MUNGU ni mmoja tu, hana mtoto, hakuzaa wala hakizaliwa wala hafanani na yeyote yule

MUNGU ni mmoja tu, hana mtoto, hakuzaa wala hakizaliwa wala hafanani na yeyote yule

Quran imeokoteza mafungu mengi toka kwenye biblia, halafu watu wakahadaiwa kuwa eti imeshushwa na Mungu.
 
Hii ndiyo imani sahihi juu ya Mungu.

Yeyote mwenye kudai kuwa Mungu yupo zaidi ya mmoja huyo ni Mshirikina.

Yeyote mwenye kudai Mungu ana mwana (Mtoto) ,jua kuwa huyo mtu amelaaniwa na amemkufuru Mungu.

Yeyote mwenye kudai Mungu amefanana na kiumbe au kitu chochote kile ,jua huyo mtu amemkufuru Mungu.

Ndugu zangu hapa duniani tunaishi mara moja tu....tunakufa na jua kuwa tutafufuliwa na kwenda kuulizwa juu ya imani tulizokuwa nazo na kuzifuata hapa duniani.

Vp utakufa hali ya kuwa ulifuata imani inayosema kuwa Mungu yupo zaidi ya mmoja na amezaa mtoto? au amezaliwa na Mwanamke?

Kumbuka kuwa hakuna chance mbili...!! Tukiipoteza hii nafasi jua huko tuendapo kuna PEPO (paradise) na MOTO (Hellfire). Na huko hakuna kufa ...Kama utaingia Peponi jua utadumu humo milele na kama utakuwa umekufuru na kuingia Motoni jua pia humo utadumu na kuishi milele ukitumikia adhabu kali kutoka kwa Mungu.
SWALI LA KIJINGAJINGA.
Ulikutana naye/ulimuona wapi hadi umjibie hoja zake?
 
Watu wanauliza mambo yasiyo na maana. Kitu wasichokijua wajinga wa neno la Mungu, ni kuwa Yesu pekee hakuwahi kunena kuwa ni Mungu. Yesu katika mwili, alifanywa kuwa mwanadamu, ndiyo maana wanadamu waliweza kumwona, kumshika, kumtesa na kumwua, sawa na anavyoweza kufanyiwa mwanadamu. Lakini Yesu katika ukamilifu wa Mungu, hakuna wa kumfikia, kumgusa wala kumtenda lolote. Ndiyo maana alipofufuka, kabla ya kupaa mbinguni, alisema, "Baba nirudishie ule utukufu niliokuwa nao PAMOJA nawe, mara akanyuka juu, wingu likamfunika, kundi la malaika likashuka, na sauti ikasikika, "enyi watu wa Galilaya, mbona mnatazama juu mbinguni, huyu Yesu mliyemwona akipaa mbinguni, atarudi kwa jinsi hiyo hiyo siku ya mwisho".

Kama mngejaliwa hekima hata ndogo sana, mngejua kuwa Mungu ambaye ana uwezo wa kila kitu, Mungu mwenye uwezo wa kuwepo kila mahali, hashindwi kufanya chochote, hashindwi kutokea katika namna yoyote aitakayo. Lakini Mungu ni yule yule, jana, leo, kesho, na hata milele. Kama ndivyo, ni nini kitamshinda kumtengeneza mwanadamu, na ndani yake, kupitia yeye akaiweka nguvu yake. Kabla yake Mungu aliweza kutokea katika namna ya wingu, moto, na hata sauti isiyoonekana inakotoka.
Waislam, na kitabu chao kilichojaa chuki, sijui kwa nini wanapoteza muda wao dhidi ya imani ya Kikristo, wakati wakristo hawana muda na huo uislam. Sijui kwa nini wislam wanapenda kujifananisha na wakristo, wakati ni imani 2 zilizo tofauti. Waislam wanaamini kuwa Allah ni bingwa wa hadaa, na ni mfalme wa Ulimwengu. Wakristo, kwa kadiri ya mafundisho ya Kristo Yesu, Ibilisi/shetani ni bingwa wa hadaa, mfalme wa Ulimwengu, amewahadaa wengi ili waangamie.
Waislam wanaamini katika kisasi, wakati wakristo wanaamini katika upendo na msamaha.
Kwa nini waislam wasitulie, wakaacha kujihangaisha na kujilinganisha na ukristo wasiouamini? Wakafanya sawa na namna kama wafanyavyo wakristo kutojishughulisha na uislam?
 
Maswali yasiyo na maana kabisa. Huu ndiyo uthibitisho wa neno la Mungu kuwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.

Mafundisho mengi ya dini ya kiislam yamejaa uwongo mwingi wa wazi:
1. Wanawadanganya watu eti quran ilishushwa na Mungu wakati iliandikwa na wanadamu. Mpaka Mohamad anakufa hakuacha quran.
2. Muhamad kwa maneno yake ni kuwa akiwa pangoni alitokewa na shetani. Ambao hawakuwepo pangoni wakasema alitokewa na malaika Jibril.

