Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Kitabu gani kinachosema kuna watu walikuwepo kabla ya Adam?
Soma Historia za Wazee wako na Babu zako na Jadi utajua Ukweli. Adam na Hawa si Binadamu wa Kwanza

Afrika Kulikuwa na Watu na Ulaya Pia Kulikuwa na Watu.
 
Similarities, tufanyaje ili tuondoe izo brainwashing
Tumieni akili Timamu Waafrika wenzangu. Na Jueni kweli kwa Kuchunguza Mnavyoletewa mtu hawezi kukusimulia mambo Ya Viumbe wengine halafu Yeye mwenyewe hajijui ametokea wapi. Leo hii mtu anakusumulia kuhusu Israeli na makabila yake ila Yeye kabila Lake hajui limetoka wapi

Jijue kwanza wewe kabla ya Kujua Wengine na Vita zao zisizokuhusu
 
Mkuu unaonekana unaamini uchawi. kuamni uchawi na unavyoviandiaka kwenye nyuzi zako, inanifanya nikupotezee.
 
Dini zinasambazwa kwa lazima, kuna mataifa ukiwa mkristo unakatwa kichwa mfano Afghanistan. Hivyo siyo ukristo tuu ulioenezwa kwa lazima.
Kwahiyo kumbe Unajua kwamba ilikuwa ni lazima uupokee Ukristo na hizo dini zingine nazo zipo zinalazima Mzikubali

Wazee wenu na Babu zenu walilazimishwa hivyo hivyo
 
Acha kutumia muda mwingi kuandika visivyoeleweka.maana hadi hapa nimegundua wewe ndiye ambaye hutaki kuelewa kilichomaanishwa kwenye biblia.badala yake inaunga unga nadharia zako ambazo hazina mantiki.

Umesema Yesu ni Mungu. Aliuawa na Akafa siku tatu akafufuka. Nimekuuliza kwahiyo Dunia Ilikuwa haina Mungu Kwa Siku tatu?

Sema Mantiki yangu Haipo wapi
 
Kwa hivyo unataka kusema Biblia Ni uongo kumuita Mungu Yehovah. Kama Biblia Ni uongo endelea kufanya Uzinzi na dhambi zingine.
Nani kakuambia watu walikuwa hawazini na Hawana Dhambi mpaka biblia ilipokuja. Na nani kakuambia Biblia imeandika ukweli kama ingekuwa imeandika ukweli watu wasingetawanyika Kwenda kuutafuta

Maana Humo humo kwenye Biblia kuna Wasabato.. Walutheri.. Wakatoliki. Wazumaridi.. Wa AIC.. Wa Anglicana.. Walokole na Madhehebu mengine 1000 na Kidogo

Mungu gani anataka Muwe makundi makundi hamna Umoja
 
Yaani hakuna sehemu Mungu huwa anadharaulika na kutukanwa Kama jf, Kama una Imani yako imelegalega unaweza Hadi kurudi nyuma kiroho.Mungu aturehemu
Imani yako haiwezi Lega Lega kama Una ukweli ndani yako ndugu yangu. Wale wasio na Ukweli ndio wanalega lega na Kupotea Direction maana wanachokiamini hawakijui kwa Undani wake
 
Japo wakristo wamekataa kunipokea ila niwasaidie tu kujibu swala la kutoa sadaka na hayo mengine mtoa mada haujarleweka zaidi ya kuleta ubishi tu wa vijiweni.
Mungu ahitaji sadake zetu ila sisi tunahitaji kutoa sadaka ili tuwe kama yeye. Yeye na sisi tunaotofauti kama vile nguo safi(yeye) na nguo chafu(sisi).
Sisi tunatenda zambi ila yy hatendi zambi na tunatumia nguvu na jitihada nyingi ili tuwe kama yeye.
 

Ndio maana watu wanakuuliza Maswali uitetee hiyo imani kama Ni ya kweli Wataufuata. Sasa unapoulizwa maswali unaanza Kumtisha Mtu na Jehanamu kisa hayampokea Yesu unakuwa unawatisha Watu ndugu yangu.

Mtu ambaye ni mtakatifu si Mcha Mungu. Mtu yeyote anaweza kuwa Mtakatifu manaa Utakatifu ni unadhifu tu ukioga na Kuoendeza Na Kuvaa Nguo safi wewe tayari ni mtakatifu.

Takatifu ni Nguo iliyooshwa na Kutolewa uchafu (imetakata) na Kuwekwa mahala pale ukiivaa wewe na Huku umeoga na Kuwa msafi ndio Unakuwa Mtakatifu

Kwahiyo Njiani huko unakutana na Watakatifu kibao tu Ndugu yangu ila si Wacha Mungu
 
Mwana wa Mungu ni Mungu au binadamu?.
Nani alisema ya kuwa Yesu ni mwana wa Mungu ?

Je katika Biblia tamko mwana limetumika kwa Yesu tu peke yake ?

