Mungu wa miujiza mbona sijawahi kumwona? Au kuona miujiza yake?

Mungu wa miujiza mbona sijawahi kumwona? Au kuona miujiza yake?

so huwezi kuanza kusema dini ni universal.
Dhana ya "Universal Religion"

Unaposema dini sio universal, unamaanisha mifumo ya taasisi za kidini. Lakini mimi nilikuambia asili ya dini ni Tawheed (Kuamini Mungu Mmoja). Tangu zamani, hata kabla ya Uislamu au Ukristo kufika kwa jina hilo, jamii nyingi za Kiafrika zilikuwa na imani ya uwepo wa Mungu Mmoja Mkuu (Mfano: Mungu kwa Waswahili, Mulungu, Enkai

kwa Wamasai, Olodumare kwa Wayoruba). Hawakuwa waatheisti (wasiomini Mungu). Huu ndio uthibitisho kuwa kutambua uwepo wa Muumba ni kitu kipo ndani ya Fitrah (asili) ya binadamu.

Qur'ani imetaja jina la waziri wa Farao (Haman) na teknolojia yake ya ujenzi (Baked Clay) ambayo sayansi imegundua karne ya 19 na 20.

Kama unadai vitabu vya dini ni vya kujitungwa tu na binadamu hivi karibuni, nitajie kitabu kimoja tu cha historia kilichoandikwa miaka 1,400 iliyopita jangwani kikajua siri hizi za kiakalojia za Misri ya kale kabla ya sayansi ya kisasa kuzigundua? Nani aliyempa Muhammad taarifa hizi kama sio Muumba wa ulimwengu?"
 
Je, umewahi kuiona hiyo Energy au Vibrations kwa macho yako? Hapana. Unaona matokeo yake tu (effects). Sasa, inakuwaje unakubali kuamini Energy ambayo hujaiona kwa macho kwa sababu tu unaona matokeo yake, lakini unakataa kumwamini Mungu ambaye hujaona dhati yake, ilhali unaona matokeo ya Uhandisi Wake (Macho, ubongo, ulimwengu)? Huku ni kuchagua nini cha kuamini kwa hisia (double standard)
The human body is limited to the spectrum of vision ndo maana tunaona asilimia chache sana ya energy spectrum called the (visible light) ndo maana wanyama wengine tunawazidi na wao wanatuzidi... Kuna viumbe majini vinaona zaidi kuliko wanyama au ndege.

Sio kwamba just because we can't see energy, it does not exist. No, energy exists and can be sensed by good conductors just like radio waves ambazo zina carry signals, na sio kwamba hazi exist zipo na zina rangi zake mahususi ambazo macho yetu ya nyama ambayo yako limited hayawezi kuona.
  1. Energy haina utambuzi (It is blind): Nishati (Energy) haina akili, haina upendo, haina huruma, na haiwezi kuchagua. Nishati ya umeme haiwezi kuandika sheria za kimaadili. Mungu tunayemwabudu sisi ni Al-Alim (Mwenye kujua kila kitu) na Al-Hakim (Mwenye hikima/akili ya juu). Nishati yenyewe ni kiumbe tu kilichoumbwa na Mungu ili kiendeshe mifumo ya ulimwengu.
  2. Kuhusu Mungu kutoonekana, Qur'ani iko wazi sana:
Kwanza hata namna ya jinsi ubongo wa mwanadamu unavyo fanya kazi ni kupitia firing and wiring of neurons, ni nishati ya ubongo inayo kufanya ukumbuke na kuongea haya yote. Zote hizi ziko biologically proven through neuroscience
Swali langu kwako ewe gunner ni hili

Ikiwa sisi ni 'more complex animals' tu kama unavyosema, kwa nini katika spishi zote mamilioni za wanyama, ni binadamu tu mwenye kiu ya kutafuta maana ya maisha, haki, usawa, na uhalisia wa mambo (existential dread)? Mnyama gani mwingine ana 'vibration' inayomfanya alie kwa sababu tu ametafakari kuhusu kifo au ulimwengu? Hiyo nishati yako kwa nini imemchagua binadamu pekee kuwa wa kipekee hivi?"
Maana ya maisha ndo maisha yenyewe wewe unategemea kiumbe kingine na kiumbe kingine kinakutegemea wewe. Unazaliwa, una reproduce na unakuta.

