Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 4,994
- 9,625
- Thread starter
- #61
1-Mungu ukidai kazaliwa ni lazima utueleze hiki kipindi cha miezi 9 wakati yupo tumboni kwa mwanamke, je ni nani aliyekuwa akiuendesha ulimwengu? Nani aliyekuwa akizishikilia mbingu zisidongoke,nani aliyekuwa akilitoa jua mashariki kwenda magharibi, nani aliyekuwa akisimamia mifumo ya mvua, nani aliyekuwa akigawa riziki??1. Una uthibitisho gani kwamba vyote vilivyozaliwa havikuwepo kabla? Mungu kama ana nguvu zote hawezi kugeuka kiumbe cha kuzaliwa?
2. Una uthibitisho gani chochote kinachozaliwa lazima kiwe na mwisho? Mbona Wahindu wanaamini hakuna mwisho wa viumbe hai vinavyozaliwa bali vinabadilika tu kutoka kiumbe kimoja kwenda kingine? (reincarnation)
3. Mbona Muhammad anasema Issa alizaliwa akiwa anaongea?
Kama uliwezekana huo muujiza vipi unasema Issa alikuwa mdhaifu?
4. Yesu ni mwana pekee wa mungu, hakuendelea kuzaa watoto wengine. Pia kwa nini unafikiri mungu haitaji kuzaa? Mbona Wagiriki, Warumi na Wamisri wa kale hawakuwa na tatizo lolote kabisa miungu yao kuzaa na kuwa na watoto?!
Kwa nini unafikiri dhana yako ya mungu asiye zaa na asiyekuwa na udhaifu ndio kweli na nyingine sio kweli??
2- Kinachozaliwa huwa kina mwisho. Uhai na kifo ni vitu viwili vinavyofuatana katika ulimwengu huu....Hiyo ya wahindi reincarnation ni dhana tu na dhana haina haki yoyote.
Quran 53:28
" Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki."
3-Issa (Yesu) mwana wa Mariam licha ya kupewa huu muujiza wa kuongea hali ya kuwa ni mtoto mchanga..bado alikuwa ni mdhaifu kwa maana ya kwamba alinyonya maziwa ya mama yake, alihitaji kulishwa,kuogeshwa,kuvalishwa,kubebwa n.k ...udhaifu kwa maana hakuwa akijiweza kwa lolote pindi alipokuwa mtoto mchanga. Je huoni kama huo ni udhaifu?
4- Labda unaweza kutaja hiyo miungu ya kigiriki na watoto wao walikuwaje na walikuwa wakifanaje ili tupate kujadili vizuri...
Yesu hakuzaa...ila alizaliwa
Kwahiyo leo hii Wanaume wasiokuwaa na uwezo wa kuzalisha au wanawake wasiokuwa na uwezo wa kubeba mimba nao tuwaite kuwa ni MIUNGU?