MUNGU ni mmoja tu, hana mtoto, hakuzaa wala hakizaliwa wala hafanani na yeyote yule

MUNGU ni mmoja tu, hana mtoto, hakuzaa wala hakizaliwa wala hafanani na yeyote yule

Alijibu vipi kuhusu hoja za hao jamaa wa 1440
Quran 83:10-17

"Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha!

Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.

Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi.

Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale!

Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma.

Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi.

Kisha wataingia Motoni!

Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha"
 
Hakuna kitu kinaitwa Mungu bila uthibitisho zaidi ya upumbavu tunaojitwika tu
Quran 6:31

" Hakika wamepata hasara walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, mpaka ilipo wajia Saa (KIFO) kwa ghafla, wakasema: Ole wetu kwa tuliyo yapuuza! Nao watabeba mizigo yao juu ya migongo yao. Ni maovu hayo wanayo yabeba."
 
Sawa
 
Umejuaje au kwa nini hayo unayoamini wewe ndio imani sahihi ya mungu??
Hayatoshi macho yako kukuonesha kuwa haya yote unayoyaona hapa duniani yameumbwa na Mungu mmoja! Toka nje usiku huu utazame mbingu,nyota na mwezi...kisha ujiulize ni nani aliyaviumba hivi vyote...Je vimetokea tu kwa bahati mbaya (random chances) au yupo aliyevipangilia?
 
hakuna hasara kubwa kama hasara hiyo maana baada ya pumzi kukata hakuna tena second chance ya kurudi duniani kurekebisha yale ambayo ulishindwa kuyarekebisha ulipopewa umri wa kuishi.
Nawajua kafie mbali gademitt
 
Watz mkishiba mihogo kahawa na bagia mnakuja kujadili udini. Wakati mna maisha magumu umasikini hadi matakoni na bado mna majini yanawasumbua. Huo muda si mngekaa vibalazani mjadili namna ya kupata pesa
 
Kwanini hakuzuia dhambi isiingie? Kwanini asimteketeze sasa anasuburi watu wake wapate dhambi ili nao awachome? Wewe unaweza acha mwanao afanye kosa unaloweza kumzuia ili umchape bakora milele?
Quran 11:7

"Na Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji, ili akufanyieni mtihani ajuulikane ni nani miongoni mwenu mzuri zaidi wa vitendo. Na wewe ukisema: Nyinyi hakika mtafufuliwa baada ya kufa; wale walio kufuru husema: Hayakuwa haya ila ni uchawi uliyo wazi."

Dhumuni la sisi kuumbwa na Mungu na kuletwa hapa duniani ni kujaribiwa. Mungu ametuumba ili atujaribu kuona ni kina nani watamuamini na kutenda matendo mema na nani watakufuru...kisha mwisho ameweka malipo kwa kila watu...Kama ulimuamini na ukatenda mema atakuzawadia PEPO na kama ulimkufuru n ukatenda maovu pia atakuzawadia MOTO.

kumbuka kuwa Mungu hapangiwi wala haulizwi katika maamuzi yake..Yeye aliamua iwe hivyo na imekuwa hivyo...Na kubwa la zaidi Mungu hamdhulumu mja wake bali mja anajidhulumu yeye mwenyewe.

mfano..Ametuumba sote na kutuleta duniani hali ya kuwa hatujui chochote ila ametupa kila kitu kutuwezesha kuishi na kukua, ametupa na elimu na pia alichagua baadhi ya watu kuwa ni Mitume na Manabii ili wapokee maelekezo kutoka kwake ambayo yatatuwezesha sisi wengine tuweze kuongoka...Bado akaleta na Vitabu vyake kama Taurat,Zaburi ,Injili na Quran ili viwe ni muongozo kwa wanadamu...!

Sasa hapa ukichagua njia ya upotovu,sidhani kama utakuwa na hoja siku ya hukumu...!! Mungu hatakuwa amekudhulumu bali umeidhulumu nafsi yako mwenyewe kwa kuchagua upotovu badala ya uongofu.
 
Hii ndiyo imani sahihi juu ya Mungu.

Yeyote mwenye kudai kuwa Mungu yupo zaidi ya mmoja huyo ni Mshirikina.

Yeyote mwenye kudai Mungu ana mwana (Mtoto) ,jua kuwa huyo mtu amelaaniwa na amemkufuru Mungu.

Yeyote mwenye kudai Mungu amefanana na kiumbe au kitu chochote kile ,jua huyo mtu amemkufuru Mungu.

Ndugu zangu hapa duniani tunaishi mara moja tu....tunakufa na jua kuwa tutafufuliwa na kwenda kuulizwa juu ya imani tulizokuwa nazo na kuzifuata hapa duniani.

Vp utakufa hali ya kuwa ulifuata imani inayosema kuwa Mungu yupo zaidi ya mmoja na amezaa mtoto? au amezaliwa na Mwanamke?

