Uyu hapa
JF-Expert Member
- Oct 14, 2021
- 394
- 476
Alibarikiwa kuwa na maseyidi kumi na mawili. Ndio baba wa makabila ya kiarabu. Pia alifanywa kuwa taifa kuu. Lakini baraka ya agano ilobebwa kwenye tumbo la Sara na sio Hajiri.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alibarikiwa kuwa na maseyidi kumi na mawili. Ndio baba wa makabila ya kiarabu. Pia alifanywa kuwa taifa kuu. Lakini baraka ya agano ilobebwa kwenye tumbo la Sara na sio Hajiri.
Adui yetu Huwa anatengeneza copy ya kila afanyacho Mungu wetu. Mara zote ameingia kufeli pakubwa mno. Maana shauri la Bwana litasimama milele.mtume alitoka kwenye uzao wa ishmael ambaye mamaake alikua kijakazi wa ibrahim,, wapendwa katika BWANA hii imekaaje kiroho?
Uko sahihi kiongozi wangu [emoji120]Kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 2019 nilikua kwenye research binafsi ya mambo yasiyoonekana kwa macho ya kawaida. Nimefanya mahojiano na watu wa fani hii,kuanzia watu wa kawaida mpaka viongozi wa fani hii katika nyanja mbalimbali.
Mambo yasiyoonekana kwa macho,watu wanaita""UCHAWI""na ni fani yenye kuchanganya kidogo sababu inajumuisha imani za dini za wanadamu na imani za dini zisizo za wanadamu. Pia inajumuisha watu ambao wanaitwa bin-adamu na inajumuisha watu wale wengine ambao hawana undugu na hawa watu wanaoitwa bin-adam.Nielezee kidogo hao watu wengine,nimewaita watu sababu wana maumbo kama binadamu ila vimo vyao vipo tofauti na wapo katika jamii mbili tofauti.
Kuna ile jamii ya wanaokaa angani ambapo bila ruhusa yao huwezi kuwafikia,na kuna ile jamii ambayo hata bila ruhusa yao unaweza kuwafikia na wanakaa chini ya bahari au mito au maziwa makubwa(Lakes).Ngoja nifafanue kidogo jamii za hawa watu.
Jamii ya watu wa angani inashuka sana duniani na sijui waga wanakuja kufanya nini ila mara nyingi wanajishugulisha na wale binadamu mnaowaita walokole,na ili uzungumze nao inategemea umekutana nao katika hali gani kwenye ulimwengu usio wazi kwa macho ya kawaida,kiasili sio waongeaji sana ila sura zao zinaakisi mwanga kwa namna ya tofauti na unaweza kujiuliza wanavaa mavazi gani, kwa mavazi wanavaa hizi nguo mnaita kanzu ila ni bwanga afu ndefu mpaka miguuni na ni nyeupe.
Jamii ile nyingine ya watu wasio na asili na binadamu ila wamefanana na binadamu kimuonekano lakini wana vimo vikubwa ni ile inayokaa chini ya bahari,maziwa(Lakes) na mito.Hii jamii wao ni wazungumzaji sana afu miili yao haiakisi mwanga na wanakuja sana duniani na unaweza kuwaona bila ridhaa yao kwa kufuata utaratibu wanaokupa wafuasi wao au wanajimu wa nyota mbao ni binadamu wa kawaida,na mavazi yao ni kanzu pia ila za rangi mbalimbali zaidi ya nyeupe.Na watu wanaojishugulisha nao sana ni wale watu ambao nyinyi binadamu mnawaita wanajimu na washirikina au wachawi ila inategemea ushirikina na uchawi wa wapi maana dunia ni kubwa kutoka bara moja mpaka lingine na ushirikina au uchawi unatofautiana.
Binadamu kuna vitu huwezi kuviona mpaka either uwe mshirika wa jamii mojawapo kati ya jamii hizo mbili nilizokutajia hapo juu.Lengo langu leo ni kuzungumzia mkuu wa jamii ile ya wale watu wa angani ambao wanapenda kushirikiana na walokole au watu wa kulia lia,maana huyo mkuu ana vitu vya tofauti kidogo ndio maana nikasema pale juu kua "Mungu wa walokole ana nguvu sana".
Katika utafiti wangu ndani ya ulimwengu usio,onekana inaonyesha kua walokole wanapendelewa sana na huyo mkuu wao,maana kuna vitu anawapa vya ziada wao hawavitumii sijui kwanini niligundua hilo huko mbele katika utafiti wangu.Nimemuita Mkuu au Mungu wa walokole sababu kila walokole wanapoanza kulialia""Kusali""wale watu wa jamii ya kuakisi mwanga wengine wana mabawa na wengine hawana wakitokea kwa mkuu wa walokole ama nilivyokuja kujua baadae huko huko angani wanawajia na wanawazunguka hawaondoki na lile eneo husika linakua na mwanga unaweza kupofusha macho (Ni kama mwanga wa jua au radi au shoti za umeme zile cheche) ila walokole waga hawawaoni nadhani waga wanalia(Kusali) kwa imani zaidi namaanisha meditation.
