Napata shaka kama ulimuona huyo MUNGU wa walokole...
Mbona umetumia Mnajimu? Maana Mnajimu huyo ni Mkuu wa giza...
Kumuona Mungu sio kwa kutumia mtu na nguvu za kibinadamu.
Bali ni kwa kumpokea Bwana kuwa mwokozi wa maisha yako, kuomba, kufunga, kusali...
Na hii ndio maana wapo ambao wanaenda kanisani kila siku ila hawaoni mambo ya Rohoni...
Wanajiita wakristo lakini YESU hawajui...
kumbuka kisa cha mnajimu na sauli,sauli alitaka kumpandisha samweli na kweli samweli alikuja ijapokuwa alishakufa na akamkemea na kumtabiria kifo chake so wanajimu wanauwezo wa kutambua yaliyo ya Mungu.
Lakini pia mamajusi(wanajimu)wa mashariki walitambua kuzaliwa kwa Yesu kupitia nyota.
13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi.
1 Samweli 28:13
14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.
1 Samweli 28:14
15 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.
1 Samweli 28:15
16 Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako?
1 Samweli 28:16
17 Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi.
1 Samweli 28:17
18 Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo.
1 Samweli 28:18
19 Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti.
1 Samweli 28:19