Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu


Mungu huyo ni stori za vijiwe vya kahawa unamuadhibu vipi mtu unayejua mwisho wake ni motoni ina maana unaumba makusudi ILI upeleke watu motoni? Halafu anakujaribu na hapo hapo anajua utafeli anajitekenya mwenyewe na kucheka

Mungu ajuaye yote, mwenye nguvu zote, upendo wote hayupo sababu dhana ya kuwepo kwake inamkanganyiko.
 
Tatizo unataka Mungu awe kama wewe unavyotaka, Je mfano Roboti akishindwa kufanya kazi si utamharibu?

Au Roboti anayefanya kazi ila kwa ufanisi wa asilimia 70%-90% si utataka kumuiprove awe Bora zaidi?

Mungu atamu-modify binadamu ambaye si mkamilifu na WA kufa Ili aweze kukamilika na kuishi milele, ameshafanya utangulizi wa hili kupitia kifo na ufufuko wa Yesu Kristo.

Ila naona unataka kumuongelea Mungu wa Spinoza, Mungu ambaye yeye hana time na mwanadamu, na wala hamuadhibu binadamu kwa dhambi zake.
 
Uzi unatakiwa uchanje mbuga kwa michango pia ya wachangiani. Hata hivyo hakuna sababu ya kupoteza nguvu nyingi kujibizana na wale wanaosema hakuna Mungu.
Mfanya research katika huu uzi unajitosheleza kuna jamii mbili katika research yake kama alivyo ainisha. Na nguvu zao zina source mbili tofauti zinazowa- back.
Katika uumbaji kuna hatua nyingi kuweza kufikia dhumuni la ukamilifu wa kile unachitaka kukiumba. Unaogopa kufa kifo cha mwili? Wala haina haja kuogopa hicho kwani madhumuni ya aliyekuumba ni kukuleta katika state ya juu zaidi ya hiyo uliyo nayo.
Umeshaona wale wanaochakata dhahabu au almasi? Inasagwa na kupondwa ikiishapitiswa kwenye moto mkali sana na halafu kisha material nyingine zote zilizokuwa zimegandamana nayo zinateketea kwa moto. Likichukuliwa sasa lile jiwe la thamani lililostahimili tanuru kali ya moto ndiyo linachongwa shape ya anachotaka muumbaji. Likiisha chongwa utaliona likiakisi rangi saba za upinde.
Mungu yeye hakutuhurumia kwa namna ile sisi tunavyoitafsiri huruma bali katika namna yake yeye mwenyewe.
Alimwingiza mwana wake Yesu katika miili hii tuliyo nayo na akapitia katika mateso yale yaliyo kawaida ya kibinadamu bila kutenda dhambi. Na aliposhinda na kufufuka ndio katoka anang'aa kama dhahabu iliyopitishwa kwenye moto wa tanuru na kutoka safi.
Sasa anamiliki juu ya uumbaji wote katika ulimwengu huu wa material na ule wa roho.
Mwanafunzi anapofundishwa na mwalimu kwani mwalimu hajui uwezo wa kila mwanafunzi hata awape mtihani?
Mtihani ni tendo la ku-justify hukumu kwa haki.
 
Kwa hiyo Mama yake Yesu yaani bikira Maria aliyemzaa Yesu alikuwa anamuitaje?
(a)Mwanangu na Yesu anamuita Mama
(b) Au alikuwa anamuita Mungu, maana yake alimzaa Mungu?Naomba jibu
 
🤣💔Hebu usituletee story zako za uwongo na porojo za kichawi Chawi hapa...sisi watu wazima ujue
 
Fanya hivyo right now. Nishaomba mara nyingi sana nirogwe ila hadi leo nadunda tu
Mbona umesharogwa? Unajiona unadunda wala hudundi🤣🤣🤣! Shetani kakufunga ufahamu, umekosa maarifa ya kimungu na wala hutaki kujua! Umerogwa, hawana shida ya kukuroga maana wewe ni wa kwao tayari!
Kama si hivyon basi inawezekanapia huna wanachotaka! Wewe ni makapi!
 

Katika watoto 100 darasani mwalimu anaweza kupanga wakwanza mpaka wa mwisho kabla hajawapa mtihani? Jibu ni haiwezekani lakini anaweza kuhisi wa kwanza wa pili au hata wa mwisho, lakini hawezi kupanga mwanafunzi wa kwanza atakuwa huyu mpaka wa mwisho atakuwa fulani.huyo mwalimu hayupo

Lakini mungu mjuzi wa yote ambaye anakufahamu kabla ya kukuumba anafahamu mpaka mwisho wako. Halafu mungu huyo huyo anayejidai kufahamu mpaka mwisho wako anakujaribu ingali anafahamu wewe ni wa motoni!! Wonderful
Anataka kuprove nini cha tofauti kutoka kwako wakati anafahamu kipindi hata hajakuumba? Utaona ni stori za vijiweni

Huo mfano wako wa mwalimu ni mfano wa ovyo hakuna mwalimu alifahamu wewe ukitoka primary utaenda sekondari aliyopo yeye halafu mwalimu huyo akafahamu watoto 100 watakaofika hapo halafu akafahamu katika watoto hao 100 wakwanza mpaka wa mwisho atakuwa nani. Hayupo

Hakuna mungu, kama yupo thibitisha
 
wewe ni mlokole ?🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…