Nilisema hapo juu kua mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao ana nguvu sana maana wale walokole baada ya kulia kwa mkuu wao huwezi kuwasogelea katika hali ya nje ya ubinadamu au katika hali ya ushirika na jamii nyingine za kiroho zaidi ya mkuu wao na wale watu wa kuakisi mwanga.Kila mlokole anakua na yule mtu wa kuakisi mwanga na yule mtu haongei ila macho yake ni ishara tosha kua usimsogelee mlokole aliyenae.Cha ajabu wengi ya walokole hao katika hali ya ubinadamu wa kawaida hawana habari yoyote ile unawakuta sokoni au kwenye daladala au barabarani au ofisini au kwenye nyumba zao za ibada.
Sasa ikabidi nifanye uchunguzi juu ya huyo mkuu (Mungu) wa walokole,yupoje na ni nani, wale watu wa jamii ya kuakisi mwanga wanaishi nae vipi maana wana ushirika nae.Sababu ukitoka nje ya mwili kupitia(meditation) huwezi kuwasogelea hawa watu wa jamii ya kuakisi mwanga au hao walokole.Nikajikuta napata hamu ya kuchunguza mambo ya ulimwengu usionekana na hasa jamii za wale watu warefu wa angani na walokole hasa wale wa kulialia sisi binadamu tunaita kusali ila wao walokole wanaita kunena kwa lugha,na ni lugha ambayo inawafanya wawasiliane na wale watu warefu wa kuakisi mwanga.
Udadisi wangu ulijikita katika mambo makuu matano(5)
Mosi: Kwanini walokole wana uhusiano na wale watu wa kuakisi mwanga wanaotokea kule juu kusikofikika hata ukitoka nje ya mwili na kusafiri nje ya mzunguko wa sayari za kawaida kwa maelekezo ya wanajimu wa nyota?
Pili: Kwanini mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao ana uhusiano wa moja kwa moja na wale watu wa kuakisi mwanga na sio ile jamii ya chini ya bahari?
Tatu: Kwanini katika jamii za nje ya mwanadamu au mtu, hasa ile jamii ya watu wa kuakisi mwanga ina nguvu sana kuliko jamii za wale watu wanaokaa chini ya bahari na wasioakisi mwanga wa jua na mwezi?
Nne: Mkuu wa walokole kwanini yeye na wale watu wa kuakisi mwanga,hawana ukaribu na Mkuu wa wale watu wa jamii inayokaa baharini na chini ya maziwa na mito(Maana nayo ina mkuu wake) na hataki wafuasi wake wa dini yake wawe na ukaribu na walokole kwa namna yoyote ile?
Tano: Kwanini mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao pamoja na nguvu zoote ila hawapi utajiri wa kibinadamu hao walokole ila ukitoka nje ya mwili hawa walokole wana nguvu sana mpaka uñashindwa kuwaelezea labda uone kwa macho.Tofauti na mkuu wa ile jamii nyingine ambayo karibia robo ya wafuasi wake wana access ya kupata mali za dunia hii tunayoishi binadamu wote.
Basi nikajikuta naanza utafiti kufuatilia nguvu za mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao.Ni nani na yupoje na anaishi wapi..Utafiti wangu ukanipelekea kuja na kichwa cha habari hapo juu kua Mungu wa walokole ana nguvu sana maana nilishuhudia mengi kumuhusu huyu Mungu wa hawa watu wa kulialia mnawaitaga walokole.
Safari yangu ya utafiti ilinikutanisha na wazee wa kibantu,wanajimu,viongozi wa dini za wanadamu zinazoonekana na zisizoonekana na watu wa jamii zile za nje ya ulimwengu wa mwanadamu.
ITAENDELEA
hapo nimekuelewa mkuuAdui yetu Huwa anatengeneza copy ya kila afanyacho Mungu wetu. Mara zote ameingia kufeli pakubwa mno. Maana shauri la Bwana litasimama milele.
