Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Hapo hujakosea,kweli kuna tofauti. Mfano mungu wa waislamu wanasema hana mwana na Yule wa walokole Ana mwana. Mungu wa waislamu anawaambia wafuasi wake wafunge mwezi wa Ramadan na Mungu wa walokole anawaambia wafunge bila kujionyesha au kujitangaza kuwa wamefunga.Tofauti ni nyingi sana,hata namna ya kusali iko tofauti sana,walokole wanalia,waislamu hawalii.
Hata kwenye ulimwengu wa roho,ni vitu viwili tofauti
 
Hata kwenye ulimwengu wa roho,ni vitu viwili tofauti
Nina maswali mengi, ila nianze na Hili. ...

Ulisema hao watu warefu wakikugusa Ile alama haifutiki. Na ukasema katika ulimwengu wa roho inaonekana.Ina maana Ile alama wachawi wanaiona muda wote? Na wachawi wakiiona wanafanyeje? Wanaiheshimu Ile alama au mtu mwenye Ile alama? Au wanamfanyia ubaya? Au Ile alama inawaogopesha wachawi?
 
Pole sana,

Kama Hadi sasa hujaelewa kuwa Mungu Baba, Mungu mwana na Roho mtakatifu ndiye huyo huyo YESU KRISTO, Bado una safari ndefu.

Ila nakuombea ufike Kwa Uweza wa Mungu.
Mitume wote waliopi
Hapo hujakosea,kweli kuna tofauti. Mfano mungu wa waislamu wanasema hana mwana na Yule wa walokole Ana mwana. Mungu wa waislamu anawaambia wafuasi wake wafunge mwezi wa Ramadan na Mungu wa walokole anawaambia wafunge bila kujionyesha au kujitangaza kuwa wamefunga.Tofauti ni nyingi sana,hata namna ya kusali iko tofauti sana,walokole wanalia,waislamu hawalii.
poleni sana
 
Tatizo mnashindwa kujibu maswali mepesi kama hayo,utaweza kuwafundisha watu vitu vigumu?dini siyo ya kukalilishwa labda nikuulize tena swali jingine Yesu alikuwa Dini gani?mimi nataka vitu vikubwa
Ukiniuliza kwa mujibu ya Islamic conception sitakujibu.Yesu alikuwa Myahudi
 
Labda nikusaidie kujibu Sifa za Mungu
(1)hakuzaliwa wala kuzaa
(2)Haonekani,hakuna aliyewahi kumuona,ila Musa alisikia sauti yake
(3)hana mwanzo wala mwisho,yaani hawezi kufa
(4)Yeye ni wa pekee hana msaidizi katika kazi zake,na dunia aliiumba peke yake,na mwisho wa dunia atarudi na kuwa peke yake inamana hata Yesu pamoja na maraika watakufa
Wewe unataka kutuharibia uzi kwa kuleta schools of thoughts za dini yako.Wee tuache sisi tuburudike na ukuu wa Yesu bwana.
 
Nina maswali mengi, ila nianze na Hili. ...

Ulisema hao watu warefu wakikugusa Ile alama haifutiki. Na ukusema katika ulimwengu wa roho inaonekana.Ina maana Ile alama wachawi wanaiona muda wote? Na wachawi wakiiona wanafanyeje? Wanaiheshimu Ile alama au mtu mwenye Ile alama? Au wanamfanyia ubaya? Au Ile alama inawaogopesha wachawi?
Umeuliza maswali ya msingi sana...
 
Tupo sifa za Mungu wako wewe, ili tupimane uelewa
Kaka wewe endelea kumuabudu Mungu wako ukiangalia Saudia.Sisi Mungu wetu yuko kila mahali hatuna haja ya kugeukia kokote.Mungu wetu huapa kwa jina lake na si vinginevyo.Halinganishwi wala hapimani na Mungu wako.
 
Nina maswali mengi, ila nianze na Hili. ...

