MUNGU ni mmoja tu, hana mtoto, hakuzaa wala hakizaliwa wala hafanani na yeyote yule

MUNGU ni mmoja tu, hana mtoto, hakuzaa wala hakizaliwa wala hafanani na yeyote yule

Swali ni umejuaje kwamba alie teremsha ni yeye wakati umeshasema hafanani na kitu chochote. Ulitumia kipimo gani kupima hayo ma andiko na kusema kwamba yametoka kwa Mungu ambae hajulikani yukoje na anafananaje?

LIKUD
Mungu ameiteremsha Quran kuja kwa Mtume Muhammad (pbuh) kwa kupitia Malaika Gabriel aka Jibril
 
Hii ndiyo imani sahihi juu ya Mungu.

Yeyote mwenye kudai kuwa Mungu yupo zaidi ya mmoja huyo ni Mshirikina.

Yeyote mwenye kudai Mungu ana mwana (Mtoto) ,jua kuwa huyo mtu amelaaniwa na amemkufuru Mungu.

Yeyote mwenye kudai Mungu amefanana na kiumbe au kitu chochote kile ,jua huyo mtu amemkufuru Mungu.

Ndugu zangu hapa duniani tunaishi mara moja tu....tunakufa na jua kuwa tutafufuliwa na kwenda kuulizwa juu ya imani tulizokuwa nazo na kuzifuata hapa duniani.

Vp utakufa hali ya kuwa ulifuata imani inayosema kuwa Mungu yupo zaidi ya mmoja na amezaa mtoto? au amezaliwa na Mwanamke?

Kumbuka kuwa hakuna chance mbili...!! Tukiipoteza hii nafasi jua huko tuendapo kuna PEPO (paradise) na MOTO (Hellfire). Na huko hakuna kufa ...Kama utaingia Peponi jua utadumu humo milele na kama utakuwa umekufuru na kuingia Motoni jua pia humo utadumu na kuishi milele ukitumikia adhabu kali kutoka kwa Mungu.


So God used alphabets invented by man to name his Angles in heaven.

Isn't it concerning??
 
Quran 11:7

"Na Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji, ili akufanyieni mtihani ajuulikane ni nani miongoni mwenu mzuri zaidi wa vitendo. Na wewe ukisema: Nyinyi hakika mtafufuliwa baada ya kufa; wale walio kufuru husema: Hayakuwa haya ila ni uchawi uliyo wazi."

Dhumuni la sisi kuumbwa na Mungu na kuletwa hapa duniani ni kujaribiwa. Mungu ametuumba ili atujaribu kuona ni kina nani watamuamini na kutenda matendo mema na nani watakufuru...kisha mwisho ameweka malipo kwa kila watu...Kama ulimuamini na ukatenda mema atakuzawadia PEPO na kama ulimkufuru n ukatenda maovu pia atakuzawadia MOTO.

kumbuka kuwa Mungu hapangiwi wala haulizwi katika maamuzi yake..Yeye aliamua iwe hivyo na imekuwa hivyo...Na kubwa la zaidi Mungu hamdhulumu mja wake bali mja anajidhulumu yeye mwenyewe.

mfano..Ametuumba sote na kutuleta duniani hali ya kuwa hatujui chochote ila ametupa kila kitu kutuwezesha kuishi na kukua, ametupa na elimu na pia alichagua baadhi ya watu kuwa ni Mitume na Manabii ili wapokee maelekezo kutoka kwake ambayo yatatuwezesha sisi wengine tuweze kuongoka...Bado akaleta na Vitabu vyake kama Taurat,Zaburi ,Injili na Quran ili viwe ni muongozo kwa wanadamu...!

Sasa hapa ukichagua njia ya upotovu,sidhani kama utakuwa na hoja siku ya hukumu...!! Mungu hatakuwa amekudhulumu bali umeidhulumu nafsi yako mwenyewe kwa kuchagua upotovu badala ya uongofu.
Mungu mnayedai kwamba anajua kila kitu tangu mwanzo na hata milele, anakupima na kukujaribu ili agundue nini asichokijua?
 
Mbona Allah ana mitoto mitatu lakini leo hataki waja wajue kama ni mitoto yake,mitoto hiyo ni l-Lat, Al-Uzza, and Manat
 
Hii ndiyo imani sahihi juu ya Mungu.

Yeyote mwenye kudai kuwa Mungu yupo zaidi ya mmoja huyo ni Mshirikina.

Yeyote mwenye kudai Mungu ana mwana (Mtoto) ,jua kuwa huyo mtu amelaaniwa na amemkufuru Mungu.

Yeyote mwenye kudai Mungu amefanana na kiumbe au kitu chochote kile ,jua huyo mtu amemkufuru Mungu.

Ndugu zangu hapa duniani tunaishi mara moja tu....tunakufa na jua kuwa tutafufuliwa na kwenda kuulizwa juu ya imani tulizokuwa nazo na kuzifuata hapa duniani.

Vp utakufa hali ya kuwa ulifuata imani inayosema kuwa Mungu yupo zaidi ya mmoja na amezaa mtoto? au amezaliwa na Mwanamke?

Kumbuka kuwa hakuna chance mbili...!! Tukiipoteza hii nafasi jua huko tuendapo kuna PEPO (paradise) na MOTO (Hellfire). Na huko hakuna kufa ...Kama utaingia Peponi jua utadumu humo milele na kama utakuwa umekufuru na kuingia Motoni jua pia humo utadumu na kuishi milele ukitumikia adhabu kali kutoka kwa Mungu.
Hata huyo Mungu mmoja umetoa story ya imani tu.