Hizo maana nyingine ni psychological na hazina maana kubwa bali kufurahisha ego zetu tu. Utafanya makubwa yatabaki kama kumbukumbu lakini binadamu anacho kujali ni survival yake tu basi.
 
Naona umesoma historia lakini umeisoma kwa upande mmoja, na unanisingizia vitu ambavyo mimi sijavisema.

1. Suala la Lugha: Hukuelewa nilichosema
Mimi sijawahi kusema kuwa 'lugha ya Kiislamu (Kiarabu) ilikuwa ya kwanza kwa dunia nzima'—hapo unanisingizia. Nilichosema ni kwamba uwezo wa kuzungumza (the faculty of language) upo kwenye DNA ya binadamu tangu anaumbwa. Binadamu wa kwanza hakuwa bubu kama nyani; alikuwa na lugha yake kulingana na mazingira yake.
Uislamu hautukuzi lugha moja tu ya Kiarabu na kusema ndio asili ya lugha zote. Qur'ani iko wazi kabisa kuwa utofauti wa lugha zetu zote duniani (ikiwemo za Kiafrika na Kimisri) ni ishara ya uumbaji wa Mungu! Allah anasema:

Kwa hiyo, kuwepo kwa lugha tofauti za Kiafrika hakupingi Uislamu, bali kunathibitisha kile kilichomo ndani ya Qur'ani.
Nani aliye kudanganya kuwa watu huu mbwa wakiwa wanajua lugha?

Lugha ni kitu najifunza tu, hakuna anayejua lugha. Mtu akizaliwa na wanyama atakuwa. Mzuri tu katika kupiga sauti za hao wanyama na asije lugha yoyote. Lugha ni by product ya conditioning ya mazingira yako, najifunza cues na namna ya kuongea through mimicking your parents, hakuna jipya katika hilo.

Sasa kama lugha ya kiialam(kiarabu) nimekuja baadae what makes you think Mungu wa Dini yako ni wa dunia nzima? Na kama sio wa Dunia nzima so kuna mungu wengine kutoka Africa na Asia?

Mbona logic ndogo tu kujua kuwa Dini ni utapeli Inakushinda?
 
unabishana na science sasa
 
Ndugu yangu, nakuomba utulie na usipaniki mpaka ufikie hatua ya kuita dini 'utapeli'. Kwenye mjadala wa kiakili, anayepaniki na kuanza kushambulia ndiye anayeonekana ameshindwa hoja. Hebu twende taratibu nikuonyeshe jinsi unavyochanganya mambo ya sayansi ya lugha na misingi ya dini
 
Lugha ni kitu najifunza tu, hakuna anayejua lugha. Mtu akizaliwa na wanyama atakuwa. Mzuri tu katika kupiga sauti za hao wanyama na asije lugha yoyote. Lugha ni by product ya conditioning ya mazingira yako, najifunza cues na namna ya kuongea through mimicking your parents, hakuna jipya katika hilo.
Tuanze na hii hoja yako:

Hapa inaonesha wazi kuwa hujui tofauti ya "Uwezo wa Lugha" na "Msamiati"

Umesema: 'Mtu akizaliwa na wanyama atakuwa anapiga sauti za wanyama tu, hakuna anayejua lugha tangu kuzaliwa.'
Hapo unazungumzia watoto wanaoitwa Feral Children (waliolelewa porini). Lakini unashindwa kutofautisha kati ya Uwezo wa Kibiolojia wa kuunda lugha (Language Acquisition Device) na Kujifunza maneno (Vocabulary).
  • Sayansi ya Lugha (Linguistics): Mwanasayansi maarufu duniani,ambaye amepewa cheoncha father of Modern linguistic, Noam Chomsky, alithibitisha kuwa binadamu anazaliwa akiwa na programu maalum kwenye DNA yake (Universal Grammar) inayomuwezesha kuunda mifumo tata ya lugha yenye viunganishi na sarufi (grammar) — kitu ambacho mnyama hana.
unaweza kusoma tafiti zake kuhusiana na hili suala.

