ya Kristo kupitia
Mungu ana nafasi zake katika utendaji wake;

Mungu akifanya Kazi ndani yako wewe Maana yake Hakuwa na Haja Ya Kukupa Akili hiyo uliyonayo. Na Kama Akifanya Kazi ndani yako hawezi kukutuma Ukazini. Ukaibe. Ukaseme uongo.. Uue n. K n. K mana Ukifanya Hayo maana Yake Yeye ndio kakutuma

*Mungu ni baba katika nafasi yake ya uumbaji,

Mungu akiwa Baba Inabidi awe na Mama pia. Akiwa Baba Atakuwa na Watoto pia. Neno baba Maana Yake ni Jina La Viumbe wa Kiume wenye Watoto

*Mungu ni mwana katika nafasi yake ya ukombozi kupitia Kristo,
*Mungu oho mtakatifu katika nafasi yake ya kutenda kazi ndani yetu

Mwana maana Yake ni Mtoto wa.. Unaposema Mwana maana Yake ni Ubin wa Mtu. Ukimwita Mungu mwana. Maana yake Kazaliwa Huyo Mungu.

Yesu ni Mungu

Na je Alipokuwa anaomba Pale mlimani alikuwa anamwomba Nani!?
 
Kwanza Hongera kwa kuwa na akili ya udadisi ( curiosity). Nilivokuelewa haimaanishi kwamba ulichokiuliza haujui ukweli No unaujua ila unajaribu kuupindisha ukweli kuwa uongo kupitia elimu na maarifa yako ya kidunia kwenye spiritual zone sehemu ambapo unamuhitaji Sana Sana sana roho mtakatifu mpaka uelewe bila hivo ni vigumu Sana.

Pamoja na hayo ila inaonesha Kuna vitu vingine kweli hufaham kwa swala la utatu wa Mungu na namna unavofanya kazi katika maisha yetu ntakueleza kwa ufupi Sana ila zaidi kasome kitabu Cha Mwanzo(Old testament) walau sura ya 1-6 ni vitu ambavyo vipo deep deep Sana then nenda kasome Mathayo ( New testament) chote kina sura 28 kwa utulivu wa Hali ya juu unaweza kuelewa Mungu akisaidie.

Ila Mwisho ya yote Mungu Ni mmoja kweli na Ni roho ambayo ina nafsi 3.....Mungu Baba,Mwana na Roho mtakatifu na ndio maana wakati wa uumbaji ilitumika nafsi ya wingi NA TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU.

Hivo basi hiyo nafsi ya pili ya ambayo ilikuja duniani kwa njia ya mwili ili kufikisha ujumbe kwetu Sisi binadam tuache maovu na kutoa dam (sacrifice) ili tuokolewe baada ya kuwa mateka wa shetani kwa muda mrefu kumbuka bila ile damu hakuna chochote ambacho kingeweza kuleta upatanishi kati ya sisi na Mungu Baba na ndo maana hata waganga mpaka Sasa wanatumia damu ili kuingia maagano au upatanishi na nguvu za Giza,Na ndio maana jina lake Yesu likapewa nguvu na mamlaka duniani na hata mbinguni na Mungu Baba kwa kazi kubwa aliyoifanya,jiulize kwa Nini pepo ukilikemea kwa jina la Yesu linapiga kelele na kutoka utaelewa lakini tumia jina lingine lolote uone kama Kuna maajabu yeyote yatayotokea.

Na hiyo nafsi ya tatu hata wewe hapo unayo ambayo pia Ni Mungu ambayo inakuongoza kutenda yaliyo mema na kukuhukumu pale unapofanya mabaya ila huwez ukawa nayo ikiwa Kama utaendelea kuishi maisha ya dhambi na kuamini imani za kishirikina au majini au kitu kingine chochote chenye uungu ndani yake.

Mwisho nipende kukwambia ili uweze kufisha ujumbe kwa jamii au tamaduni Fulani basi Ni lazima na wewe na ile jamii (Be natural) Kama n wamasai basi vaa kimasai alafu kawape elimu watakuelewa sana ndivo ilivokuwa kwa yesu ambaye Ni Mungu nafsi ya pili ilibidi avae uhalisia wa kibanadamu ili ujumbe ufike lakini angekuja kama Mungu watu wangeogopa na wasingeelewa na kwanza hakuna ambaye angeweza kumuona kwasababu Ni Roho yenye nguvu Sana.

In short Ni hayo MUNGU AKUBARIKI.
 
Yohana 10:17-18
"Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu."

