Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?


Mkuu

Endelea kuelimisha na kuinjilisha. Inatufaa 🙏🏽
 
Wewe unakaribia kuchanganyikiwa. Andaa mkutano uanze kufundisha watu Imani yako na sio kuvamia Imani za watu wengine ili Cha kwako kiwe Bora. Kwa kukufahamisha tofautisha Mungu na miungu yako. Mungu Ni mmoja na miungu Ni mingi zaidi ya elfu kumi.
Kama Mungu ni Mmoja Inakuwaje Yesu ni Mungu!?
 
Imani we Amini tu...., Ukiweka Logic sio Imani tena its a Science....

Kwahio kama wewe upo huko yabebe kama yalivyo... kuepuka kuombewa au kutolewa mapepo...
Logic in faith it's Science.

I can't agree more. Thank you
 
Kasome amri kumi za Mungu. Unafanya dhambi kwa sababu humpendi Mungu na unatumikia mapenzi ya shetani.
Yesu si Alifia dhambi zako msalabani. Inakuwaje wewe bado unadhambi!?
Tena Bado una dhambi ya Asili ambayo hakuifia Hiyo

Katika Amri kumi za Mungu Imeandikwa Usiue Ila Mbona Mwanamke mzinzi aliuawa ila Huoni mwanaume Mzinzi akiuawa huoni Bado Inaenda Nje ya Amri zake
 
Jikite kwenye hoja ya mleta mada,
Usihamishe magoli.


Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
 
Jibu swali, lete Aya inayosema Yesu si Mungu acha kuleta maelezo.
Tumia Akili ndugu yangu Kadhi Mkuu 1 . Kwani Wewe ubongo wako umeweka Pembeni mpaka Usaidiwe na Aya.

Yesu anatakuwaje Mungu halafu hapo hapo Anaomba Mungu? Hili si swala la Kutumia tu akili.

Basi Wewe niletee sehemu aliposema Yeye ni Mungu
 
Umesoma Biblia au unauliza ili uelewe.
Kasome mistari hii ifuatayo.

Yohana 1:18
Yohana 10:30
Wafilipi 2:5-6

Yeye Mwenyewe hakujinasibu kuwa ni Mungu ila Yohana.. Na Wafilipi ndio walimwita Mungu. Hivi mkuu unajua Kutumia tu akili timamu ni Jambo Jema sana

Hivyo vitabu vya Yohana na Wafilipi waandishi wake hawakuwepo hata Kipindi cha Yesu na VITABU vingi hivyo ni Masimulizi ya Watu ambao wengi wao si Mitume ila viliandikwa kwamba Ni Vitabu vya Mitume wakati Mitume hawakuandika Vitabu hivyo
 
Tafuta Neno Crusade. Sijakuletea Picha Tu Jua hizo vita Zilipiganwa kwa Kupitia Dini Gani
 

Hakuna kisichoeleweka hapo ni wewe tuu hutaki kuelewa

Unavyojivuruga mwenyewe kwa kushindwa kusoma maandiko na kuyaelewa badala ya kubeba mistari michache na kukimbia nayo ndivyo unavyozidi kuvurugika

Aliyezaliwa na Mariam ni Kristo ambaye malaika alitumwa amwambie akishazaliwa amwite jina lake Yesu, Sio Yusufu wala Mariam walimpa hilo jina

Mathayo 2: 3-4
"Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, KRISTO azaliwa wapi?"
Luka 1: 26-27; 30-33
Malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,
kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.
Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.
Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

Ijue maana ya jina Imanueli. Baada ya jina hilo kutajwa kwenye Isaya 7:14 nenda kasome Isaya 9:6. Usisome biblia vipandevipande ukatoa hitimisho, jitahidi kusoma uelewe. Ila kama imani yako sio kwa biblia basi nyamaza tuu sababu utaongea hata yasiyokuwako
Isaya 7:14
"Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli."
Isaya 9: 6
"Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani."
 
Ndugu yangu huoni Unazidi kujipotosha. Mungu haongei na Wala haandiki chochote kile. Ukiona Umeambiwa Usichunguze maana Yake Yana Uongo humo Ndani yake.
Sasa hapo unasemaje juu ya Jiwe kuliweka shirika la ndege chini ya ofisi ya Rais ili lisichunguzwe?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna watu wengi Kama wewe wanaopotosha. Biblia ndio inasema tena Yesu Kristo mwenyewe anasema ya kwamba utafuteni ufalme wa Mungu na mengine yote mtazidishiwa. Hiyo ndio Imani ya Kikristo.
Mungu Kaumba Viumbe wengi. Majini.. Malaika.. Binadamu n.k kwahiyo akakupenda Wewe sana Akakuambia Umtafute

Yaani Amekuumba halafu akakuweka Duniani Halafu akakuambua Umtafute tena yeye Alipo?

Mungu keshakuumba Ukiamua Kumtii ni juu yako ukiamua Kutomtii wala Hakukasirikii maana Teyari keshakupa Akili
 
Kuna Utata mkubwa Sana Katika kuzaliwa kwa Yesu kutokana Na Maandiko ya Biblia. Ila Kwa Akili Timamu Binadamu yeyote lazima Azaliwe kwa Mifumo maalumu ya Mbegu ya Kiume kuungana Na Mbegu ya Kike Tofauti na Hapo Binadamu hawezi Kutokea
Mkuu kwani Yesu ni binadamu au Mungu?
 
Kwani Corona Imeisha!? Mbona Raisi wako anasisitiza Ipo na Anavaa Barakoa
 
Kama Mshana Jr ??
 
Wewe unakaribia kuchanganyikiwa. Andaa mkutano uanze kufundisha watu Imani yako na sio kuvamia Imani za watu wengine ili Cha kwako kiwe Bora. Kwa kukufahamisha tofautisha Mungu na miungu yako. Mungu Ni mmoja na miungu Ni mingi zaidi ya elfu kumi.
Mungu wa Kweli haubiriwi kama Ulivyokaririshwa Wewe ndugu yangu. Watu wengi sana Hapa Duniani waliitwa Miungu. (Yehovah. Yire.. Zambe..Allah n.k) hao si Mungu mana Hawana Sifa za Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…