Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Mimba Hutungwa Kwa Mwanaume na Mwanamke kukutana na Mbegu zao kuungana. Ndipo mtoto hutokea
Ukitaka kuhoji kila kitu kinachomhusu Mungu utaona kama haiwezekani ila vyote kwake inawezekana...ukikataa kuzaliwa kwa yesu bila mbegu za kiume utaweza kukubali adamu kutoka kwenye udongo?
 
Kisai Nilisha kupa mafunzo naona bado unafanya kichwa kuwa kigumu, anapoongelewa Mungu wa wakristo usiweke uelewa wako wa mungu allah , utaishia kujiuliza maswali kama unavyouliza hapa

Allah huyu hapa
  • Anajihoji mwenyewe atakuwaje awe na mwana na hana mke? yani uwezo wake hawezi kuwa na mwana bila mke, yani angepata mke angekuwa na mwana kwa logic yake!
    • Koran 6:101. .... Itakuwaje awe na mwana naye hakuwa na mke?
  • Anajijibu kama angetaka mke basi angechukuwa wa jamii yake allah anatumia neno sisi, Hapa kuna cha kujiuliza Allah wako wangapi mpaka achukue jamii yake? anajijibu jamii yake ni malaika na houris wenye macho makubwa
    • Koran 21:17 Tafsir al-Jalalayn Had We desired ... partner or a child We would have found it with Ourselves from among the beautiful-eyed houris or angels were We to do so
  • Anajijibu mwenyewe kwamba kama angetaka kuwa na mwana basi angeteua amtakae
    • Koran39:4. Lau kuwa Allah angeli taka kuwa na mwana, basi bila ya shaka angeli teua amtakaye katika alio waumba.
Usirudie tena kuweka Allah uwezo na jinsi alivyo na Mungu wa Wakristo , wapo tofauti kabisa
Allah ni physical Being na Mungu wa Wakristo ni Roho ni nature mbili tofauti kabisa
Huna uwezo wa kunipa mafunzo katika hili labda kwenye mambo mengine kijana. Kingine nimeuliza maswali hujibu maswali niliyo uliza unaruka ruka kuleta ujuaji na mambo usiyo kuwa na elimu nayo.

Jibuni maswali niliyo uliza kisha ulete hoja nyingine. Katika watu wanao kimbia maswali humu ndani wewe ni mmoja wapo.
 
Usirudie tena kuweka Allah uwezo na jinsi alivyo na Mungu wa Wakristo , wapo tofauti kabisa
Allah ni physical Being na Mungu wa
Wewe ndiyo ulikimbia maswali yangu, ya kuelezea inakuwaje roho bila umbo.

Usiwe unakimbia maswali nakurudia hoja ulizo jibiwa.
 
Wewe unapenda Reference za Vitabu basi Kubali Kuwa Ulikuwa Sokwe pia maana Si Vitabu vimeandikwa vya Historia ndugu yangu

Mkuu

Kuchamba kwingi sio sawa na kuupiga mwingi.

Nakuhakikishia, ipo siku neno la tafuteni mtapata litatimia kwako. Sina mashaka.
 
Kuna Mungu Mmoja aliye baba na ana mwanawe anaitwa yesu kristo
Yesu anaitwa Mungu kwa sababu kazaliwa na Mungu na karithi asili,tabia na sifa za Mungu
Ndugu unahisi umetumia akili yako vizuri hapo. Adam yeye ni mtoto wa nani km Yesu ni Mtoto wa pekee
 
Ndugu yangu Ngoja nikuambie kitu Kimoja. Ambacho najua Kitakufungua Akili kidogo kama Mm unaona Naamini Uchawi.

Yesu alipopatwa na Magumu alikimbilia Kuongea na Musa na Elia ambao walikuwa si malaika wala si Mungu bali Binadamu waliowahi ishi hapa Duniani. Maana Yake ki Utu tu ni kwamba alienda Kuongea na Mizimu ya Musa na Elia

Jiulize kwanza Hilo kabla Hujaanza Kuniuliza naaminj Uchawi(ushirikina) wakati Yesu alishirikiana na Mizimu ya Musa na Elia. Kitu ambacho ww unakiona si Ushirikina. Kwanini Aongee na Musa na Elia wakati Mungu Yupo.

