Mungu mwenye Upendo hawezi kuchoma watu kwa moto. Huo ni Ushetani

yofauti yako na yangu ni ndoooogo sana.. mimi naamini Mungu kupitia Mwanadamu yaani nguvu na sifa zote alizonazo utazipata kwa mwanadamu..
hata maelezo yako yananisapoti japo mimi sikatai uwepo wa nguvu za kiMungu kwetu wanadam.. ndio mana tunasameheana. tunasaidiana. tunahukumiana. yunaoneana hutuma. tunazalishana. tunaabudiana. tunaumba na viumbe vingine mfano chawa... nk
 
Kwamba yesu alipokufa ndo ikawa nini.

Kwamba Mungu ndo anamamlaka ya kufuta na kusamehe dhambi.
Halafu amtume yesu aje kufa kwa ajili ya hzo dhambi...

Akifa mwanae ndo dhambi zifutike

This is insane
yesu hakuuliwa na Mungu.. inasemwa hivyo ili kutuliza wafuasi wake.. yesu aliingilia maslah ya watu... hivi kwa mfano. atokee mtu anatibu kila ugonjwa.. anagawa vyakula. hivi watu wa tiba na wakulima au wafanyabiashara watamuacha Hai??
 
Baada ya UASI mbinguni
Mungu alituumba kwa mfano wake, lengo kuu ni tumuabudu.
Kwa kutamka vyote vikawa

Shetani akaileta dhambi duniani

Mungu akamtuma Yesu atukomboe kwa kufa.

Tukapokea Neema na Rehema

Mungu ataangamiza dhambi na dunia ya dhambi, kama binadamu naye ni mdhambi itampasa naye aangamizwe.
 
Kuna vitu hatuvioni kwa macho, je ndiyo tuseme havipo? mfano upepo,mawimbi ya sauti,electronic signals etc . Wewe kutokumuona Mungu haimaanishi hayupo
katika ukweli na kiukweli, kisichoonekana kusikika wala kunusika ujue hiko hakipo.. ila kiimani yaweza kua konyume chake.

na kwanini mnaamini Mungu haonekano huku mkiamini alituumba kwa mfano wake.? Jipende mpende na mwenzako basi utakua umempenda Mungu. MUNGU NI UPENDO FULL STOP
 
yesu hakuuliwa na Mungu.. inasemwa hivyo ili kutuliza wafuasi wake.. yesu aliingilia maslah ya watu... hivi kwa mfano. atokee mtu anatibu kila ugonjwa.. anagawa vyakula. hivi watu wa tiba na wakulima au wafanyabiashara watamuacha Hai??
Si tunaambiwa eti Yesu alitumwa na babaye aje kufa Ili watu wakombolewe kwenye dhambi!?

Au nnakosa ufahamu wa jambo hili?
 
Mbingu haipo, ni hadithi tu

Hata huyo Mungu na shetani ni hadithi tu, hawapo in real dimension.

Kwanini Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote alimshusha shetani kwenye sayari hii ya dunia?

Kwanini asimshushe hata Alpha centauri B huko nje ya solar system?
 
MUNGU MUUMBA MBINGU NA NCHI NI PENDO, HAKIMU WA HAKI... HUHUKUMU SAWA NA AGIZO LAKE... HAPANGIWI.... MWANADAMU AKING'ANG'ANIA JEHENAMU MUNGU AFANYEJE!!! UTAJIHUKUMU KWA MATENDO YAKO... MUNGU ALAUMIWE KWA LIPI WAKATI UCHAGUZI NI WAKO ??
 
kuna sehemu Mungu amekusikia Fimbo umfuate
Kuna sehemu amekusikia fimbo umfuate achana naye kwanin uteseke
If you think education is expensive try ignorant

Kuna watu kibao hawana dini na wanaishi kawaida kama huamin mapokeo yake achane naye sababu huwezi mbadilisha
 
Mungu mwenye kujua yote, Je Hakujua kwamba shetani atakuja kuwepo amdhibiti?

Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Alishindwaje kuumba Binadamu na dunia isiyo na dhambi?

Mungu muweza wa yote, Alishindwaje kumdhibiti shetani tangu mwanzo wa uasi?
 
Wanao sema hakuna Mungu naomba mniambie
Ni nini chanzo cha ulimwengu,maji,hewa ardhi na viumbe hai.

Kifo ni nini.
Mimi sifahamu fika chanzo cha huo ulimwengu.

Na naamini hakuna ajuaye zaidi ya nadharia tu,

Wewe unaweza kuwa unajua chanzo cha hayo uliyoyasema ili unieleze nami nisiwe mjinga tena!?
 
Kama wewe huamin hakuna ni uhuru wako kuamini hivyo sababu hujashikia fimbo umwamini

Lakin sis wengine tunaamini mbingu ipo tutaendelea kuamini
 
Mungu ameshindwa kila kitu basi kuwa mpagani sio lazima umwamin najiulizaga kwanini unateseka kwa kitu au jambo umesha-rule ni uongo we achana naye
 
Hujielewi kijana.

Ukisikia Mungu ndiye hakimu wa haki unaelewa nini?

Kuna watu dunia hii wanaringia vyeo vyao pesa zao kuwanyanyasa wengine ,kuwadhulumu nafsi zao nk ,hao watu wanaringia kwa sababu hakuna lolote wanaweza kufanya, sasa haki ya huyu mnyonge aliyedhulumiwa iwe kuishi au kunyanyaswa vyovyote vile Mungu ndiye husimama kama hakimu kujikimu kesi hii.

Bila Mungu kutoa adhabu unafikiri hao watu waliodhulumiwa haki zao watazipata wapi?

Tuanzie hapa kwanza.
 
Kuna vitu hatuvioni kwa macho, je ndiyo tuseme havipo? mfano upepo,mawimbi ya sauti,electronic signals etc . Wewe kutokumuona Mungu haimaanishi hayupo
Hakuna aliyesema anataka kumuona Mungu

Ulivyovitaja vyote vinathibitishika kuwa vipo,
Vinaweza kupimwa kabisa na ikiwezekana hata kufanyiwa maneuvers.

Huyo Mungu unawezaje kumthibitisha kuwa yupo?
 
MUNGU MUUMBA MBINGU NA NCHI NI PENDO, HAKIMU WA HAKI... HUHUKUMU SAWA NA AGIZO LAKE... HAPANGIWI.... MWANADAMU AKING'ANG'ANIA JEHENAMU MUNGU AFANYEJE!!! UTAJIHUKUMU KWA MATENDO YAKO... MUNGU ALAUMIWE KWA LIPI WAKATI UCHAGUZI NI WAKO ??
Mungu muumba mbingu na nchi anawezaje kuwa Pendo, Kwenye Dunia yenye Uovu, Mabaya, Magonjwa na Majanga ya asili kama radi, mafuriko, matetemeko ya ardhi, vimbunga?

Huyo Mungu mwenye upendo yupo kweli?
 
Mungu aliyeumba mbingu na nchi na vilivyomo.
Asiyejulikana hata jina lake Kwa sababu hajawahi kuonekana popote pale na Wakati wowote ule.
Kwakulazimisha uamuamin mbona unalazamisha mambo hayana mantiki
We kuwa mpagani hata kufanya chochote sababu wewe hutakua wakwanza

Kuna namna nakuonaga una upeo mdogo sana wa maisha kila siku unaanzisha uzi wa kumponda Mungu inshort huna content sababu mada zako ni zile zile kila siku

Unachofanya hata sio unique wala acts of genius kama lengo lako unalotaka lionekane watu kibao walishamkataa Mungu na wakaanzisha dini yao inaitwa atheist
 
That is your wishful thinking tu,

Hakuna wa kuwawajibisha hao.

Unataka kusema Simba bob junior nae atalipiwa aliyofanyiwa!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…