Hujathibitisha kuwa kweli yupo.
 
Nenda leo hii kakojolee geti la ikulu au kituo cha polisi au mahakama ya serikali...utapata majibu kama watakupa maua au vp?

Kuhusu kumuadhibu mtoto labda kama wewe ndio huadhibu wanao, sinui unajenga kizazi chenye maadili gani? Ila kwa mimi nawaadhibu wanangu kwa lengo la kuwafundisha adabu ,maadili na nidhamu.

Kwahiyo Mungu hakuwa na uwezo wa kuzuia uwepo wa dhambi na 'shetani'? Kama alikua nao kwanini hakufanya hivyo in the first place? Kama hakuwa nao ina maana nguvu zake zipo limited tofauti na story zenu za kusadikika.
 
Huyo Mungu alishindwaje kuumba Dunia isiyo na dhambi?

Hivi huyo Mungu wenu anajielewa kweli?
Bado muda unao wa kuendelea kuamini uwepo wa Muumbaji!

Wewe siyo wa kwanza kukataa uwepo wa Mungu,mpo wengi mno kwenye msafara,Hivyo fursa ya uhai pekee ulio nao leo si kwa ajili ya kukataa uwepo wake bali ni umepewa neema ya kujifunza kupitia kazi ya mikono yake ili uamini uwepo wake!
 
Kwahiyo Mungu hakuwa na uwezo wa kuzuia uwepo wa dhambi na 'shetani'? Kama alikua nao kwanini hakufanya hivyo in the first place? Kama hakuwa nao ina maana nguvu zake zipo limited tofauti na story zenu za kusadikika.
aliamua vyote viwepo..Yeye ndiye muumbaji, hapangiwi hata akiamua kutuchoma moto wote bado sisi ni wake...hata akiamua kutupa maisha ya raha peponi wote ni wake....So wewe kiumbe huna haki yoyote ya kumuhoji mfalme wa ulimwengu.
 
Hata huyo Mungu mmoja umetoa story ya imani tu.

Hujathibitisha kuwa kweli yupo.
mzee wa ligi umekuja...ni hivi wewe siwezi kukupa uthibitisho wowote...ukiamua amini, imani yako itakufaa baada ya kufa kwako au ukiamua pia puuza ili uende kujutia baada ya kufa.

Lengo langu ni kufikisha ujumbe wa Mungu na wala si kubishana..!! Ukiamua amini na ukiamua pia kufuru..Mungu ndiye mwenye kuongoza waja wake

Salama
 
Bado muda unao wa kuendelea kuamini uwepo wa Muumbaji!

Wewe siyo wa kwanza kukataa uwepo wa Mungu,mpo wengi mno kwenye msafara,Hivyo fursa ya uhai pekee ulio nao leo si kwa ajili ya kukataa uwepo wake bali ni umepewa neema ya kujifunza kupitia kazi ya mikono yake ili uamini uwepo wake!
Huyo Mungu anahitaji binadamu wamwamini?
 
mzee wa ligi umekuja...ni hivi wewe siwezi kukupa uthibitisho wowote...ukiamua amini, imani yako itakufaa baada ya kufa kwako au ukiamua pia puuza ili uende kujutia baada ya kufa.

Lengo langu ni kufikisha ujumbe wa Mungu na wala si kubishana..!! Ukiamua amini na ukiamua pia kufuru..Mungu ndiye mwenye kuongoza waja wake

Salama
Hii si habari yangu mimi, umeweka hapa kwa wote.

Hii si habari ya imani tu, imani hata uongo unaweza kuamini.

Lakini je, ukiamini, hicho unachoamini ni kweli?

Hujaonesha hilo.

Mpaka sasa huwezi kuthibitisha imani yako ipo katika ukweli.
 
Huyo Mungu anahitaji binadamu wamwamini?
Hats ulimwengu mzima umkufuru Mungu bado hatumpunguzii wala kumuongezea chochote katika ufalme wake na hata kama wote tutakuwa wachamungu na kumuamini pia hatumuongezei wala kumpunguzia chochote katika ufalme wake .

Ukimuamini Mungu jua ni kwa manufaa ya nafsi yako na ukimkufuru pia ni kwa maangamio ya nafsi yako mwenyewe.

Ila tambua mwisho wa yote kuna mafikio mawili tu PEPO na MOTO...

Utachagua sehemu ipi iwe ni makazi yako ya milele.
 
Watu wa dini ukiwafuatilia kwa ukaribu ni kama wana matatizo ya akili hivi......

Yaani mtu yeye kaamua kuamini jambo lakini anakoseshwa raha na watu ambao hawajaamini jambo ambalo analiamini yeye
 
Watu wa dini ukiwafuatilia kwa ukaribu ni kama wana matatizo ya akili hivi......

Yaani mtu yeye kaamua kuamini jambo lakini anakoseshwa raha na watu ambao hawajaamini jambo ambalo analiamini yeye
Mungu ametuhusia kuwa tufikishe ujumbe kwa watu wote ili siku ya mwisho wakati mmefufuliwa msije na hoja ya kuwa ujumbe wa Mungu haukuwafikia.
 
Back
Top Bottom