Ulisema hao watu warefu wakikugusa Ile alama haifutiki. Na ukasema katika ulimwengu wa roho inaonekana.Ina maana Ile alama wachawi wanaiona muda wote? Na wachawi wakiiona wanafanyeje? Wanaiheshimu Ile alama au mtu mwenye Ile alama? Au wanamfanyia ubaya? Au Ile alama inawaogopesha wachawi?
Mi kutokana na expiriencee naami unakua target Yao ndio lkn ushindi unakua kwako, ni kama umevishwa kombati kwenye uwanja WA vita , manake unakua target ya maadui ila msaada WA ushindi upo na ndio maana Mungu anapewa utukufu kwa kule kutusaidia kushinda
 
INAENDELEA............
Sasa Mzee Matata akaja na mbinu zake za kinajimu za kunifundisha jinsi ya kukariri majira ya anga kama wanavyofanya wale watu warefu kuweza kupaa.Akaendelea na somo lake kua kinachowapaisha sio mabawa au mazingaombwe bali kusoma na kuelewa na kukariri majira ya anga.Lengo letu ni kupeleleza na kupata majibu ya udadisi wangu,sasa ikabidi tuanze kujifunza mbinu mpya nje ya ulimwengu na cha kwanza kabisa kujifunza kupaa.
Siku hiyo mchana kweupe mwalimu na mkufunzi wangu mzee matata akanichukua mpaka barabarani ambayo watu wanapita kama kawaida.Akanipa kombe nikanywa na yeye akanywa afu akasema hapa sasa hatuonekani.Akakaa chini aanze kutoa vifaa kazi anifunze kupaa kwa hesabu za kinajimu,mara tukasikia sauti""Hivi nyie mna akili kweli""alafu kikafuatia kicheko.Yaani mnaloga mpaka kwenye kikao chetu wajinga nyie.Eeeh kuangalia kumbe lile eneo ni eneo la kikao cha wazee wa jadi,nao walikua na mambo yao mchana ule.Mzee matata akageuka ndipo nikaona wazee kumi na saba wakiwa wamevaa lubega zao za kahawia na nyeusi walikua eneo lile wanazindika mambo yao.Wakahoji nyinyi wakurungwa mnafanya nini hapo?????,Mzee matata akawasalimia kwa heshima na kusema nipo na kijana wangu tunapata darasa la elimu anga.Wakamuuliza nani kawapa ruhusa na yeye mzee matata kabla hajawajibu nikasikia kishindo""Puu"na wale wazee kila mtu mbio barabara nzima ikabaki nyeupeee🤣🤣.
Nikabaki mimi na mzee matata nae kakimbia🤣🤣.Kumbe bhana alikua anapita mlokole barabarani mda ule yupo na mtu mrefu pembeni yake,sababu pale palikua ni barabarani afu mchana tu watu wanapita.Bas bwana wale wazee wa vilinge wakatimua kona kidogo nibaki kucheka.Mm nipo pale nashangaa shangaa mara mzee matata huyo katokea na kuniambia""Kijana wangu wale wazee wa tambiko wasingetuingilia tungekua hewani mda huu"""Nikamuuliza kwanini walikimbia,akanijibu kua walikua wanamkimbia yule mlokole na kampani yake ya mtu mrefu.Akasema zoezi limeshaingia gundu tuhairishe mpaka siku nyingine.Mda ukasogea na utafiti wetu ukaendelea ila suala kujaribu kupaa halikufanyika tena.Kuna kipindi nilikua mkoa wa pwani nikakutana na mzee mmoja na yeye pia ni mnajimu nikamdokeza dokeza ila sio moja kwa moja issues hizi naye akanielezea mengi nitafunguka huko mbele.
Bas mzee matata akaniambia unajua kufanya utafiti wako kwa vitendo ni hatari zaidi sababu unaingilia himaya za watu,,kwanini usichague upande mmoja????? Maaana duniani kuna himaya mbili kubwa.Haya maoni ya mzee Matata ndio kama yakanifungulia udadisi zaidi.Kwanini wale wazeee walimkimbia mtu mrefu na kwanini mzee matata anamkimbia pia mtu mrefu.Maswali juu ya maswali nikapambana niyatafutie ufumbuzi.Unajua haya mambo ya udadisi wa mazingaombwe yapo hivi,jinsi unavyojua zaidi ndio jinsi unavyokua na hamu ya kujua zaidi ya pale ulipokomea.
NITAENDELEA.........!!!
 