Kwanza nataka tufikie muafaka hapa je ni kweli Yesu ni mwana wa Mungu. Naomba nithibitishie hilo, sababu nachojua mimi Mola wetu hajazaa wala hakuzaliwa na wala hana mfano wa kitu chochote.
 

Shida kubwa ni uelewa wako wala sio kutokueleweka kwa maandiko
Baba maana yake ni muanzilishi/Muumbaji

Muumbaji wa kwanza na pekee ni Mungu na yeye aliwarithisha binadamu kazi ya kuuendeleza uumbaji katika ulimwengu huku mwanaume akiwa muumbaji katika ngazi ya kuongeza uzazi yaani baba

Baba asili yake ni muumba sio wewe uliye mwanaume wa leo
 
Shida ya mtoa mada ni kuwa umeziamini sana Akili zako na kuona ww unauwezo mkubwa wa kuchanganua mambo na kuyaelewa..
labda tu nikwambie kitu ambacho kitafanya ujue kuwa akili uliyonayo ni ndogo sana kwa ufahamu wa mambo ya Mungu(Yesu).
Hiki ndicho kitu kilichowaharibu sana Waafrika mpka mnaambuwa IQ zenu ni ndogo. Ndugu yangu hakuna kitu kikubwa kama Akili yako Timamu uliyonayo na Mungu mwenye Vyote ndie aliyekuwekea. Ukitegemea Mzungu aje ndie akutafsirie Sijui Roho gani ije Ikuingie ndio ujue Maandiko utazidi haribikiwa.



.
Hao ndio viumbe wanaowaharibu akili sana Mpaka leo Hamjijui Mnataka Nini. Kama Wewe mwenyewe umekiri kwamba Kuna Viumbe wanatembea na Miili kumbe si Watu basi kubali Pia Unaweza Hubiriwa Pale Kanisani na Huyo Huyo Jini na Walozi



.
ushauri wangu kwako:- mambo ya Mungu(Yesu) ni mambo ya kiroho kwaiyo ukitaka kuyaelewa vzr nenda kiroho zaid lakini ukienda kimwili kwa akili hizo unazozitegemea hakuna kitu utaelewa

Mimi nina Mwili unatakaje niende kiroho wakati unatakiwa Unieleweshe nikiwa na Akili zangu mwenyewe ndugu yangu. Wewe unataka Upate Akili kutoka kwa Nani ndio uelewe. Yaani Ili Nielewe inabidi hii akili yangu niiweke Pembeni nisubiri akili kutoka Kwingineko ndio nielewe

Hapo ndugu yangu si unaona Kabisa unakuwa Msukule kabisa. Yaani Hao Viumbe wamewaambia Ili Myajue Maandiko inabidi Mtolewe akili zenu za Kawaida mpewe zingine. Daaah
 

Sasa Nini maana Ya Kuja Kunihubiria Kama unayenihuburia siwezi kuyaelewa. Hivu hili jambo Lako linaingia akilini kweli yaani Mimi Nione umesema Kikombe au umeandika Kikombe ila Nisitafsiri ni Kikombe ila nisubiri Akili Nyingine ije iniambie kwamba Kile si kikombe ni Sahani. Kuniambia Mimi kwa Mafumbo maana Yake unakitu unataka nisijue




Mungu hawezi akawa Mmoja Halafu akawa tena Na Wengine wawili. Hivi hili jambo linaingia Akilini kweli. Au ndio Ukiuliza Unaambiwa Ni Fumbo la Imani

Tutumie tu akili Zetu. Ndio maana Utatu hauna Majibu yanaoingia Akilini ndio maana Inafikia Hatua Mnasema Ni Fumbo la Imani. Fumbo maana Yake ni Kufungwa Kutoakujua Kitu chochote kwahiyo usiseme wewe unaujua Utatu wakati Umeshambiwa Ni Fumbo
 
Mtu alipigwa kipigo cha mbwa koko akashindwa kujitetea akaanza kumlilia Mungu wake amsaidie bado watu wanasema mtu huyo ni Mungu.. cha ajabu zaid hadi wasomi wakubwa wapo kwenye mkumbo huo yaan elimu zao za kwenye makaratasi hazijawasaidia kufikiria zaid.

Hivi hizo siku 3 alizokufa dunia ilikuwaje? Nani alikua akiongoza hii dunia? Hayo madhambi mbona yanazidi kama alifia msalaban kwa ajili yenu?

Waafrica njli watumwa sna kujikomboa kiuchum na kifikra tutasubiri sana
 
Andiko litanoga ukitujaalia Reference materials (Books, Journals, Reports, etc).

Bila hivyo hili andiko linafanana na Ramli zinginezo.
Kwahiyo bila Kutumia Vitabu vilivyoandikwa na Binadamu wenzako wewe Akili zako pekee huziamini mpaka Upate reference

Kwahiyo ukiambiwa hata Yesu ndio Mungu Mkuu unakubali tu kisa Imeandikwa sehemu ingawa unajua Sivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…