Chomsky, N. (1957). Syntactic Structures. The Hague: Mouton.

  • Ukimchukua mtoto wa sokwe ukamfuga ndani ya nyumba ya binadamu kwa miaka 20 na ukawa unamfanyia conditioning na mimicking kila siku, hatawahi kuongea lugha ya binadamu. Kwa nini? Kwa sababu hana hiyo programu kwenye DNA yake. Lakini binadamu akikaa na binadamu wenzake, hiyo programu inajiwasha yenyewe. Sisi hatukubishana kuhusu mtoto wa porini; tulibishana kuhusu uwezo wa kipekee wa kibiolojia alionao binadamu pekee ambao wanyama hawana.
Katika Uislamu, uwezo huo wa kuchambua na kueleza mambo kwa lugha ni uumbaji maalum wa Mungu:

"Mwingi wa Rehema. Amefundisha Qur'ani. Amemuumba mwanadamu. Amemfundisha kubainisha (kuzungumza kwa ufasaha)."

(Surat Ar-Rahman: 1-4)
 
nimekuja baadae what makes you think Mungu wa Dini yako ni wa dunia nzima? Na kama sio wa Dunia nzima so kuna mungu wengine kutoka Africa na Asia?
Ukaleta hoja yako nyingine

Je, Mungu wa Uislamu ni wa Waarabu Tu? (Hapa umenithibitishia kuwa una uelewa Mdogo wa Dini)

Umeuliza: 'Kama lugha ya Kiarabu imekuja baadaye, kwa nini unaona Mungu wako ni wa dunia nzima? Kwani kuna miungu wengine wa Afrika na Asia?'
Hapa unaonyesha kutofahamu kabisa msingi wa Uislamu. Allah sio Mungu wa Waarabu; Yeye ni Mungu wa kila kitu (Rabbil 'Alamin).

Kiarabu ni lugha tu iliyotumika kushushia Kitabu cha mwisho (Qur'ani) kwa sababu Mtume wa mwisho alizaliwa uarabuni. Kitabu kikitokea lazima kitumie lugha moja wapo ya hapa duniani ili kieleweke.

Uislamu unatufundisha kuwa Mungu hakutuma Mitume uarabuni tu. Alituma Mitume katika kila taifa duniani (ikiwemo Afrika na Asia) na waliongea lugha za huko huko! Qur'ani inasema:

"Na hatukumtuma Mtume yeyote ila kwa lugha ya watu wake ili apate kuwabainishia..." (Surat Ibrahim: 4)

Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume (akisema) kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa Mwenyezi Mungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.
"(Surat An-Nahl: 36)
Kwa hiyo, hakuna 'Mungu wa Kiafrika' wala 'Mungu wa Kiarabu'. Mungu ni Mmoja yuleyule aliyetuma ujumbe kwa mababu zetu wa Kiafrika kupitia lugha zao za kale, na akatuma ujumbe uarabuni kwa Kiarabu. Tofauti ni kwamba, ujumbe wa zamani ulikuwa wa makabila fulani tu, lakini Qur'ani ndio ujumbe wa mwisho uliotumwa kama Ukurasa wa Mwisho kwa dunia nzima.
 
Mbona logic ndogo tu kujua kuwa Dini ni utapeli Inakushinda?
Swali Langu la Mwisho Kwako (Ambalo Unalikwepa):
Kama dini ni 'utapeli' na vitabu vilitungwa tu na Waarabu, mbona mpaka sasa umeshindwa kunijibu: Mtu wa miaka 1,400 iliyopita jangwani (Muhammad) alijuaje siri za kiakiolojia za Misri ya kale — kama jinsi Farao alivyotumia udongo wa mfinyanzi uliomwagiwa moto (Baked Clay) kujenga minara yake, na akataja jina la waziri wa ujenzi aitwaye Haman?
Vitu hivi vimegunduliwa na sayansi ya kisasa juzi tu baada ya kusoma maandishi ya kale ya hieroglyphs. Kama Muhammad alikuwa tapeli wa kawaida tu aliyekaa chini akatunga kitabu, alizitoa wapi data hizi za siri za miaka 3,000 kabla yake?
 
Back
Top Bottom