Kwa ujumla uislam ulianzishwa kwaajili ya harakati za kivita kushindana na wayahudi, ili kuwapa hamasa wapiganaji, ndiyo maana vipengere vingi ndani ya quran, vinahamasisha mauaji kwa wasio waislam.
1-Mtume Muhammad (pbuh) wakati anafariki aliiacha Quran ikiwa imehifadhiwa ktk vifua vya wanafunzi wake, pia ilikuwa ikinakiliwa ktk ngozi,mawe n.k alipofariki waislam wakaamua waikusanye ktk mfumo wa kitabu kimoja ili ihifadhiwe na vizazi vijavyo.

2-Kama Shetani ndio muasisi wa Uislam, inakuwaje Quran inamlaani na kumsema vibaya shetani?
 
Quran imeokoteza mafungu mengi toka kwenye biblia, halafu watu wakahadaiwa kuwa eti imeshushwa na Mungu.
kama Quran imekopi biblia, Je kwanini Quran imekemea vikali imani na misingi ya ukristo?

Quran imekemea juu ya kauli ya utatu mtakatifu,

Quran imekataa Uungu na umwana wa mungu wa Yesu.

Quran imeharamisha nguruwe,

Quran imekataa utume wa Paulo .

Quran imekataa dhana ya kuwa Yesu aliuliwa na kusulubiwa msalabani.

na mengine mengi
 
hakuna hasara kubwa kama hasara hiyo maana baada ya pumzi kukata hakuna tena second chance ya kurudi duniani kurekebisha yale ambayo ulishindwa kuyarekebisha ulipopewa umri wa kuishi.
Fear of the unknown mzee!
Wakati mwingine huwa nawaza kwamba huenda sisi ni ma mifugo ya huyu Mungu
 
Hakuna kitu kinaitwa Mungu bila uthibitisho zaidi ya upumbavu tunaojitwika tu
Bwashee ww umejiumba? Ata iyo simu unotumia imetengenezwa na binadamu ambae hata humjui kwanini ukatae kua hakuna Muumba ?
 
Watu waliopita kabla yako walidai kama haya unayoyadai wewe leo hii ila Mungu aliwajibu hivi

Quran 6:8

"Na wao husema: Mbona hakuteremshiwa Malaika? Na kama "tungeli teremsha Malaika", basi bila ya shaka ingesha hukumiwa amri, tena hapo wasingeli pewa muhula."
Umeshawahi kutumia akili yako kwenye mambo ya Imani? Ukitumia akili yako utaelewa nini maana ya maneno yaliyopigiwa mstari.
Unaelewa maana ya maneno "Kama tungeliteremsha"
 
1-Mungu ukidai kazaliwa ni lazima utueleze hiki kipindi cha miezi 9 wakati yupo tumboni kwa mwanamke, je ni nani aliyekuwa akiuendesha ulimwengu? Nani aliyekuwa akizishikilia mbingu zisidongoke,nani aliyekuwa akilitoa jua mashariki kwenda magharibi, nani aliyekuwa akisimamia mifumo ya mvua, nani aliyekuwa akigawa riziki??

2- Kinachozaliwa huwa kina mwisho. Uhai na kifo ni vitu viwili vinavyofuatana katika ulimwengu huu....Hiyo ya wahindi reincarnation ni dhana tu na dhana haina haki yoyote.

Quran 53:28
" Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki."

3-Issa (Yesu) mwana wa Mariam licha ya kupewa huu muujiza wa kuongea hali ya kuwa ni mtoto mchanga..bado alikuwa ni mdhaifu kwa maana ya kwamba alinyonya maziwa ya mama yake, alihitaji kulishwa,kuogeshwa,kuvalishwa,kubebwa n.k ...udhaifu kwa maana hakuwa akijiweza kwa lolote pindi alipokuwa mtoto mchanga. Je huoni kama huo ni udhaifu?

4- Labda unaweza kutaja hiyo miungu ya kigiriki na watoto wao walikuwaje na walikuwa wakifanaje ili tupate kujadili vizuri...

Yesu hakuzaa...ila alizaliwa

Kwahiyo leo hii Wanaume wasiokuwaa na uwezo wa kuzalisha au wanawake wasiokuwa na uwezo wa kubeba mimba nao tuwaite kuwa ni MIUNGU?
Inaonekana Mungu unayemuabudu anauwezo mdogo sana na Yuko limited kufanya baadhi ya mambo!
Mungu ninayemuabudu ana uwezo wa kujifanyia mwana kwa neno tu na kwa namna atakayo!
 
Inaonekana Mungu unayemuabudu anauwezo mdogo sana na Yuko limited kufanya baadhi ya mambo!
Mungu ninayemuabudu ana uwezo wa kujifanyia mwana kwa neno tu na kwa namna atakayo!
Mungu sio cartoon... Yaani kajifanya mwana ili akae tumboni kwa miezi 9 ili apate kuja kuuliwa na viumbe wake ili aweze kuwasamehe viumbe wake aliyewaumba....? Hii ni blasphemy
 
Umeshawahi kutumia akili yako kwenye mambo ya Imani? Ukitumia akili yako utaelewa nini maana ya maneno yaliyopigiwa mstari.
Unaelewa maana ya maneno "Kama tungeliteremsha"
wewe ndio ueleze shida yako ni ipi?
 