Amen,Ubarikiwe
Napokea Baraka hizo,Kwa Mikono yote, nakushukilu Sana , kwakunitakia Baraka ,Ubarikiwe
Napokea Baraka hio ,Kwa jina lake kuu yesu kristo,Ubarikiwe Uyu hapa
amina!Napokea Baraka hio ,Kwa jina lake kuu yesu kristo,
Mtu ,anapokubariki ,kama wewe ulivyo nibariki sio swala la kuchukuliwa masihara,
Maana ni moyo wa MTU umekubariki,
Na unaelewa moyo unapotowa hazina yake ya baraka,kwenda Kwa mwingine, yaani unapokerewa na moyo wangu,
Unasafirishwa kwenda Rohoni hio baraka na inakaa rohoni Kwa Ile Imani ya moyo wangu ,na huku mwilini inakuja kunipa kibari Cha kufanyika baraka wa watu wote.
Toka nijitambue ,hakuna baraka ninayoiacha kimasihara,
YAKOBO ALIIPANBANIA BARAKA MARA MBILI TENA KWA MBINDE, MPAKA MOJA WAKAGOMBANA NA KAKAE NA NYINGINE NGUMI HASWA MPAKA AKATEGUKA ,KISA BARAKA HIIHII , UNAYO NIBARIKIA KWA BURE KABISA,
ASANTE,
NA WEWE PIA UBARIKIWE
Safi Sana, nimesoma ushuhuda wa kitabu Nika Kumbuka kijana wangu pia alipata muujiza kama huo, maana alipoteza akiwa likizo na alipokua a arudi shule ndio kastuka hanacho, alilia Sana, tu kamwambia mlilie Mungu anajua kilipo, a kaenda shule alipokua a natoa madaftari anasema akakiona ktk ya madaftari akafurahi yaani katoka shule anashuhudia kakwepa fimbo kwa Muujiza huu... Asee kumwamini Mungu raha Sana... Kamanda Rudi tu kwa Mungu, haja kuacha Bali umemuacha na yeye anakutamani Sana uwe mwanawe Tena.. Njoo kwa Yesu!Mwanzo ulipokua unasema walokole walokole sikuelewa, niakajua unaongelea makanisa ya kilokole.
Lakini kadri uzi unavyoenda nikaelewa kua watu wanatangatanga na makanisa bure tu, MUNGU yupo popote..
Wakati niko primary nilikua na imani kwelikweli, nikikumbuka enzi zile nilikua tofauto kiimani na watoto wenzangu. Nilikuwa nikimuomba MUNGU kitu kinakua.
Nakumbuka kuna siku nilipoteza kitabu cha hesabu na tulikua tunakaribia kufunga shule, na ticha alisema kama umepoteza kitabu itabidi ulipe na mimi kumwambia mshua naogopa. Basi kuna siku nilisali sana, nililia na MUNGU mno, ajabu kesho yake nilikuta kitabu kwenye begi langu wakati kilipotea kitambo sana.
Kiukweli kipindi kile nilikua na imani sana, nikisali inakua, tena vilevile au zaidi ya kile kwa njia tofauti.
Kwasasa nshakua kijana wa hovyo ila maisha ya wokovu yana raha sana aisee. Ukianza wokovu tangu utoto wako bila kupuliziwa moshi akilini alooo utapata raha maisha yako yote, utakua na stress ila MUNGU atakushangaza.
Mitihani mingi shule nimepass kimiujiza tu baada ya kusali sana.
One day Yes nitarudi kwa miguu yote miwili kwa Muumba.
Imani ni ngao....I remember Kuna siku nlilala nkaota nlikua nimesimamishwa kweny mti Kuna watu walikua wanawapiga watu mishale..ikafika zamu yangu nikawaambia Namuamini Mungu wangu hataniacha yule mtu akasema tumuone huyo Mungu wako sasa...basi akafyatua mshale mshale ukawa unakuja lkn cha ajabu kabla haijanifikia Ile mishale ikawa inapotea Yan anafyatua mshale unakuja Ile unakaribia tu kunipiga gafla mshale unapotea kusikojulikana......Imani ndo Kila kitu shetani akikutafuta Kwa njia tofaut akishindwa anaanza kuishambulia Imani yakoSafi Sana, nimesoma ushuhuda wa kitabu Nika Kumbuka kijana wangu pia alipata muujiza kama huo, maana alipoteza akiwa likizo na alipokua a arudi shule ndio kastuka hanacho, alilia Sana, tu kamwambia mlilie Mungu anajua kilipo, a kaenda shule alipokua a natoa madaftari anasema akakiona ktk ya madaftari akafurahi yaani katoka shule anashuhudia kakwepa fimbo kwa Muujiza huu... Asee kumwamini Mungu raha Sana... Kamanda Rudi tu kwa Mungu, haja kuacha Bali umemuacha na yeye anakutamani Sana uwe mwanawe Tena.. Njoo kwa Yesu!