Naamini kuwa asilimia kubwa ya wanaadamu wanaishi hapa duniani wakiwa hawajui dhumuni la kwanini wameletwa hapa duniani.
Wengi wanaishi kama wanyama tu, kwa kula,kunywa , kuzaana na mwisho kufa.
Yaani kula,kunywa,kuzaana,kutafuta mali na mwisho kufa ndio watu wengi hudhani wameumbwa kwa ajili ya hayo.
Ila kamaa utakuwa ni deep thinker ukautazama huu ulimwengu kwa jicho la tafakari ni lazima utajua kuwa hatukuumbwa na kuletwa hapa duniani bure. Lazima kuwe na lengo maalumu..!
Hapa ndipo safari ya kumtafuta yule aliyetuumba inapoanza. Lazima tumjue huyu aliyeweka huu mfumo wa ulimwengu kwa tunaamka asubuhi tunaona jua limechomoza, jioni ikifika jua linazama, mwezi unachomoza tunapata kupumzika baada ya mihangaiko ya mchana kutwa. Mara tunaona mvua inanyesha, upepo unapuliza, mawingu yanakwenda...mimea inakua...!!
Hii system imejengwa na nani? Je imetokea tu kwa bahati mbaya??