Kumbuka kuwa hakuna chance mbili...!! Tukiipoteza hii nafasi jua huko tuendapo kuna PEPO (paradise) na MOTO (Hellfire). Na huko hakuna kufa ...Kama utaingia Peponi jua utadumu humo milele na kama utakuwa umekufuru na kuingia Motoni jua pia humo utadumu na kuishi milele ukitumikia adhabu kali kutoka kwa Mungu.
Wewe umeumbwa na, Mungu, umeweza kupata watoto, ila aliyekuumba Hana uwezo wa, kupata mtoto! Surely!!
 
Watz mkishiba mihogo kahawa na bagia mnakuja kujadili udini. Wakati mna maisha magumu umasikini hadi matakoni na bado mna majini yanawasumbua. Huo muda si mngekaa vibalazani mjadili namna ya kupata pesa
Quran 87:17-18

"Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia! Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi."

Siku moja jitahidi ufanye ziara kutembelea makaburini halafu usome vile vibao kuonesha wale waliolala pale wameishi muda gani na je ni nani kati yao aliyezikwa na mali yake"
 
Hayatoshi macho yako kukuonesha kuwa haya yote unayoyaona hapa duniani yameumbwa na Mungu mmoja! Toka nje usiku huu utazame mbingu,nyota na mwezi...kisha ujiulize ni nani aliyaviumba hivi vyote...Je vimetokea tu kwa bahati mbaya (random chances) au yupo aliyevipangilia?
Kila siku natazama anga sio "mbingu", nyota na mwezi ila sijawahi kupata jibu la uthibitisho kama vimeumbwa au vimetokea tu na kama vimeumbwa nani ameviumba ( ila najua asilimia kubwa ya watu duniani wamekuwa "wanaamini" kwa Imani tu kwamba vimeumbwa bila uthibitisho wowote)

Pia nikiangalia naona masikini wanaoteseka, watu wanaugua magonjwa ya kutisha, vilema wa kuzaliwa na wa ajali, vichaa, watu dhaifu wanadhulimiwa na wenye nguvu na mamlaka, vita, vimbunga na matetemeko nashindwa kujua kwa nini kama kuna muumbaji mwenye nguvu hivyo ameruhusu na haya pia kutokea!
 
Wewe umeumbwa na, Mungu, umeweza kupata watoto, ila aliyekuumba Hana uwezo wa, kupata mtoto! Surely!!
kuzaa na kuzaliwa ni sifa za udhaifu...Mungu ametakasika juu ya kila sifa yenye upungufu.

Ndio maana sisi viumbe tunalala, tunachoka, tunakula, tunakwenda haja n.k ila yeye hahitaji hayo..masna yeye ni mkamilifu na mtakatifu
 
Wapumbavu nyie, mnaitukuza quran yenu na kuiamini ni ya mungu, acheni na wengine waamini kuwa Mungu ana mtoto ndivyo wanavyoona ni imani yao. Nyie inawauma nini watu wengine kuamini Mungu ana mtoto?
 
Quran 6:31

" Hakika wamepata hasara walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, mpaka ilipo wajia Saa (KIFO) kwa ghafla, wakasema: Ole wetu kwa tuliyo yapuuza! Nao watabeba mizigo yao juu ya migongo yao. Ni maovu hayo wanayo yabeba."
Wamepata hasara gani?
 
Wapumbavu nyie, mnaitukuza quran yenu na kuiamini ni ya mungu, acheni na wengine waamini kuwa Mungu ana mtoto ndivyo wanavyoona ni imani yao. Nyie inawauma nini watu wengine kuamini Mungu ana mtoto?
Hili ni tatizo la hizi dina tatu za Abrahamic, kila moja inaona yenyewe ndio sahihi na wengine wote wamepotea na hamnazo.
 
Kila siku natazama anga sio "mbingu", nyota na mwezi ila sijawahi kupata jibu la uthibitisho kama vimeumbwa au vimetokea tu na kama vimeumbwa nani ameviumba ( ila najua asilimia kubwa ya watu duniani wamekuwa "wanaamini" kwa Imani tu kwamba vimeumbwa bila uthibitisho wowote)

Pia nikiangalia naona masikini wanaoteseka, watu wanaugua magonjwa ya kutisha, vilema wa kuzaliwa na wa ajali, vichaa, watu dhaifu wanadhulimiwa na wenye nguvu na mamlaka, vita, vimbunga na matetemeko nashindwa kujua kwa nini kama kuna muumbaji mwenye nguvu hivyo ameruhusu na haya pia kutokea!
Quran 29:2-7

" Je! Wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe?

Hakika tuliwajaribu walio kuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na atawatambulisha walio waongo

Au wanadhani wanao tenda maovu kwamba watatushinda (watatuponyoka)? Hukumu mbaya hiyo wanayo hukumu.

Mwenye kutaraji kukutana na Mwenyezi Mungu, basi hakika miadi ya Mwenyezi Mungu itafika bila ya shaka. Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua

Na anaye fanya juhudi basi bila ya shaka anafanya juhudi kwa ajili ya nafsi yake. Hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji wa walimwengu.

Na walio amini na wakatenda mema, kwa yakini tutawafutia makosa yao, na tutawalipa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.
 
Back
Top Bottom