Angekufa akazikwa na kuoza ingekua joke. Siku tatu tuu alifufuka na anaishi hadi sasa duniani kote

Unapojadili kuhusu ukweli halafu una quote Kitabu ambacho watu wanautafuta Ukweli hawauoni kuna Leta ukakasi kidogo na Kwamba wewe mdugu yangu hutaki kutumia akili timamu

Unaposema Baba Maana Yake yeye Ni Binadamu kama Wewe maana Neno Baba Ni Mzazi wa Kiume
 
Kitu usichokijua uulize na sio kuwa mjuaji. Utakuwaje na Mungu ndani yako wakati unampinga na huamini juu ya Yesu Kristo.
Sasa Ndugu yangu ukiamini basi ndio anakuja Ndani yako anakaa. Kwahiyo unaenda kanisa kufanya Nini wakati yupo ndani yako. Na kama Yupo ndani yako Hao waumini wengine wanaenda Kumtafuta Nani huko kanisani wakati wewe ndie uliye naye

Anayekuongoza uende kwa Malaya ni shetani unayemshabikia ambaye mwisho wake sio mzuri. Tubu dhambi zako na uache maovu uzishike amri kumi za Mungu. Umpokee Yesu Kristo kuwa bwana na mwokozi wako hakika utaiona tofauti kabisa.

Mungu hakai ndani ya Kiumbe chochote ndugu yangu akikaa kwako maana Yake tayari Yeye mwenyewe ana Umbo La Size kama Yako. Wakati huo huo unasema Yupo mahali Pote

Majini na Malaila Waovu ndio wanaweza Kukaa ndani yako wewe wakakuendesha Watakavyo. Mungu hafanani na Viumbe vyake na Hana Tabia Ya Kiumbe Chake
 
Kuna Mambo Yapo Ulimwenguni ukiyatafakari kwa Kina hayaingii Akilini ndugu waafrika wenzangu

Kuna Historia katika Vitabu kwamba Mungu alimtoa Mwanae Ili aje Kuikomboa Dunia katika Dhambi (ambazo zipo mpaka Leo)

Ukiangalia kwa Undani Historia hii ya kuzaliwa kwake inatia Shaka sana kabla ya Kujua Majibu ya kuzaliwa kwake inakuja Historia kwamba hana Baba. Kabla hujapata Majibu ya Baba ni nani Inakuja Kwamba ni Uwezo wa Mungu ndio akazaliwa. Yanakuwa Maswali juu ya Maswali

Kumbuka Yusufu na Mariam si kwamba Walikuwa ni Wachumba la hasha bali walikuwa tayari wapo Ndani (wameoana) wanaishi pamoja. Hakuna wachumba Wanaoishi pamoja kwa Utaratibu wa Kuishi. Ukichumbia wewe utakaa kwako na Huyo mchumba atakaa kwao. Kama Waliishi pamoja maana Yake waliweza Kushiriki Tendo la Ndoa yao na Ukifuatilia kwa Makini Yusuf alikuwa Pamoja na Mariam kila Sehemu hakuna Sehemu inayosema Alikuja Kumuoa mariam Ikiwa na Maana Kwamba Tayari alikuwa keshaoa maana yake ule uchumba ulio andikwa Tayari ukayeyuka

Binadamu huzaliwa Kwa Mwanaume na Mwanamke hili halina ubishi. Ila Kuna Kuja Utata wa Hapa Kwamba Yesu alizaliwa bila Mfumo maalumu wa Uzazi wa Baba na Mama ila Roho Mtakatifu kama Wanavyodai (kumbuka Hata Huko india Wapo Watu wenye Hadithi hizi hizi za Kuzaliwa bila Baba)

Sasa Hapa Unajiuliza Maswali. Mungu huyo aliyeweza Kumuumba Mwanadamu wa Kwanza Bila Kutumia mifumo ya Uzazi Inakuwaje leo aje Aanze Kumuumba Binadamu mwingine anayedaiwa ni Mwanae kwa Mifumo ya Uzazi na Akaenda kwa Mariam ambaye alikuwa teyari ana Mume(kumbuka Hapa Mungu hazai na Wala Hakuzailiwa)

Sasa Anamzaa mwanae kupitia Mariam mara Yusufu atake kumkimbia Mariam maana Kuna Siri May be Yusufu aliiona akaona Hapa Nimepigwa na Baada ya Yesu kuzaliwa Yusuf Anapotea Ghafla kwenye Maandiko na Historia yake inaishia Hapo hapo

Mungu anamtoa Mwanae. Anakuja Mnamkataa, mnampiga, mnamtesa anawahubiria mnagoma Kukubali maneno yake mnamfukuza kwenye masinagogo yake, Anaenda Kusali mlimani peke yake, anakusanya wanafunzi wake. Hao wanafunzi nao mnawakataa mnawafukuza. Hivi Mungu hapo anawaogopa Nyie kisa Nini mpak Awafanyie Haya Yote Nyie Viumbe wake