Tafakari hilo kwanza
Uchawi na mambo ya mizimu vitu viwili tofauti, uchawi ni Imani ya kuwepo kwa nguvu isiyo ya kawaida kufanya shughuli mbalimbali, Kwa mfano, kutumia chumaulete au misukule kupata Hela kirahisi, kupaa na ungo, kurogana nk hii Imani ni ujinga sana kuiamini, inarudisha nyuma sana IQ. Kuzimu ni sehemu ambayo siyo motoni Wala mbinguni, ila wanakaa wafu kungojea hukumu, baada ya kufa na kufufuka Kwa Yesu, kilifunguliwa Hali tatu, mbinguni, motoni na toharani. Hiyo ni kadiri ya mafundisho ya kanisa katoriki, ndo kusema Sasa kuzimu haipo Tena, waliokuwa wanakaa kuzimu ndiyo mizimu
 
Wewe ndiyo ulikimbia maswali yangu, ya kuelezea inakuwaje roho bila umbo.

Usiwe unakimbia maswali nakurudia hoja ulizo jibiwa.
Roho ambayo ipo ndani yako ina umbo?
Cha msingi nacho kukusisitiza tambua kwanza utofauti wa Allah na Mungu wa wakristo ,ukisha tambua hilo hutauliza maswali kwa kuweka uelewa wako wa Mungu Allah kwa Mungu mwingine

Allah amesema wazi na scholar wote wa waislamu wanakubali ni physical being , una umbile linashikika

Sema umbile lake ndio hivyo la kutisha , mikono miwili upande mmoja
 
Kusoma Biblia hakuwezi kukuokoa anayekuokoa ni Binadamu mwenzako tu. Ukizama majiini utaokolewa, ukipata ajali utaokolewa, Biblia imejaa utunzi wa Binadamu

Ni bora ukakombolewa maana anayekukomboa ni Yule anayekuambia Ukweli. Kumbuka Adam na Hawa si Binadamu wa kwanza Kama Biblia inavyosema mana Adam na Hawa waliwakuta Binadamu Duniani kitu ambacho Biblia haijakisema
Hapa kuna kitu cha kujifunza. Umesema binadamu wa kwanza sio Adam na Hawa. Ehe, binadamu wa kwanza hapa duniani alikuwa nani?
 
Wewe ndiyo ulikimbia maswali yangu, ya kuelezea inakuwaje roho bila umbo.

Usiwe unakimbia maswali nakurudia hoja ulizo jibiwa.
Issue sio maswali nataka ukiri kwanza Allah na Mungu wa wakristo ni tofauti ,ndio nitaendelea na majibu , kinyume Cha hapo siwezi kukujibu maana unaleta nature ya physical being (Allah) na nature ya Spirit (Mungu wa wakristo) ambavyo ni vitu viwili tofauti
 
Kuna Mambo Yapo Ulimwenguni ukiyatafakari kwa Kina hayaingii Akilini ndugu waafrika wenzangu

Kuna Historia katika Vitabu kwamba Mungu alimtoa Mwanae Ili aje Kuikomboa Dunia katika Dhambi (ambazo zipo mpaka Leo)

Ukiangalia kwa Undani Historia hii ya kuzaliwa kwake inatia Shaka sana kabla ya Kujua Majibu ya kuzaliwa kwake inakuja Historia kwamba hana Baba. Kabla hujapata Majibu ya Baba ni nani Inakuja Kwamba ni Uwezo wa Mungu ndio akazaliwa. Yanakuwa Maswali juu ya Maswali

Kumbuka Yusufu na Mariam si kwamba Walikuwa ni Wachumba la hasha bali walikuwa tayari wapo Ndani (wameoana) wanaishi pamoja. Hakuna wachumba Wanaoishi pamoja kwa Utaratibu wa Kuishi. Ukichumbia wewe utakaa kwako na Huyo mchumba atakaa kwao. Kama Waliishi pamoja maana Yake waliweza Kushiriki Tendo la Ndoa yao na Ukifuatilia kwa Makini Yusuf alikuwa Pamoja na Mariam kila Sehemu hakuna Sehemu inayosema Alikuja Kumuoa mariam Ikiwa na Maana Kwamba Tayari alikuwa keshaoa maana yake ule uchumba ulio andikwa Tayari ukayeyuka

