Wataalamu wa dini mje hapa?
Je, kuna andiko lolote linaonesha kuwa Mungu ni Allah au Allah ni Mungu?
Mungu alijifunua kwa mara ya kwanza kwene uzao wa Israel (mlolongo uliowaleta Israel yaan Abraham—Isack —-Yakobo (Israel)——Yesu)
Wakati ALLAH alijifunua kwa waarabu uzao wa mtoto wa nje ya ndoa Ishmael.
Yaan mlolongo ulioleta Waarabu
(Abraham——Ishmael (arabs)——Mtume Muhammad).
Mungu alijifunua miaka mingi kabla ya kuja kwa Yesu kuja kwamba miaka mingi kabla (2000+ nyuma).
Allah miaka 600 baadaa ya kuja Yesu au alikuja miaka zaidi ya mingi baada ya kujifunua Mungu wa kwanza.
Mungu anajua kila lugha huitaji kutumia Lugha ya sehemu alipojifunua kwa mara ya kwanza ndio uwasiliane yeye hata kwa lugha yako ya asili anaijua
Allah ye anajua kiarabu Lugha nyingine hazijui,Hivo inabidi watu wajifunze kiarabu ndio wawasiliane nae hata jina lake Haliruhusiwi kuitwa kwa Lugha nyingine isipo kua kiarabu.
Kwanini hawa wawili wawe ni wamoja?
NB: Ni suali la uelewa tu sina maana mbaya ndugu zangu.
Mtahangaika sana ila hakuna mtu anayeweza kupinga utume wa Mtume Muhammad labda awe kilaza kama wewe
Habakuki 3:3
Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.
Isaya 21:13
Ufunuo juu ya Arabuni. Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala, Enyi misafara ya Wadedani.
Isaya 21:14
Waleteeni wenye kiu maji, Enyi wenyeji wa nchi ya Tema; Nendeni kuwalaki wakimbiao na chakula chao.
Mwanzo 25:13
Na haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, kwa majina yao, na kwa vizazi vyao. Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, ni Nebayothi, na Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu,
Mwanzo 25:14
na Mishma, na Duma, na Masa,
Mwanzo 25:15
na Hadadi, na Tema, na Yeturi, na Nafishi, na Kedema.
Tema ni jina la mtoto wa nabii Ishmael baadae likawa jina mji ambayo ndio Saudi Arabia ya sasa
Nakuwekea ramani ya kale ya bibilia kukuonyesha huo mji wa Tema
Nakuwekea na ramani ya Sasa ya Saudi Arabia kuonyesha huo mji wa Tema Hadi Leo bado upo
Hayo ni mandiko ambayo yamo ndani ya bibilia yaliyokuwa yanatabiri ujio wa Mtume Muhammad katika nchi ya Saudi Arabia kupitia uzao wa Ishmael