Yaani Mungu mpaka Anatoa Mtoto wake Wa Pekee ili awabembeleze nyie mmrudie Yeye na Mnakataa. Sasa Hapo Mungu Anakuwa na Ule Uwezo na Kutoshindwa Kitu kweli. Kama Kawatumia Mwanae na Mmemgomea kawatumia Manabii na Mitume mmemgomea Tena na hamtaki kumrudia. Hivi Mungu anawalemba Hivyo Ili Iweje

Si kila Mtu anayezaliwa bila Baba Yake basi Baba Yake ndio Mungu. Wachawi wanazini na Binadamu kila Siku na Wachawi hao hao ndio Binadamu wenzenu. Wanawake wanabeba Mimba zingine wasizozijua zimetoka wapi

Basi Mjue Kwamba Hapo Mwenye Enzi Mungu hayupo na Mnaozeshwa Akili zenu ndugu zangu. Kaeni Chini Mtafakari kwa Akili zenu Timamu. Mungu hawezi kufanya hayo Kwa Viumbe wake. Yeye hayupo Hivyo

[emoji3507]Mungu si Mmoja
[emoji3507]Mungu si Wengi
[emoji3507]Mungu si Baba
[emoji3507]Mungu si Mama
[emoji3507]Mungu si Kiumbe
[emoji3507]Mungu hachukii Viumbe
[emoji3507]Mungu hapendi Viumbe wake ila Ana Enzi na Viumbe wake (usijione wewe Kiumbe Mtu unapendwa na Mungu Kuliko Viumbe wake wengine aliowaumba)
[emoji3507]Mungu hakuzaa wala Kuzaliwa

Yachunguzeni maandiko Yenu mtajua kwamba si Maandiko ya kiucha Mungu ila Maandiko ya Viumbe wenye Tamaa

ASANTENI

Andiko litanoga ukitujaalia Reference materials (Books, Journals, Reports, etc).

Bila hivyo hili andiko linafanana na Ramli zinginezo.
 
YESU ameshakuja na hakuwalazimisha wayahudi wamuamin hata wewe hulazimishwi umuamini YESU kama mtoto wa Mungu, ukristo tofauti na dini nyingine haumlazimishi mtu aamin doctrine yake
Umesema vema ndugu yangu.Binafsi ninasadiki kwa moyo wangu wote juu ya Yesu Kristo kuwa ni MUNGU kweli aliyeamua kuuvaa ubinadamu.Kimsingi sina swali kuhusu imani Yangu kwa MUNGU mmoja nafsi tatu.
 
Imani we Amini tu...., Ukiweka Logic sio Imani tena its a Science....

Kwahio kama wewe upo huko yabebe kama yalivyo... kuepuka kuombewa au kutolewa mapepo...
 
Wewe unamatatizo makubwa. Binadamu ndio anamuokoa binadamu mwenzake?.
Waliokufa na Meli ya Mv Bukoba nani alienda Kuwaokoa!? Wanaopata Ajali kila siku huko barabarani nani huwa anaenda Kuwaokoa. Mbona Ndugu yangu Hatutumii akili ya Kawaida tu. Hakuna Siku Mungu kaenda kuokoa Viumbe wake ndugu yangu

Acha kujitoa akili, nyie ndio mkiuguua tumbo mnaanza kulia Mungu nisaidie nakufa. Wakati wa Nuhu walikuwepo wabishi zaidi yako lakini mwisho ulipofika waliliia Kama watoto. Juzi hapa kulikuwa na Corona Tanzania tukafany maombi ya kufunga, je Kuna binadamu gani alikuwa ana uwezo wa kuondoa corona?.

Tumia tu Akili ndugu yangu hata Wajinga Wanaugua matumbo. Wachina Wanaugua matumbo. Washenzi wanaugua Matumbo kuugua Tumbo Ni hali ya Kawaida kwa Binadamu si kwamba Wanaougua Eti hawamjui Yesu ndio mana wanaugua

Kwani Babu zako waliokufa Kabla Ya Kumjua Huyo Mungu walikuwa hawaugui hayo Matumbo

Stori za Nuhu na Gharika wewe umezijua Juzi tu hapa Ndugu yangu baada ha Hiyo Biblia kuja Ulishawahi kusimuliwa hata na Bibi zako au Babu zako kwamba Mungu aliwaadhibu kwa Gharika. Hata Wao watakushangaa Gharika Ni Nini. Tatizo lenu mnapata Historia za Watu wengine hamuwajui mnazifanya Ndio Historia za Ulimwengu mzima. Gharika Linahusika Vipi na Wewe Mwafrika
 
Back
Top Bottom