Hii ndiyo imani sahihi juu ya Mungu.

Yeyote mwenye kudai kuwa Mungu yupo zaidi ya mmoja huyo ni Mshirikina.

Yeyote mwenye kudai Mungu ana mwana (Mtoto) ,jua kuwa huyo mtu amelaaniwa na amemkufuru Mungu.

Yeyote mwenye kudai Mungu amefanana na kiumbe au kitu chochote kile ,jua huyo mtu amemkufuru Mungu.

Ndugu zangu hapa duniani tunaishi mara moja tu....tunakufa na jua kuwa tutafufuliwa na kwenda kuulizwa juu ya imani tulizokuwa nazo na kuzifuata hapa duniani.

Vp utakufa hali ya kuwa ulifuata imani inayosema kuwa Mungu yupo zaidi ya mmoja na amezaa mtoto? au amezaliwa na Mwanamke?

Kumbuka kuwa hakuna chance mbili...!! Tukiipoteza hii nafasi jua huko tuendapo kuna PEPO (paradise) na MOTO (Hellfire). Na huko hakuna kufa ...Kama utaingia Peponi jua utadumu humo milele na kama utakuwa umekufuru na kuingia Motoni jua pia humo utadumu na kuishi milele ukitumikia adhabu kali kutoka kwa Mungu.
UONGO.

HAKUNA KUISHI MILELE MOTONI,BALI KIFO CHA MILELE.

HALAFU,MUNGU AKIFANANA NA CHOCHOTE AU AKAFANANA NA MWANADAMU KUNA SHIDA GANI?

SI NI MUNGU,NA HAYO LABDA YAKAWA MAAMUZI YAKE AFANANE NA WANADAMU,KUNA SHIDA?
 
Mungu sio cartoon... Yaani kajifanya mwana ili akae tumboni kwa miezi 9 ili apate kuja kuuliwa na viumbe wake ili aweze kuwasamehe viumbe wake aliyewaumba....? Hii ni blasphemy
Mungu muweza wa yote ana uwezo wa kufanya atakavyo!
 
UONGO.

HAKUNA KUISHI MILELE MOTONI,BALI KIFO CHA MILELE.

HALAFU,MUNGU AKIFANANA NA CHOCHOTE AU AKAFANANA NA MWANADAMU KUNA SHIDA GANI?

SI NI MUNGU,NA HAYO LABDA YAKAWA MAAMUZI YAKE AFANANE NA WANADAMU,KUNA SHIDA?
Quran 4:56

"Hakika wale walio zikataa Ishara zetu tutawaingiza Motoni. Kila zitapo wiva ngozi zao tutawabadilishia ngozi nyengine ili waionje hiyo adhabu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima."
 
Mungu muweza wa yote ana uwezo wa kufanya atakavyo!
Hesabu 23:19
Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalitimiza?


kupitia andiko hilo hapo juu tunaona kuwa Mungu hawezi kuwa Mtu, Mungu hawezi kuwa binadamu, Mungu hawezi kusema uongo. Mungu havunji ahadi.


So kuna mambo Mungu amejiamulia kutokuyatenda au kuyafanya kutokana na utakatifu wake.
 
Quran 4:56

"Hakika wale walio zikataa Ishara zetu tutawaingiza Motoni. Kila zitapo wiva ngozi zao tutawabadilishia ngozi nyengine ili waionje hiyo adhabu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima."
HAKUNA MUNGU WA HIVI;

NASEMA TENA,HUU NI UONGO.

WEWE UNAONA HEKIMA KWENYE HICHO KITENDO?

HALAFU NANI AMEKUHAKIKISHIA KUWA QURANI NI KITABU KILICHO NA MANENO YA UZIMA?
 
Quran 2:2
" Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu,"


Quran 3:2-4

" Mwenyezi Mungu, hakuna mungu ila Yeye Aliye Hai, Msimamizi wa yote milele. Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili, Kabla yake, ziwe uwongofu kwa watu. Na akateremsha Furqani (Upambanuo). Hakika walio zikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu watakuwa na adhabu kali. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye kulipa."
Swali ni umejuaje kwamba alie teremsha ni yeye wakati umeshasema hafanani na kitu chochote. Ulitumia kipimo gani kupima hayo ma andiko na kusema kwamba yametoka kwa Mungu ambae hajulikani yukoje na anafananaje?

LIKUD
 
Hesabu 23:19
Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalitimiza?


kupitia andiko hilo hapo juu tunaona kuwa Mungu hawezi kuwa Mtu, Mungu hawezi kuwa binadamu, Mungu hawezi kusema uongo. Mungu havunji ahadi.


So kuna mambo Mungu amejiamulia kutokuyatenda au kuyafanya kutokana na utakatifu wake.
Kwamba Mungu Yuko limited hawezi fanya atakavyo?
 
Back
Top Bottom