Huwezi kuamshwa na Yesu, wakati aliyekuumba Mungu, na ndiye aliyekumba, na ndiye atakayekufisha, na ndiye atakayekufufua na ndiye atakayekuhukumu siku ya hukumu

Kwa rehema zake, atakuingiza peponi au motoni
 
Mkuu kila mtu ana mapokeo yake kutokana na imani yake.Wakrsto wao mungu wao ni Yesu na baba yake Mungu Jehovah ni mapokeo yao na huwezi kuwabadili..Sawa na wewe na mapokeo yako hayo uliyoandika juu hawawezi kukubadili na nyote mpo sawa kimapokeo kutokana na imani zenu mlizorithishwa na wazee wenu..Nimekujibu kibinadamu zaidi ila sio kinajimu.
 
Nina maswali mengi, ila nianze na Hili. ...

Ulisema hao watu warefu wakikugusa Ile alama haifutiki. Na ukasema katika ulimwengu wa roho inaonekana.Ina maana Ile alama wachawi wanaiona muda wote? Na wachawi wakiiona wanafanyeje? Wanaiheshimu Ile alama au mtu mwenye Ile alama? Au wanamfanyia ubaya? Au Ile alama inawaogopesha wachawi?
Nitakujibu mkuu....Huu uzi twendeni taratibu hakuna anaetukimbiza...Sawa mkuu
 
Mkuu kila mtu ana mapokeo yake kutokana na imani yake.Wakrsto wao mungu wao ni Yesu na baba yake Mungu Jehovah ni mapokeo yao na huwezi kuwabadili..Sawa na wewe na mapokeo yako hayo uliyoandika juu hawawezi kukubadili na nyote mpo sawa kimapokeo kutokana na imani zenu mlizorithishwa na wazee wenu..Nimekujibu kibinadamu zaidi ila sio kinajimu.
Kuna vitu vingine inabidi ufikilie kwa akili ya ubinaadamu siyo lazima uende shule ukasoma, nafasi ya Mungu kwa binadamu ni kila kitu, yeye alikuwepo, yupo, atakuwepo daima.

Pole sana ndugu yangu, lakini ujuaji wetu huu wote mwisho wake ni kaburini, halafu Mungu mwenyewe kaweka pazia, kiasi kwamba hatuna nafasi ya kuludi tena kuja kusahihisha makosa yetu
 
Popote pale mkuu,,walokole wanasali na kulia hata kimoyo moyo wakiwa popote pale.Wakija wale watu warefu wanakaa pembeni yao wanawaangalia kwa huruma kama wanataka wawakumbatie hivi.

Na walokole wakizidi kulia kwa kusali na wale watu warefu wanaongezeka na eneo zima linazungukwa na moto wa blue tupu.Lakini duniani walokole sio wengi hawazidi milioni kumi,,ni wachache chini ya hapo.
Kwanini unasema walokole duniani hawazidi milioni kumi ikiwa kila mahali duniani kuna makanisa mengi ya kilokole.
 
Napata shaka kama ulimuona huyo MUNGU wa walokole...

Mbona umetumia Mnajimu? Maana Mnajimu huyo ni Mkuu wa giza...

Kumuona Mungu sio kwa kutumia mtu na nguvu za kibinadamu.

Bali ni kwa kumpokea Bwana kuwa mwokozi wa maisha yako, kuomba, kufunga, kusali...

Na hii ndio maana wapo ambao wanaenda kanisani kila siku ila hawaoni mambo ya Rohoni...

Wanajiita wakristo lakini YESU hawajui...
kumbuka kisa cha mnajimu na sauli,sauli alitaka kumpandisha samweli na kweli samweli alikuja ijapokuwa alishakufa na akamkemea na kumtabiria kifo chake so wanajimu wanauwezo wa kutambua yaliyo ya Mungu.
Lakini pia mamajusi(wanajimu)wa mashariki walitambua kuzaliwa kwa Yesu kupitia nyota.
13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi.
1 Samweli 28:13

14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.
1 Samweli 28:14

15 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.
1 Samweli 28:15

16 Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako?
1 Samweli 28:16

17 Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi.
1 Samweli 28:17

18 Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo.
1 Samweli 28:18

19 Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti.
1 Samweli 28:19
 
Back
Top Bottom