50thebe
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 4,088
- 4,059
Kwanza Hongera kwa kuwa na akili ya udadisi ( curiosity). Nilivokuelewa haimaanishi kwamba ulichokiuliza haujui ukweli No unaujua ila unajaribu kuupindisha ukweli kuwa uongo kupitia elimu na maarifa yako ya kidunia kwenye spiritual zone sehemu ambapo unamuhitaji Sana Sana sana roho mtakatifu mpaka uelewe bila hivo ni vigumu Sana.
Pamoja na hayo ila inaonesha Kuna vitu vingine kweli hufaham kwa swala la utatu wa Mungu na namna unavofanya kazi katika maisha yetu ntakueleza kwa ufupi Sana ila zaidi kasome kitabu Cha Mwanzo(Old testament) walau sura ya 1-6 ni vitu ambavyo vipo deep deep Sana then nenda kasome Mathayo ( New testament) chote kina sura 28 kwa utulivu wa Hali ya juu unaweza kuelewa Mungu akisaidie.
Ila Mwisho ya yote Mungu Ni mmoja kweli na Ni roho ambayo ina nafsi 3.....Mungu Baba,Mwana na Roho mtakatifu na ndio maana wakati wa uumbaji ilitumika nafsi ya wingi NA TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU.
Hivo basi hiyo nafsi ya pili ya ambayo ilikuja duniani kwa njia ya mwili ili kufikisha ujumbe kwetu Sisi binadam tuache maovu na kutoa dam (sacrifice) ili tuokolewe baada ya kuwa mateka wa shetani kwa muda mrefu kumbuka bila ile damu hakuna chochote ambacho kingeweza kuleta upatanishi kati ya sisi na Mungu Baba na ndo maana hata waganga mpaka Sasa wanatumia damu ili kuingia maagano au upatanishi na nguvu za Giza,Na ndio maana jina lake Yesu likapewa nguvu na mamlaka duniani na hata mbinguni na Mungu Baba kwa kazi kubwa aliyoifanya,jiulize kwa Nini pepo ukilikemea kwa jina la Yesu linapiga kelele na kutoka utaelewa lakini tumia jina lingine lolote uone kama Kuna maajabu yeyote yatayotokea.
Na hiyo nafsi ya tatu hata wewe hapo unayo ambayo pia Ni Mungu ambayo inakuongoza kutenda yaliyo mema na kukuhukumu pale unapofanya mabaya ila huwez ukawa nayo ikiwa Kama utaendelea kuishi maisha ya dhambi na kuamini imani za kishirikina au majini au kitu kingine chochote chenye uungu ndani yake.
Mwisho nipende kukwambia ili uweze kufisha ujumbe kwa jamii au tamaduni Fulani basi Ni lazima na wewe na ile jamii (Be natural) Kama n wamasai basi vaa kimasai alafu kawape elimu watakuelewa sana ndivo ilivokuwa kwa yesu ambaye Ni Mungu nafsi ya pili ilibidi avae uhalisia wa kibanadamu ili ujumbe ufike lakini angekuja kama Mungu watu wangeogopa na wasingeelewa na kwanza hakuna ambaye angeweza kumuona kwasababu Ni Roho yenye nguvu Sana.
In short Ni hayo MUNGU AKUBARIKI.
Mkuu
Endelea kuelimisha na kuinjilisha. Inatufaa 🙏🏽