Binadamu huzaliwa Kwa Mwanaume na Mwanamke hili halina ubishi. Ila Kuna Kuja Utata wa Hapa Kwamba Yesu alizaliwa bila Mfumo maalumu wa Uzazi wa Baba na Mama ila Roho Mtakatifu kama Wanavyodai (kumbuka Hata Huko india Wapo Watu wenye Hadithi hizi hizi za Kuzaliwa bila Baba)

Sasa Hapa Unajiuliza Maswali. Mungu huyo aliyeweza Kumuumba Mwanadamu wa Kwanza Bila Kutumia mifumo ya Uzazi Inakuwaje leo aje Aanze Kumuumba Binadamu mwingine anayedaiwa ni Mwanae kwa Mifumo ya Uzazi na Akaenda kwa Mariam ambaye alikuwa teyari ana Mume(kumbuka Hapa Mungu hazai na Wala Hakuzailiwa)

Sasa Anamzaa mwanae kupitia Mariam mara Yusufu atake kumkimbia Mariam maana Kuna Siri May be Yusufu aliiona akaona Hapa Nimepigwa na Baada ya Yesu kuzaliwa Yusuf Anapotea Ghafla kwenye Maandiko na Historia yake inaishia Hapo hapo

Mungu anamtoa Mwanae. Anakuja Mnamkataa, mnampiga, mnamtesa anawahubiria mnagoma Kukubali maneno yake mnamfukuza kwenye masinagogo yake, Anaenda Kusali mlimani peke yake, anakusanya wanafunzi wake. Hao wanafunzi nao mnawakataa mnawafukuza. Hivi Mungu hapo anawaogopa Nyie kisa Nini mpak Awafanyie Haya Yote Nyie Viumbe wake

Yaani Mungu mpaka Anatoa Mtoto wake Wa Pekee ili awabembeleze nyie mmrudie Yeye na Mnakataa. Sasa Hapo Mungu Anakuwa na Ule Uwezo na Kutoshindwa Kitu kweli. Kama Kawatumia Mwanae na Mmemgomea kawatumia Manabii na Mitume mmemgomea Tena na hamtaki kumrudia. Hivi Mungu anawalemba Hivyo Ili Iweje

Si kila Mtu anayezaliwa bila Baba Yake basi Baba Yake ndio Mungu. Wachawi wanazini na Binadamu kila Siku na Wachawi hao hao ndio Binadamu wenzenu. Wanawake wanabeba Mimba zingine wasizozijua zimetoka wapi

Basi Mjue Kwamba Hapo Mwenye Enzi Mungu hayupo na Mnaozeshwa Akili zenu ndugu zangu. Kaeni Chini Mtafakari kwa Akili zenu Timamu. Mungu hawezi kufanya hayo Kwa Viumbe wake. Yeye hayupo Hivyo

[emoji3507]Mungu si Mmoja
[emoji3507]Mungu si Wengi
[emoji3507]Mungu si Baba
[emoji3507]Mungu si Mama
[emoji3507]Mungu si Kiumbe
[emoji3507]Mungu hachukii Viumbe
[emoji3507]Mungu hapendi Viumbe wake ila Ana Enzi na Viumbe wake (usijione wewe Kiumbe Mtu unapendwa na Mungu Kuliko Viumbe wake wengine aliowaumba)
[emoji3507]Mungu hakuzaa wala Kuzaliwa

Yachunguzeni maandiko Yenu mtajua kwamba si Maandiko ya kiucha Mungu ila Maandiko ya Viumbe wenye Tamaa

ASANTENI
Dah ndio maana sipendi kuwa na hela sana wala kukosa hela sana ,matokeo yake ndio kuanza kutoa maneno makufuru,Kumbuka kila neno ulinenalo utatoa hesabu(ushahid )siku ya mwisho.
 
Back
Top Bottom