Mungu ni mwema kaniokoa na Kifo japo nipo kitandani hospitalini muda huu

Mungu hakupi mtihani isipokuwa ule unaoweza kuumudu na kwenye kila janga kubwa basi kuna janga kubwa zaidi umeepushwa nalo.

Mola akupe ahueni na kupona haraka urudi katika hali yako ya uzima kabisa.

Kumbuka kutoa sadaka kumshukuru Mungu kwa kuokoa na kubwa zaidi na kujikinga na shari.
 
Wakuu Ukisikia zile kauli labda zinaonekana za kukera "TAFUTA PESA" japo kwa sababu zinatumima katika mazingira ya Utani, kejeli, dhihaka au dharau ndio maana zinaonekana kama kelele,

Katika mazingira haya hapa Sasa ndio utaona application yake, imagine ghafla Bin Vuu linakukuta hili ,huna chochote cha kukuungizia pesa wewe ukiwa nje wala Saving yoyote, Ndugu ukute ni wa mchongo, Si utauguza maumivu mara mbili??,

Huyu Asingekua labda na kazi aliyonayo au chochote, Unafika ili usiwasumbue, ni mguu unaenda, haya kwa mpambanaji uliyekua unajitafuta, Si safari imekwisha? Ndio wale Wanaokuja wanaomba misaada ya matibabu kwenye karatasi kutoka Serikalini wanakuambia nilikua mzima ghafla nikapata ajari.
 
Pole
Mshukuru Mungu tu kwakweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…